Mwenyikiti
mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO
Ndugu STANSLAUS PETER akila kiapo kulitumikia shirikisho hilo mbele ya
mwanasheria HAMZA JABIRI leo Jijini Dar es salaam kuanza kazi rasmi ya
kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania
Na Exaud Mtei (msaka habari) wa Habari24 blog
Uongozi
mpya wa shirikisho la elimu ya vyuo vikuu nchini Tanzania TAHLISO
umesema kuwa upo tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dr John pombe
magufuli kwa kasi aliyoanza nayo na kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania
hasa elimu ya vyuo vikuu inakuwa ya ubora unaofaa na inaheshimika nchini
Tanzania.
Makamu Mwenyekiti mpya wa TAHLISO Ndugu JUMA ALLY OMARI akila kiapo leo jijini Dar es salaam
Akizungumza
na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya
kuwasimika viongozi wa shirikisho hilo wapya mwenyekiti mpya wa TAHLISO
Tanzania Bw STANSLAUS PETER amesema kuwa kwa miaka mingi elimu ya juu
nchini Tanzania imekuwa haina ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na
mitaala mibovu,ukosefu wa mokopo kwa wanafunzi wengi jambo
linalowakatisha tamaa wengi kusoma,ambapo amesema uongozi wake umeona
kasi nzuri ya serikali ya awamu ya tano na wapo tayari kushirikiana na
serikali kutatua changamoto za wanafunzi nchini.
Naibu katibu mkuu wa TAHLISO KHAMIS ELLY akiapa leo Jijini Dar es salaam
Mwenyekiti
huyo amesema kuwa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka huu
umeonyesha kuwa serikali ya Magufuli inawajali wanafunzi kwani asilimia
kubwa ya wanafunzi walipata mikopo na wengine wanaendelea kupata mikopo
huku akiwataka wanafunzi kutulia kwani neema kwao inakuja kutokana na
kasi ya uongozi huo mpya pamoja na ule wa serikali ya awamu ya tano.
Katibu mkuu Mtendaji mpya wa Shirikisho hilo SAGOLE WAMBURA akiapa leo
Viongozi
wa TAHLISO wameapishwa leo rasmi Jijini Dar es salaam baada ya uchaguzi
wa Kidemocrasia uliofanyika tarehe 23 mwezi huu na wataiongoza Taasisi
hiyo kwa mwaka mmoja kwa mujibu wa katiba yao.
JOSEPH SHABAN ambaye ni muazini mpya wa shirikisho hilo Akiapa leo
Omary Idd Naibu muazini akiapa leo tayari kulitumikia shirikisho hilo
Mwenyikiti
mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO
Ndugu STANSLAUS PETER akizungumza na wanahabari mara baada ya kuapishwa
rasmi kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini
Wanahabari waliokuwa katika hafla hiyo
Picha za pamoja baada ya kula kiapo kwa viongozi hao wapya wa TAHLISO leo Jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment