Tuesday, December 22, 2015

URUWA WAMEOMBA KUKUTANA NA VIONGOZI WA ZAC, CUF,CCM NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

Katibu mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na viongozi wa mashirkiano ya umoja wa vyama vya UDA, TADEA,UDP,UPDP,na SAU kwa kuwaomba viongozi wa ZEC,CUF,CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili waweze kukutana na kuzungumza pamoja kuhusiana na migoro wa kisiasa nchini humo, ameyasema leo jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda katikati akizungumza na waandishi a habari jijini Dar es Salaam leo, kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti SAU na mjumbe wa URAWU, Yusuf Manyanga, na Mwenyekiti wa Taifa UPDP, Katibu mkuu wa URUWA, Comrade Fahami Dovutwa na kulia ni Naibu Katibu mkuu wa UDP na mjumbe wa URAWU, Izaak Cheyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimksikiliza Katibu mkuu wa chama cha ADA-TADEA, John Shibuda wakati akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Legho jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo Globu ya Jamii.
UMOJA wa Rufaa ya Wananchi (
URUWA
)
unaoundwa na viongozi  wa Mashirikiano ya umoja wa vyama vya UDA,TADEA,UDP,UPDP na SAU (URUWA) wameomba kukutana na viongozi wa  ZAC, CUF,CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hayo yamesemwa na  Katibu Mkuu wa  chama cha ADA-TADEA, John Shibuda wakati akizungumza na waandishi wa habari 
katika Hoteli ya Legho 
jijini Dar es Salaam leo.

Ombi  hilo limekuja  baada ya viongozi hao kutaka kuelimishwa kuhusu sintofahamu ya uchaguzi wa Zanzibar
 na kuwataka viongozi wa zanzibar waache kutoa kauli na matamko ya mivuno iliyo na tija kwa wanchini humo.

Pia Shibuda amesema kuwa wanataka ifahamike kwamba ugomvi wa Akili makini na giza totoro ni mwanga nao wameamua kuwa mwanga na kubaini kilichomo katika hili giza la mabishano kati ya 
ZAC, CUF,CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Wakati huhohuo Shibuda amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuri pamoja na wasaidizi wake wakuu Makamu wa Rais, Samia Suluhu pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuwaunga mkono kwa juhudi zao za utumishi, uaminifu na utiifu kwa ustawi wa maendeleo ya jamii na Taifa.
 

No comments: