Sunday, January 31, 2016

Habari kutoka vituo vya televisheni

Serikali wilayani Mbalali mkoani Mbeya imeagiza kupitiwa upya kwa mikataba ya ukusanyaji wa mapato na wazabuni. https://youtu.be/bzL1BxShJrM
Jeshi la wananchi kamandi ya nchi kavu limewataka maafisa wa jeshi hilo kuzingatia weledi katika kufanya kazi zake za ulinzi na usalama. https://youtu.be/mrHG7c36zKE

Wananchi wanaotumia kivuko cha Musoma kutoka Musoma kwenda Kinesi Mkoani Mara maisha yao yako hatarini kutokana na kujaa kwa kina cha maji.https://youtu.be/AxMAiMJ1rjg

Mkuu wa wilaya ya Mbulu mkoani Manyara amepiga marufuku ukataji wa miti bila kupata kibali maalumu cha serikali. https://youtu.be/8wnEU-RYMH8

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu. https://youtu.be/QLNH4PHDCCY

Makamu wa rais Samia Suluhu amesema vita dhidi ya ufisadi na rushwa inapaswa iungwe mkono na wananchi wote. https://youtu.be/WamaGfD2e1w

Shirikisho la Mchezo wa masumbwi limetangaza kuvunja kambi ya timu ya taifa ya mchezo huo ili wachezaji wakajiunge na klabu zao. https://youtu.be/cGK6X4-NP78

Rais Magufuli amemwapisha balozi mnadhimu wa jeshi la wananchi wa Tanzania na makatibu tawala leo Ikulu jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/Wd3uGozHFsI

Serikali imevunja uzio uliojengwa na Hotel ya Indian Ocean View katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam baada ya wamiliki kukiuka utaratibu. https://youtu.be/v0Ymo2_7djI

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam leo ameongoza zoezi la usafi katika maeneo mbalimbali ya jiji licha ya mwitikio mdogo wa wananchi waliojitokeza. https://youtu.be/g14O4VK4zio

Rais Magufuli awaapisha mnadhimu mkuu wa jeshi la Ulinzi JWTZ, Balozi mpya wa Kuwait na makatibu tawala wa mikoa Ikulu jijini Dar. https://youtu.be/RDjK4zJ2WZo

Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa baadhi ya maafisa wa wakuu wa jeshi la wananchi wa Tanzania. https://youtu.be/8O1-Iy1E5CI

Makamu wa rais Samia Suluhu amesema vita dhidi ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma inapaswa kuungwa mkono na wananchi wote. https://youtu.be/2yeA__XRMMs

Serikali imeagiza kufanyika uchunguzi dhidi ya maafisa wake waliohusika katika kutoa hati za ujenzi wa eneo lililohifadhiwa katika ufukwe wa Coco Beach. https://youtu.be/m07RZqjAr6U

Coastal Union yaitandika Yanga bao 2 kwa 0 huku Simba ikiibuka na ushindi wa bao 4 dhidi ya African Sports.  https://youtu.be/s4s61Rko3Mw

Serena Williums wa Marekani ashindwa kufikisha rekodi mpya ya ubora katika tenesi kimataifa baada ya kufungwa na Angelique Kerber   https://youtu.be/zdFzSQJws9c

Rais Magufuli amemuapisha mapema leo  Mh.Venance Mabeyo kuwa  Mnazimu mkuu wa jeshi la kujenga taifa la Tanzania: https://youtu.be/5Fy7P1bc8JM

Rais Magufuli ameagiza kumsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Bariadi kwa tuhuma za ujenzi wa barabara: https://youtu.be/sll8ygNhvxw

Mkuu wa wilaya ya Moshi amemsimamisha kazi mkuu wa shule  baada ya kutokea sintofahamu baina ya wazazi na uongozi wa shule: https://youtu.be/0av9RWj9xz4

Waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Mawenzi mkoani Moshi na kutumbua majipu: https://youtu.be/NdXWEfl1VOI

Serikali imesema itaendelea kuweka juhudi na kusaidia maendeleo ya timu ya wanawake Twiga Stars na kuwa imara: https://youtu.be/F8jbtjAqYMg

Nyota wa soka barani Afrika Mbwana Samatta amesema amefarijika kusajiliwa katika timu ya Genk nchini Ubeligiji:https://youtu.be/u6E2T4zKb0o

No comments: