Monday, December 7, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamemuunga mkono Rais John Magufuli kwa juhudi zake za kupambana na ufisadi nchini; https://youtu.be/DlGbxzyO668

Kesi ya upotevu wa bilioni 1 inayowakabili waliokuwa watumishi wa shirika la TANESCO mkoani Kagera imebadilishwa na kuwa kesi ya Uhujumu uchumi;https://youtu.be/AHL8tx0NsJ0

Watu takribani arobaini wamenusurika kifo baada  ya trekta walilokuwa wakisafiria  kutumbukia mtaroni mkoani Tabora; https://youtu.be/oB5yjv2Bxcw

Inaelezwa kuwa pesa zilizokuwa zitumike kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani tayari zimetumika kununua dawa; https://youtu.be/GfbHeqhno_A

Kampuni ya Watumishi housing imeanza ujenzi wa nyumba za  bei na fuu kwa watumishi wa umma mkoani morogoro ; https://youtu.be/E1cJ2cIWEhw

Taasisi za kifedha nchini zimeombwa kulegeza masharti ya mikopo ili kuviwezesha vikundi vya akiba na mikopo kutumia huduma zao; https://youtu.be/D8iYddyrcUk

Wadau wa soka mkoani Mwanza wanaamini serikali ya awamu ya tano itawasaidia uwanja wao wa Nyamgana kuwekewa nyasi bandia; https://youtu.be/rhouFkytopM

Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini ameanza kujipanga kupangua tuhuma za rushwa zinazomkabili kigogo huyo wa FIFA. https://youtu.be/MhUDfilY3JE

Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imewasimamisha watumishi wa umma 9 kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha; https://youtu.be/LQ0p_2XzqV0

Jeshi la ulinzi la wananchi la Tanzania JWTZ limesema litawachukulia hatua kali wananchi wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kusambaza taarifa za uongo juu ya jeshi hilo; https://youtu.be/Bjm8wZfqDew

Wakazi wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe waiomba serikali kuharakisha ujenzi wa hospitali ili kuwapunguzia gharama za matibabu;https://youtu.be/gHhSsuHcA5w

Jeshi la polisi nchini limesema litapambana vikali dhidi ya vitendo vya unyanysaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto nchini; https://youtu.be/yLTdyUhJb2Y

Inaelezwa kuwa Tanzania inahitaji kuwa na hoteli za kutosha zenye viwango vya kimataifa kwa lengo la kuboresha utalii nchini; https://youtu.be/a1F9AF-DzkM

Mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi NEEC umewashauri wananchi kujiunga katika vikoba ili waweze kujipatia mikopo pamoja na mitaji;https://youtu.be/Dw_fD2S4BFs

Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF limewaagiza wamiliki wa viwanja vya mpira nchini kuvifanyia ukarabati kabla ya michezo ya ligi kuu kuanza kutimua vumbi jumamosi; https://youtu.be/KhXhpPIzPrw

Rais Magufuli atengua uteuzi wa katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi Shaban Mwinjaka baada ya kubaini utendaji usio kidhi viwango; https://youtu.be/NjD6F2tHHS0

Zaidi ya wakulima 200 wilayani Hanang mkoani Manyara wavamia shamba la mwekezaji kwa madai ya mwekezaji huyo kushindwa kuliendeleza.https://youtu.be/uhHiWsjZhOQ

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar yasema tume ya uchaguzi ya Zanzibar iko huru katika kusimamia na kuendesha mambo yake kwa mujibu wa katiba na sheria bila kuingiliwa na jumuiya za kimataifa. https://youtu.be/5Ac-QHNmCTI
 Hatimaye mgogoro kati ya wafanyakazi na kiwanda cha nguo cha urafiki na wamiliki wafikia ukomo baada ya katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara kuingilia kati.https://youtu.be/ytgZka7660U

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC yatangaza December 13 kuwa tarehe maalum kwa ajili ya uchaguzi katika majimbo ya Arusha na Handeni. https://youtu.be/6eEIFuc4HXc

Kituo cha polisi cha Stakishari jijini Dar es salaam chazindua rasmi ofisi ya dawati ya jinsia na watoto ikiwa ni kwa msaada wa shirika la umoja wa mataifa.https://youtu.be/SfOYhGY2RK0

Hatimaye mgogoro kati ya wafanyakazi na kiwanda cha nguo cha urafiki na wamiliki wafikia ukomo baada ya katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara kuingilia kati.http://simu.tv/6Gl2pui

Rais Magufuli avunja bodi ya bandari na kutengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo pamoja na katibu mkuu wizara ya uchukuzi. https://youtu.be/qmz1BpVF-uY

Jeshi la wananchi watanzania JWTZ linawashikilia wafanyakazi 4 wa shirika la huduma za viwanja vya ndege la SWISS PORT kwa tuhuma za kupiga picha vifaa vya jeshi hilo wakati vikiingia uwanja wa ndege na kuzisambaza kweye mitandao.https://youtu.be/0DZ-Peui7bM

Beki kuu ya Tanzania yaanzisha na kuboresha kanuni mpya za kudhibiti utakatishaji fedha haramu kwa kutumia mfumo wa kieletronic. https://youtu.be/RJhHtMI8KMs

Raisi John Magufuli akutana na mwakilishi mkazi wa benki ya dunia katika ikulu jijini Dar es salaam na kuzungumzia mchango wa benki hiyo katika maendeleo ya Tanzania.https://youtu.be/TPiTdJGVoE4

Ripoti ya jukwaa la uchumi duniani imeeleza kuwa Tanzania inashika nafasi ya 7 kati ya nchni 141 duniani katika ushindani wa sekta ya utalii kufuatia kuwa na vivutio vingi vya utalii. https://youtu.be/1Mo9DyU6EZE

Wavuvi kandokando ya mto Ruvuma mkoani Mtwara waiomba serikali kuwasaidia kupamabana na mamba kwani wamekuwa tishio kwa maisha yao.https://youtu.be/sFVZlac5m_0

Mgombea ubunge wa Arusha mjini kupitia CUF asema yuko tayari kujitoa endapo atarudishiwa gharama zake za kampeni. https://youtu.be/kCoh1eE594A

Baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC latoa siku 6 kwa watu waliovamia na kujenga katika kingo za mto mbezi kubomoa nyumba zao wenyewe huku likimshikilia raia wa uturuki. https://youtu.be/uvi_NXKiA7s

No comments: