Mvuvi Waziri Mfaume ambaye ni mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam alikutwa na mpiga picha leo akishimba shimo kwa ajili ya kuhifadhia uchafu kandokando ya barabara ya Barrack Obama ambayo zamani ilifahamika kwa jina la barabara ya bahari (Ocean Road). Anayeonekana akifagia eneo hilo ni Mama Chiku Hamadi Mkazi wa Mwananyamala.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando akiongea na waandishi wa Habari waliofika katika soko la samaki la Feri jijini Dar es Salaam kuona jinsi usafi wa mazingira ulivyokuwa unafanyika sokoni hapo.
Makatibu wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt .Donan Mmbando (wapili kulia) na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ndg. Jummanne Sagini (watano kulia) wakifanya usafi katika Soko la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam. Wengine walioshirikia kazi ya kufanya usafi ni wafanyakazi wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Donan Mmbando akiongea na wafanyakazi wa wizara hiyo mara baada ya kumalizika kwa kazi ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa wizara hiyo walifanya usafi katika mahabusu ya watoto Kisutu, Makazi ya Wazee ya Nunge, Taasisi za Mifupa MOI na Saratani ya Ocean Road, Hospital ya Taifa Muhimbili, Masoko ya Kariakoo na Feri, na Mbagala Zakhem.Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumaliza kazi ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa wizara hiyo walifanya usafi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakifanya usafi wa mazingira leo katika soko la samaki la Feri ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kufanyika kwa usafi wa mazingira nchi nzima ikiwa ni maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
No comments:
Post a Comment