Tuesday, December 29, 2015

SOMO LA YOGA: Ulaji Nyama, Afya na Sanaa ya Yoga

Tatizo Gani Kula Nyama

Je! Ni kawaida asili ya mwanaadam kuwa nakula nyama? Kufuatana na mafunzo ya sanaa ya Yoga, inashauri sana kuepuka madhara yanayosababishwa na athari ya kula nyama ambayo ni mjadala mrefu na uanaleta hoja nyingi katika maisha ya mfumo mzima wa sanaa hiyo.

Leo, kama tunajiandaa kuelekea mwaka mpya 2016 na malengo mapya, basi moja ya ushauri na mazungumzo ni kufahamishana na kuhusu mambo kazaa ya sanaa ya Yoga na uhusiano wake wa kutokula nyama kiafya.

Mfumo wa kuchanganya na kuyeyusha chakula wa binaadam “ Digestive system” pamoja na jinsi meno na maumbo yaliyo kunatofauti sana kulinganisha na wale walao nyama kiasilia “Carnivorous”, wanatofauti kubwa kama vile maumbile ya mfumo wao wa chakula tumboni. Tumbo lao“Bowel” ni  fupi mara tatu tu ya urefu wa mwili wao.  Hii inawaruhusa kuweza kutoa  mabaki ya chakula chao cha nyama mwilini haraka sana kwa ufupi huo wa utumbo. Hivyo wadudu wa “Bacteria” hawakai muda mrefu tumboni na kutoka kupitia mfumo wa haja kubwa. 
Utumbo wa “Carnivorous”  unauwezo mara 10  zaidi ya kemikali ijulikanayo kama “Hydrochloric Acid” kulinganisha na wale wasiao kula nyama kisilia kama vile wanyama wanao kula majani tu, na huwawezesha wala nyama kuchanganya na kuyeyusha nyama  mbichi na hata mifupa bila taabu yeyote. Meno yao pia ni ushahidi dhahiri, “ Canines” meno yalioyochongoka na marefu kuwawezesha kumudu hali ya ulajiwao wa nyama.

Binaadam, ni wazi kabisa sio mlaji nyama asilia “ Natural”. Maumbile ya mfumo wao wa kuchanganya na kuyeyusha chakula “Digestive system”, unadhihirisha hivyo. Ni aina zote za mazao ( Maharage, kunde, mbaazi, soya) ya aina mbali mbali, matunda karanga aina zote ni vyakula ambavyo asili ya mwanaadam tokea enzi na enzi. 

Kimaumbile, utumbo wa binaadam una urefu mara 12 ya urefu wa mwili wake,  endapo kama utumbo utanyooshwa ndivyo jinsi utadhihiri urefu wake. Hii inaonyesha jinsi gani kwamba chakula cha binaadam huchukua muda mrefu kuchanganywa na kuyeyushwa tumboni kulinganisha na mfumo wa “Carnivorous” ulio mara tatu tu ya urefu wao. Nyama, huanza kuoza mara tu iingiapo tumboni, na kuchukua muda mrefu sana kutoka mwilini  kulinganisha na wa nyama wenye kula nyama.

Vilevile, nyama ina aina ya kemikali yenye sumu ijulikanayo kwa jina la “Toxic” na “Adrenalin” ambazo hubaki mwilini mwa mwanyama anapochinjwa au kuuwawa. Hii pia husababisha, aina nyingine ya kemikali ijulikanayo kama“ Uric Acid” ni sumu inayobaki katika viungo na damu ya nyama ambayo watu wanakula.
Kufuatana na “Encyclopidia Brittanica” protini “Protein” inayopatikana katika mazao kama vile karanga, maharage, kunde, mbaazi, maziwa  na soya, ambayo ni safi kabisa, kulinganisha na ile inayopatikana kutoka katika nyama, siyo safi kwa asili mia 56%. 

Mafuta ya nyama “Meat Fat” au “Cholesterol” hujijenga katika mishipa au milija ya damu “ Arteries”, na jinsi mwili unavyo zeeka, ndivyo jinsi mishipa na milija hiyo uzeeka na kupoteza nguvu zake wakati ikikupungua ukubwa wa upana wake kwa sababu za mafuta kujaa ndani ya mishipa hiyo.  Hii husababisha njia ya damu kuwa nyembamba na kusababisha shinikizo katika kwenye moyo.

Hapo ndipo sasa, moyo haunabudi bali kufanya kazi mara dufu ya kawaida yake kusambaza damu mwili mzima. Matokeo, ni kuleta madhara ya kupasuka mishipa ya damu ( Stroke ), ni matatizo ya kiharusi, shinikizo la moyo ( Blood Pressure ) ni mingoni mwa matatizo makubwa sasa  katika  jamii yetu na ulimwengu mzima. Moja ya kazi kubwa na majukumu anayobeba mla nyama ni kemikali ya aina ya “Urea na Uric Acid” “(Nitrogen Compound)”, kutoka katika nyama. Moja ya mifano,  “Beefsteak” kwa mfano huu  ina gram 14  za “Uric Acid, kwa kila pound moja ya nyama. Hii ni kweli hasa kupitia vipimo vya mkojo wa mtu wanao  kula nyama na asiye kula, kuna tofauti kubwa ya ushahidi huo.

Matokeo yake, figo za mtu anaekula nyama hazina budi kufanya kazi mara tatu ya kawaida yake kutoa sumu au kemikali hiyo ya aina ya “Nitrogen Compound” iliyopo katika nyama na hubaki mwilini, na figo ndio yenye jukumu la kuhakikisha mwili upo katika mazingira ya usafi au ndio husafisha  kemikali zote zilizopo mwilini. Nahatimaye  kutoka kwa njia ya  mkojo mwilini.

 Mtu akiwa kijana na nguvu zake kikawaida, hilo huwa sio tatizo kabisa kwa figo kufanya kazi ya ziada.  Hivyo basi, mwili unapo anza zeeka na kupoteza uwezo wake wa kawaida jinsi  maisha yalivyo, hivyo ndio jinsi figo nayo hupungua nguvu zake za kuwajibika kwa ziada kusafisha hizo kemikali mwilini. 

Figo zinapokuwa zimeelemewa kupita kiasi kiwango Fulani,  sababu ya kula nyama nyingi, kemikali ya “Uric Acid” inaanza sambaa mwilini mzima kutokana na kile kijulikana cho kama figo kushindwa ( Kidney failure) hazikufanya wajibu wake kama inavyo stahili.  Hiyo kemikali “ Uric Acid” husambaa katika viungo vya mwili, inavutwa kama jinsi sponji inavyo fyonza maji, na kuganda kama jiwe katika viungo au (Joints) na misuli ya mwili.

Hii matokeo yake husababisha maumivu makubwa ya viungo yaani (Joints pain) na misuli katika mwili. Kwa namna moja au nyingine, inaaminika pia huu ni chanzo cha matatizo ya magonjwa kama vile : Gout, Arthrititis na Rheumatism.

Hatua hiyo ndio yupasa madaktari kushauri wagonjwa kupunguza kula nyama au kuacha kabisa kula nyama, ambapo kwa kweli tayari madhara yameshafanyika mwilini. Na kupitia mazoezi ya sanaa ya Yoga, husaidia kuimarisha viungo na misuli kupitia mafunzo yake ya umakini na utaratibu kuambatana na pumzi kuwezesha mwili kupata nguvu zaidi kulinganisha na mazoezi ya aina nyingine yenye kutumia nguvu za misuli tu, na hatimae kuchoka haraka.

Imetolewa na Sensei Rumadha Fundi; mkufunzi wa Yoga; 
 Eastern Metropolitan Bypass, Tiljala, Culcutta, India. 
 College of Neo-Humanist Studies; 
Gullringen, Vimmerby, Sweden.

No comments: