Sunday, December 13, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

SIMU .TV: Mamlaka ya chakula na dawa mkoani kanda ya kaskazini imeteketeza shehena ya chakula na vipozi hatarishi kwa matumizi ya binadamu zenye thamani ya Zaidi ya shilingi millioni 5. https://youtu.be/iDts4PiCnZU 
SIMU .TV: Mkoa wa Ruvuma awataka madiwani wa kata mbalimbali za mkoa huo kusimamia na kudhibiti matumizi ya mapato ili waweze kuitumikia jamii kujipatia maendeleo. https://youtu.be/IIrnuyFsYXI
 SIMU .TV: Serikali mkoani Morogoro imesema haitowavumilia madiwani watakao endekeza makundi mkoani humo badala ya kufanya kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo. https://youtu.be/lvfHFe2Pdb0
 SIMU .TV: Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Damian Lubuva awataka viongozi wa serikali,dini na vyama ya siasa kutoingilia mchakato wa uchaguzi unaotegemewa kufanyika katika majimbo ambayo hayakufanya uchaguzi.https://youtu.be/cjVctVInyNI
 SIMU .TV: Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aanza kazi rasmi kwa kufanya ziara ya kushitukiza hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.https://youtu.be/vbEq20gq-xM
 SIMU .TV: Mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali yanyesha wilayani Iringa na kuharibu mazao pamoja na makazi ya watu. https://youtu.be/jiwfKSHNvmg
 SIMU .TV: Elimu juu ya namna bora ya utunzaji wa hali ya hewa na mazingira yaelezwa kuhitajika Zaidi kwa jamii zenye uelewa duni juu ya athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira. https://youtu.be/ebkThHY09ts
 SIMU .TV: Baada ya jeshi la polisi wilaya ya Misungwi mkoani mwanza kuchelewa kumchukulia hatua imamu wa msikiti wa Bukumbi anayetuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 11 hatimaye mtoto wa mama huyo aamua kuangua kilio kwa serikali.https://youtu.be/izkbt4GygRI
 SIMU .TV: Tume ya haki za binadamu na utawala bora yalaani tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali kuamuru watumishi wa umma wakamatwe na kuweka rumande kwa kutowajibika ipasavyo kwa kushindwa kutimiza majukumu yake.https://youtu.be/sJL-Ba3A0jY
 SIMU .TV: Jeshi la polisi wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu 38 mkoani humo kwa tuhuma za wizi wa nyaya za umeme za shirika la umeme Tanzania TANESCO zenye thamani ya shilingi Zaidi ya  milioni 150.https://youtu.be/tOeKTKm_yNQ
 SIMU .TV: Mufti mkuu wa Tanzania Shekhe Zuberi awataka viongozi wa baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA katika ngazi mbalimbali nchini kubadili fikra na mwenendo katika utendaji wao ili chombo hicho kiwe dira kwa waislamu na si chanzo cha migogoro. https://youtu.be/U7zWS7bi98M
SIMU .TV: Baada ya siku 7 alizotoa Raisi Magufuli kwa wafanya biashara waliokwepa kodi kwa kutoa makontena bandarini baadhi ya makampuni yaelezwa kupuuza agizo hilo. https://youtu.be/lT43mUNau5g
SIMU .TV: Baada ya uapisho naibu waziri wa afya Hamis Kigwangala afanya ziara ya kushitukiza katika hospitali ya Amana ya jijini Dar es salaam na kukuta hali ya isiyoridhisha. https://youtu.be/PPwE16tBLdQ
SIMU .TV: Baadhi ya wananchi wilayani Misungwi mkoani Mwanza waiomba serikali kuwaboreshea miundo mbinu ya Barabara kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo na kuleta adha. https://youtu.be/TGirc0__kLo

No comments: