Mvua kubwa iliyonyesha wilayani Rungwe imesababisha maafa makubwa baada ya kubomoa nyumba 23 na zahanati na pia ikiharibu mazao.https://youtu.be/rhdRMRtRiDE
Serikali yapiga marufuku biashara za uuzwaji wa matunda yaliyowazi na vyakula katika maeneno ambayo hayakuanishwa na wataalam wa afya.https://youtu.be/ZjQ3Nh1TNOU
Juhudi za makusudi zaelezwa kuhitajika ili kutokomeza mapigano kati ya wakulima na wafugaji yanayotishia kutokea kwa uhasama kati ya makundi hayo wilayani Kilwa. https://youtu.be/HiwnZLj-20k
Wafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya ACACIA wapinga kusidio la mwajiri wao la kutaka kuwapunguza kazi jumla ya wafanyakazi 250.https://youtu.be/wubBOw6B0es
Rais Magufuli awaapisha mawaziri na naibu waziri aliowateua hivi karibuni huku mawaziri hao wakiahidi mambo makubwa kwa taifa;https://youtu.be/MAeRULxkNb0
Serikali imesema iko tayari kuzungumza na wataalam wa tiba asili nchini kwa lengo la mashauriano juu ya kutangaza huduma zao kwenye vyombo vya habari kwa kufuata taratibu. https://youtu.be/4MtWBUoaaFo
Waziri wa maliasili na utalii Prof.Maghembe asema serikali haina mpango wa kuteketeza maelfu ya meno ya tembo na nyara nyingine zilizohifadhiwa katika ghala la serikali. https://youtu.be/_DoUBH2K04Q
Siku kadhaa baada ya serikali kuendesha zoezi la bomoa bomoa baadhi ya waathirika wa zoezi hilo waelezwa kujenga vibanda ili kujistiri.https://youtu.be/Q8F1OAOZlhQ
Serikali mkoani Mwanza imesema itawachukulia hatua kali wazazi wa wanafunzi waliofaulu watakaoshindwa kuwapeleka shule.https://youtu.be/xkjwozis-7A
Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela, amuomba waziri wa nishati na madini prof. Sospeter Muhongo kuingilia kati mkwamo wa upatikanaji wa umeme katika wilaya ya Kyerwa. https://youtu.be/eYkciJN-uN8
Wachimbaji wa wawili wa madini wasadikiwa kufukiwa na kifusi mkoani Mbeya. https://youtu.be/aahcIgP3GXE
Shirikisho la vyama vya tiba asili nchini laibuka na kukanusha taarifa zilizotolewa na jukwaa la tiba asili la kugomea agizo la serikali.https://youtu.be/TvgS7q4hCMc
Rais John Magufuli amewaapisha mawaziri na naibu waziri aliowateua hivi karibuni kukamilisha baraza lake la mawaziri; https://youtu.be/FMSy8ReiYFE
Inaripotiwa kuwa jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu 18 kwa tuhuma za kukutwa na makosa toafuti ikiwemo ujambazi;https://youtu.be/szIZeiZ-zl8
Polisi 6 wanaotuhumiwa kwa mauaji ya watuhumiwa wa ujangili nchini wapandshwa kizimbani hii leo katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam;https://youtu.be/_7cEAWS-UhQ
Mahakama kuu kanda ya Mbeya imeitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na mgombea wa CHADEMA dhidi ya mbunge wa Kyela na waziri wa katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe;https://youtu.be/qrLZsWccXHo
Watanzania wameshauriwa kuwekeza nchini ili kuhimarisha sekta ya uchumi;https://youtu.be/9QokCf6J6do
Klabu ya soka ya Yanga imevunja mkataba na mchezaji wake wa kimataifa toka nchini Rwanda Haruna Niyonzima; https://youtu.be/mGnn7r7V2mY
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona, Xavier Hernández amesema kuwa mbinu za Jose Morinho zililenga ushindi pekee badala ya kujenda timu imara;https://youtu.be/q7cBMjRiKN
Wachimbaji wadogo wa dhahabu mkoani Mara wamemuomba waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo kuwapatia huduma ya umeme;https://youtu.be/FOSO-c3dte8
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itaiagiza mamlaka ya bandari TPA kukaa pamoja na wakazi Kibirizi na katosho mkoani Kigoma ili kutatua mgogoro uliopo baina ya mamlaka hiyo na wakazi wa vijiji hivyo;https://youtu.be/33kjkqHAB_k
Inaelezwa kuwa ugonjwa wa kipindupindu unazidi kushika kasi jijini Mwanza huku idadi ya wagonjwa wapya wa kipindupindu wakiripotiwa kufikia 17;https://youtu.be/FMitS7rtz7I
Biashara ya mirungi mkoani Kilimanjaro imetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi mkoani humo;https://youtu.be/pVdUkbjVQNA
Serikali imewataka wamiliki wa viwanda vidogo vilivyopo jijini Dar es Salaam kuvisajili mara moja na kuanza kulipa kodi; https://youtu.be/Rm-EjWFyRWs
Baadhi ya wafanyabishara wa mchele jijini Dar es Salaam wamelalamikia kuwepo kwa idadi ndogo ya wateja katika kipindi hiki cha siku kuu;https://youtu.be/xyuMeuWjyQY
No comments:
Post a Comment