Wednesday, December 23, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Waziri wa kilimo, umwagiliaji na mifugo Mwigulu Nchemba, atoa onyo kali kwa maafisa wanyamapori wanao wanyanyasa wafugaji.https://youtu.be/4AI49WFQgSY  

Baadhi ya wakazi katika manispaa ya Musoma wailalamikia manispaa hiyo kwa kuwataka kuhama eneo la makazi yao ili hali makazi ya matajiri hayaguswi.https://youtu.be/lqW8JyfcwKI  

Zaidi ya wakazi 108 wilayani Masasi Mkoani Mtwara hawana mahali pa kuishi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kuharibu nyumba na mali zao.https://youtu.be/_8h8VHj0xyk  

Waumini wa dini ya kiislam nchini watakiwa kulinda na kudumisha amani miongoni mwao pamoja na wananchi wenzao ikiwa ni njia sahihi ya kumuenzi mtume Muhammad. https://youtu.be/pOktMrjqY-w

Serikali ya mkoa wa Dar es salaam yalitaka shirika la maji safi na maji taka Dar es salaam DAWASCO kwa kushirikiana na sekretarieti ya miundombinu ya mkoa kuteua mkandarasi wa kujenga mradi wa maji taka eneo la Buguruni Kisiwani baada ya kukamilika kwa usanifu wa wake. https://youtu.be/M6HJduQ__w4
Katika hali isiyokuwa ya kawaida askari polisi amuua askari mwenzake na kisha kujiua mwenyewe kwa kujipiga risasi jijini Mwanza.https://youtu.be/whaVZeLpNvE
Serikali imetoa agizo kwa shirika la hifadhi ya jamii nchini NSSF, kusimamia wakandarasi waliopewa tenda ya ujenzi wa daraja la Kigamboni, kukamilisha ujenzi huo haraka ifikapo Januari 30 mwakani. https://youtu.be/htluGaC7gAk

Waziri wa mambo ya ndani Mhe.Charles Kitwanga atoa siku 30 kwa wageni waishio nchini bila vibali kufuata taratibu la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. https://youtu.be/NCXTDff93pY
Kufuatia kukamilika kwa uchaguzi mkuu nchini, serikali yapiga marufuku mikutano yote ya kisiasa inayoashiria kuwashukuru wananchi hasa kwa wagombea walioshindwa. https://youtu.be/R4eJWexjYVE

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amsimamisha kazi kaimu mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Ocean Road kufuatia mgongano wa kimaslahi na taasisi hiyo pamoja na malalamiko ya wananchi. https://youtu.be/ty9FKBhiTiI
Jeshi la polisi nchini lapiga marufuku abiria kusimama ndani ya magari ya abiria huku likiahidi kuwakamata abiria wote watakao kaidi pamoja na madereva.https://youtu.be/HezFvfLisvI

Waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo atishia kuwanyaganya maeneo ya uchimbaji yanayomilikiwa na wachimbaji wakumbwa bila kuendelezwa na kuwapatia wachimbaji wadogo. https://youtu.be/jvZuQSspKcI

Waziri wa mambo ya ndani Mh. Charles Kitwanga amuagiza katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani kupeleka wakaguzi katika idara ya uhamiaji;https://youtu.be/COSIj7OHrRA

Baadhi ya wanawake mkoani Ruvuma wameitaka serikali kuongeza adhabu kwa wanawake wanaofanya vitendo vya kikatili hasa kwa watoto;https://youtu.be/wCpq8yix9dk

Serikali imesitisha zoezi lake la Operesheni toa ng’ombe ndani ya hifadhi ya misitu kwa muda mpaka pale itakapotoa agizo jipya;https://youtu.be/UMQQ6KRKkrE

Waumini wa dini ya kiislamu nchini wameungana na wengine duniani katika kusheherekea sherehe za Maulidi ambayo kitaifa itafanyikia jijini Dar es Salaam;https://youtu.be/04shlNZX1jY

Inaelezwa kuwa wakulima wa zao la Muhogo eneo la kanda ya ziwa wanatarajia kufaidika na soko jipya la zao hilo; https://youtu.be/Gn1_n6WgOps
Rais wa zamani wa klabu ya Yanga Abbasi Tarimba ameunga mkono dhamira ya Mohammed Dewji kutaka kuinunua klabu ya Simba;https://youtu.be/RdS3ndBX85A

Serikali ya Ufaransa yaliijia juu shirikisho la soka duniani FIFA juu ya hukumu iliyotolewa kwa Rais wa shirikisho la mpira barani Ulaya Michel Platinhttps://youtu.be/IlcWK2m9wtM

Mtendaji mkuu wa DART, Asteria Mlambo amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kukiuka sheria ya manunuzi ya umma; https://youtu.be/vCkU7VQRYHA

Waziri wa maji na umwagiliaji Prof.Makame Mbalawa aagiza kuchukuliwa kwa hatua za kisheria kwa baadhi ya watumishi wa wizara hiyo walioshindwa kusimamia mradi wa ujenzi wa maji mkoani Simiyu;https://youtu.be/WuwfK11GOVc

Rais John Magufuli amemalizia kutangaza nafasi za mawaziri wa wizara nne zilizokuwa zimebakia wakati alipotangaza baraza la mawaziri;https://youtu.be/e9T3038FAAk
Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Mhe.Charles Mwijage, amewataka wasimamizi na watafiti wa wizara yake kuhakikisha Tanzania haiingizi bidhaa zilizochini ya kiwango; https://youtu.be/ABxjPckwmoc

Benki ya posta nchini TPB imetoa mkopo wa zaidi ya shilingi millioni 244 kwa vikundi vya vikoba 185 ili viweze kujishughulisha na shughuli mbali mbali za kiujasiriamali; https://youtu.be/17PR0WJ1Dd0

Kampuni ya simu nchini TTCL imezindua huduma mpya ya intaneti ya 4G yenye kasi Zaidi; https://youtu.be/GohNs-DET70
Vilabu vya Azam na Yanga vimesema vimeshangazwa na kauli ya TFF kuwa bado havijapeleka majina ya wachezaji waliowasajili kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika na ile ya kombe la shirikisho;https://youtu.be/ABes2Pb-4Co

No comments: