Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni
ya PanAfrican Energy Andrew
Kangashaki (kushoto ) na Mkurugenzi
wa Wilaya ya Kilwa
Twalib Mbasha wakikabidhiana mkataba wa miradi ya ujenzi wa nyumba ya
mama ngojea katika hospital ya Kinyonga na ukarabati wa wodi ya
uzazi mara baada ya kumaliza kusaini mikataba hiyo katika hafla fupi
iliyofanyika jana Kilwa Kivinje.
Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni
ya PanAfrican Energy Andrew
Kangashaki(wa tatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa
Twalib Mbasha (wa tatu kulia) wakisaini makubaliano ya miradi miwili ya ujenzi
wa mama ngojea ‘maternity waiting home’ yaani nyumba maalum kwa kina mama
wajawazito watakaokua wakisubiri kujifungua itakayojengwa katika hospitali ya
Kinyonga – Kilwa Kivinje na kukarabati wodi ya uzazi na chumba maalum cha
uangalizi wa akina mama mara tu baada ya kujifungua katika kituo cha afya cha
Kilwa Masoko.
Huku wakishuhudiwa na Mwanasheria wa Wilaya Mh. Godfrey Makary (wapili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Juma Abdalah Njwayo(wa pili kushoto), Mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia chama cha CUF Mh. Vedasto Edgar Ngombale(wakwanza kushoto) pamoja na Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wakwanza kulia).
Huku wakishuhudiwa na Mwanasheria wa Wilaya Mh. Godfrey Makary (wapili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Juma Abdalah Njwayo(wa pili kushoto), Mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia chama cha CUF Mh. Vedasto Edgar Ngombale(wakwanza kushoto) pamoja na Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wakwanza kulia).
Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha
CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wapili kulia) akitoa neno la shukrani kwa
Kampuni ya PanAfrican Energy kwa niaba ya wananchi wa Kilwa Kusini mara baada
ya makabidhiano ya mkataba wa miradi itakayowanufaisha wananchi wa kilwa.
Wafadhili wa mradi wa ujenzi wa wodi ya
wazazi Kampuni ya PanAfrican Energy pamoja wakiwaonesha wanahabari chumba cha
uzazi katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko ambacho kipo katika mradi uliosainiwa
kati ya wilaya ya Kilwa na kampuni hiyo. Hii ni katika kuunga jitihada za
serikali za kuboresha huduma za afya.
Hali
halisi ya mazingira ya wodi ya wagonjwa katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko,
hii ni wodi ya wanaume. Kiyuo hichi cha afya
kilijengwa mwaka 1952 enzi za ukoloni mpaka sasa hakijawahi
kukarabatiwa.
Wakisaini makubaliano ya miradi ya ujenzi
wa mama ngojea na ukarabati wa chumba cha uzazi na wodi maalum ya uangalizi wa
kina mama mara tu baada ya kujifungua wilayani Kilwa ni Meneja Uwajibikaji kwa
jamii kutoka Kampuni ya PanAfrican Energy Andrew Kangashaki(wa pili kushoto)
pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Twalib Mbasha (wa pili kulia)
wanaowashuhudiwa ni Mwanasheria wa Wilaya ya Kilwa Mh. Godfrey Makary ( kulia),
Mkuu wa Wilaya ya hiyo Juma Abdalah Njwayo (kushoto) jana katika hafla fupi
iliyofanyika jana katika hospitali ya Kinyonga Kilwa Kivinje.
Wanahabari wakihakikisha wanapata habari
sahihi kutoka kwa wahusika.
Wauguzi
wa Hospitali ya Kinyonga Kilwa Kivinje wakishuhudia makabidhiano ya mkataba wa
miradi ya ujenzi wa mama ngojea ‘maternity waiting home’ utakaofanyika katika
hospitali yao na mradi mwingine wa ukarabati wa wodi ya uzazi utakaofanyika
katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo
jana.PICHA NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP.
========= ======= ====== ==========
PANAFRICAN
ENERGY KUTOA TSH .335,142,142 KUFADHILI UJENZI WA WODI ZA AKINA MAMA WAJAWAZITO
WANAOSUBIRI KUJIFUNGUA ‘MAMA NGONJEA’ YAANI MATERNITY WAITIING HOME, HOSPITALI
YA WILAYA ,KINYONGA KILWA KIVINJE NA KUKARABATI
WODI ZA UZAZI NA CHUMBA MAALUM CHA UANGALIZI WA AKINA MAMA MARA TU BAADA YA
KUJIFUNGUA KITUO CHA AFYA CHA KILWA MASOKO.
Wakazi wa Kilwa wana
haki ya kuendelea na kuwa na matumani baada ya kushuhudia makubaliano ya miradi
mingine mikubwa katika eneo lao kati ya
Kampuni ya PanAfrican Energy na Wilaya ya Kilwa. Moja ya miradi hiyo ni ujenzi
wa wodi ya kupumnzikia wakina mama wakisubiri kujifungua katika Hospitali ya
Kinyonga iliyopo Kilwa Kivinje, na mradi mwingine ni ujenzi wa wodi ya wazazi
na chumba maalum cha uangalizi wa akina mama mara baada ya kujifungua katika
Kituo cha afya cha Kilwa Masoko.
Katika hospitali ya wilaya , PANAfrican Energy
watafadhili ujenzi wa wodi ya kusubiria akina mama, yaani mama ngonjea
(maternity waiting home,) ambayo ni sehemu wanaposubiri akina mama ambao wanaweza kuwa kwenye uzazi
hatarishi. Hii ni njia kuu ya kuondoa tatizo la umbali mrefu kama
kikwazo cha akina mama kujifungua salama ambapo hivi sasa wakina mama hushindwa
kufika mapema hospitalini kutokana na kutokuwa na chumba maalum kwa ajili ya
kusubiria huduma ya kujifungua.
Kuwepo kwa wodi ya kupumnzikia akina mama hawa hapa
Kinyonga ni manufaa tosha ukiangalia hali halisi ya mazingira na miundombinu ya
Kilwa. Pamoja na na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kwani
watakuwa karibu na hospitali, pia itapunguza gharama kwani mama huyu anaweza kuchukua usafiri wa
kawaida na kwa utaratibu wake na kwenda kusubiria.
Miradi hii miwili inaunga mkono
jitihada za serikali za kuboresha huduma za afya nchini na imekuja muda muafaka
ambapo serikali inachukua hatua kupunguza na kutokomeza kabisa vifo vya akina
mama wajawazito na matatizo yanayotokana na ujauzito. Kutokana na utafiti uliofanywa mwaka 2009/10
nchini inaonesha kuwa wanawake 454 hufariki kwa kila 100,000, kila mwaka kutokana
na matatizo yanayotokana na ujauzito.
Vifo vya akina mama wajawazito vinatokana
na kutokwa damu nyingi wakati na baada
ya kujifungua, utoaji mimba usio salama, shinikizo la damu, na kukosa uchungu wa
kutosha au kukosa kabisa wakati muda wa kujifugua umefika .Uwepo mdogo wa
sehemu za dharura na huduma kwa mtoto aliyezaliwa, ukosefu mkubwa wa watoa
huduma za afya wenye ujuzi pamoja na mfumo duni wa rufaa, yote haya yanachangia
kwa kiasi kikubwa vifo vya kina mama wajawazito.
Akiongea katika hafla ya kusaini
makubaliano ya miradi hiyo leo kwa niaba ya Kampuni ya PanAfrican Energy, Meneja
Uwajibikaji kwa jamii wa Kampuni ya PanAfrican Energy Bwana Andrew Kangashaki alisema, “Idadi ya vifo vya kina
mama wajawazito imekua kubwa ya kutisha na tunataka kuwahakikishia wakazi wa
kilwa kwamba ni kupitia miradi kama hii mabpo tunaweza kuwa sehemu ya kumaliza tatizo
hili kwa pamoja.
Leo tena tunasaini makubaliano mengine na wilaya ya kilwa
katika masuala ya afya; Tutafadhili miradi hii miwili yenye gharama ya Tshs
335,142,142. Moja ni nyumba ya kupumzikia kina mama wajawazito wanaosubiri
kujifungua katika hospitali ya Kinyonga, Kilwa, ambayo itagharimu Tsh 220,292,430.00 huku wodi
za wazazi katika kituo cha afya cha kilwa masoko kitagharimu Tsh
114,849,636.00.
Huu ni muendelezo
wa kusapoti Nyanja za afya katika wilaya ya kilwa. Mwanzoni mwa mwaka huu kampuni ya PanAfrican
Energy ilikamilisha ujenzi wa nyumba za wauguzi wa kituo cha affya cha Nangurukuru, ambacho
hapo awali walikikarabati. Nyumba za
wauguzi zilikabidhiwa mwezi Juni kwa mkuu wa wilaya ya Kilwa.
“Lengo letu kuu
ni kuchangia mafanikio ya kiuchumi na ya kijamii katika wilaya ambapo Kampuni
inafanya kazi, kutambua na kuimarisha uhusiano usiotengeka kati ya ustawi wa
biashara na ustawi wa jamii kwa kutimiza mahitaji yao. Tunawasikiliza wananchi
wa Kilwa na kuyazingatia mahitaji yao kwa umaakini. “aliongeza, Bw.Andrew.
Naye Mkurugenzi wa wilaya ya kilwa Bw.Twalib Mbasha aliishukuru Kampuni ya PanAfrican Energy kwa jitihada kubwa
wanazoendelea kuzifanya katika kuwawezesha wakazi wa kilwa. “Mmetuhakikishia
kuwa mpo nasi, nyie ni washirika tunaweza kuwategemea katika Nyanja zinazogusa
na kuhusu maisha yetu.
Tunapenda kuwahakikishia kuwa tutakuwa pamoja katika
kukamilisha miradi hii kuanzia mwanzo mpaka mwisho.” Alisema. Pamoja na wauguzi na wafanyakazi wa sekta ya
afya wilaya ya Kilwa, pia walioshuhudia usainishaji wa makubaliano hayo ni Mkuu
wa wilaya ya Kilwa, Mhe.
Juma Njwayo pamoja na wabunge wa Kilwa Mh.Vedasto Edgar Ngombale and Selemani Bungawa.
No comments:
Post a Comment