Friday, January 22, 2016

Dalbit Petrolem yamwaga msaada wodi ya watoto MOI

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed Bakari (katikati) akikata utepe kuashiria kupokea msaada wa vitanda 27 na magodoro yake kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa vichwa na mgongo wazi,vilivyotolewa na Kampuni ya mafuta ya Dalbit Tanzania,hafla hiyo ilifanyika katika wodi ya watoto hao katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha Mkurugenzi Mkuu wa Dalbit Tanzania,Margaret Mbaka(kulia) na Mkurugenzi wa huduma za wauguzi wa Hospitali hiyo Flora Kimaro.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mafuta ya Dalbit Tanzania,Margaret Mbaka( kulia) akimfafanulia jambo Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Mohammad Bakari juu ya msaada wa vitanda 27 na magodoro yake kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa vichwa na mgongo wazi,vilivyotolewa na Kampuni hiyo wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada huo iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za wauguzi wa Hospitali hiyo Flora Kimaro.
Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Patrick Mvungi na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni ya mafuta ya Dalbit Tanzania, Anthony Kagiri,wakibandika stika kwenye vitanda na vifaa mbalimbali vilivyotolewa msaada na kampuni hiyo kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa vichwa vikubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili vyenye thamani ya shilingi Milioni16/-
Mganga Mkuu wa Serikali ,Profesa Mohammed Bakari (Kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mafuta ya Dalbit Tanzania,Margaret Mbaka wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vitanda 27,Magodoro 27 na Televisheni kubwa moja vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 16/-Kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa vichwa vikubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa, Mohammad Bakari (Watatu kutoka kushoto) Mkurugenzi wa huduma za wauguzi wa Hospatali ya Muhimbili,Flora Kimaro wa Nne, na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Dalbit Tanzania Margaret Mbaka, wapili kushoto wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Dalbit Tanzania na Hospitali ya Muhimbili baada ya kukabidhiwa msaada wa vitanda 27 na magodoro yake vyote vyenye thamani ya Shilingi Milioni 16/-Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya mafuta ya Dalbit Tanzania,Margaret Mbaka( kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammad Bakari msaada wa TV wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Vitanda 27 na magodoro yeke vyote vyenye thamani ya shilingi Milioni 16/-Hafla hiyo ilifanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa huduma za wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili, Flora Kimaro.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutoa huduma za kiafya kwa wananchi wake zinazotosheleza mahitaji yao.

Kutokana na hali hii yapo mashirika yasiyo ya kiserikali na makampuni ya kibiashara ambayo yamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha huduma za afya nchini na kuleta faraja kwa wahanga wanaosumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya.

Moja ya kampuni ambayo malengo yake na mtazamo wake ni kuunga mkono jitihada za serikali kuboresha huduma za afya nchini kwa kutoa misaada mbalimbali na kusaidia makundi ya wagonjwa wenye mahitaji ni Kampuni ya mafuta ya Dalbit ya jijini  Dar es Salaam leo imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika wodi ya watoto kitengo cha MOI kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Msaada huo ulikabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Dalbit Margaret Mbaka kwa Mganga mkuu wa Serikalini kwa niaba ya Hospitali hiyo Prof Mohammed Bakari, Kwenye hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo.
Vifaa vilivyobidhiwa ni vitanda 27,magodoro 27 na Televisheni kubwa moja vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 16.

Akiongea muda mfupi kabla ya kukabidhi msaada huo,Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni ya mafuta ya Dalbit Tanzania, Margaret Mbaka amesema kuwa kampuni yake imeguswa na changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya afya nchini hususani upungufu wa vifaa vya kuhudumia wagonjwa mahospitalini.

“Tumeguswa sana na changamoto zilizopo kwenye sekta ya afya mojawapo ikiwa ni upungufu wa vifaa vya kuhudumia wagonjwa mahospitalini ndio maana tumeamua kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya afya kwa kutoa vifaa hivi kwenye wodi ya watoto MOI tukiamini vitasaidia kupunguza uhaba wa vifaa vya kuhudumia wagonjwa”,Alisema Mbaka.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Serikali,Profesa Mohammed Bakari alishukuru kwa msaada huo na kuwataka wadau wengine waendelee kujitokeza kuunga mkono jitihaza zinazofanywa na serikali ya awamu tano katika kuboresha mazingira ya tiba katika hospitali zake zote nchini.

No comments: