Wednesday, December 2, 2015

TPDC YATEKELEZA DHANA YA UWAJIBIKAJI KWA JAMII MKOANI MTWATRA.

Mkurugenzi wa Undelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia Dk. Wellngton Hudson (kushoto), akitoa mfano wa Hundi ya shilingi 15,000,000, kwa uongozi wa Mkoa wa Mtwara na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Ndanda, kuanzia kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, Mkurugenzi wa Klabu ya Ndanda Athuman Kambi na Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Cosmas Luanda.
Mkurugenzi wa Undelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia Dk. Wellngton Hudson (pili kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi 10,000,000 kwa uongozi wa Wilaya ya Mtwara kwa ajili ya kumalizia jengo la Ofisi ya Kata ya Ufukoni, Uongozi wa Wilaya ya Mtwara uliwakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Fatuma Ali (wa tatu kulia), Meneja Mawasiliano-TPDC Marie Msellemu (wa kwanza kushoto).

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kwa kutambua dhana ya uwabikaji kwa jamii (Social Corporate Responsibility) mwishoni mwa wiki limekabidhi msaada kwa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Ndanda na kata ya Ufukoni Mkoani Mtwara. TPDC imefikia hatua hii baada ya kupokea maombi ya uhitaji kutoka kwa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Ndanda na Kata ya Ufukoni Mkoani Mtwara.

Klabu Mpira wa Miguu ya Ndanda imenufaika na kiasi cha Shilingi milioni 15,000,000 kwa ajili ya kuiwezesha kushiriki vyema na kuleta ushindani katika Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu Tanzania Bara.

Aidha, TPDC imechangia kiasi cha shilingi milioni 10,000,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Ufukoni. Hatua hii imekuja ikiwa jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. John Pombe Mangufuli kuhakikisha utawala bora unatekelezwa kwa vitendo.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Undelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia Dk. Wellngton Hudson alisema TPDC itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kusukuma gurudumu la maendeleo katika maeneo yaliyo jirani na miundombinu ya Mradi wa gesi asilia pale linapokuawa na uwezo wa kifedha.

No comments: