Tuesday, December 8, 2015

MRAGHABISHI MAIMUNA SAIDI AGEUKA SHUJAA WA KIJIJI CHA MWIME KAHAMA

Na krantz mwantepele ,       
Ziara niliyofanya katika Kijiji cha Mwime kata ya Mwendakulima  wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga mwishoni wa  mwezi Novemba mwaka huu ,ilinipa mwanga wa jinsi ambavyo wananchi wakiamua kuchukua hatua wanaweza kubadili mfumo mzima na kuweza kujiletea maendeleo katika Nyanja zote za maendeleo .Kijiji cha Mwime ambacho wananchi wengi wanajihusisha na biashara, uchimbaji wa madini na kilimo cha pamba na wapo katika eneo ambalo Barick Buzwagi wanafanya uchimbaji mkubwa wa dhahabu.
Ofisi za   kijiji hicho cha Mwime kilichopo kata ya Mwendakulima wilayani Kahama 
Mgogoro wa Maslahi wa wananchi wanaozunguka mgodi uliokuwa unamilikiwa na Barrick na sasa Accaccia uliopo  wa Buzwagi kwenye wilaya ya Kahama katika kijiji cha Mwime kilichopo kata ya Mwendamkulima  katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Unaibua mashujaa wa kutetea haki na kudai uwajibikaji u wa viongozi katika kuendeleza utawala bora na maendeleo kwa ujumla lakini mwishoni inageuka kuonekana ni maadui wa maendeleo . 
Kwa muda wa miaka zaidi ya mitano  sasa kijiji hiki kimekuwa katika pilikapilika za kuhakikisha wan-aendelea kunufaika na rasilimali yao ya madini ya dhahabu ambayo kwa sasa yanachimbwa na kampuni ya Accacia  katika mgodi wa Buzwagi kupitia Makubaliano ya Nyongeza ya Mkataba yaliyosainiwa mwaka 2007.
Kwa mujibu wa kifungu  1.1 cha Makubaliano ya Nyongeza ya Mkataba baina ya Kampuni ya Madini ya Pangea kwa niaba ya Barrick na kijiji; kampuni itakuwa ikikilipa kijiji kiasi cha Tsh milioni 60/- kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano baada ya uzalishaji kuanza na kisha pande mbili hizi zitakaa pamoja na kupitia kiwango hiki kwa kadri ya uzalishaji utakavyokuwa kwa nia ya kuboresha zaidi. Na uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huu ulianza rasmi mwaka 2009.
Nikiwa ziarani  wilaya ya Kahama nilitembelea kijiji hiki ambacho mwanzoni mwa mwaka 2007 wananchi wengi wa kijiji cha Mwime na maeneo ya karibu walijihusisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu kabla kampuni ya Pangea kuja kuchukua maeneo hayo kwa kuhodhi mashimo yaliyojulikana kwa majina ya  Zanzibar na majimaji na kuwafanya wakazi hao kuondoka hapo kupisha uchimbaji wa kisasa,
Mategemeo ya wananchi kupata maendeleo makubwa baada ya kampuni ya Pangea kuanza uchimbaji huo wa kisasa yaliendelea kufifia kila uchwao baada ya makubaliano ya kulipwa kiasi cha milioni  60 kila mwaka kwa kipindi cha miaka kipindi cha miaka mitano  cha uchimbaji  wa madini kutotimizwa kwa wakati.Licha ya kutokuwa na uelekezi rasmi wa kiseheria wa makubaliano hayo lakini yaliwafanya  wananchi wa mMwime kuendelea kuishi maisha magumu  licha ya kuwa mgodi wa Buzwagi  kuweza kufanya uchimbaji kwa muda mrefu.
Kuchelewa kwa malipo kama walivyokubaliana kulisababishwa pia na mapungufu ya uongozi wa kijiji kushindwa kufuatilia suala hilo kwa ukaribu.Sababu nyingine inayotajwa ni kwa Wanamwime wenyewe kushindwa kudai na kuwahimiza vi-ongozi wao kuchukua hatua kwa kufuatilia suala hilo.

Bi Maimuna akiwa na  mjukuu wake katika duka lake analouza pembejeo za kilimo kwa wakazi wa kijiji cha Mwime

Mraghabishi na mpambanaji wa haki za binadamu Bi Maimuna Saidi ambaye pia ni mwananchi wa kijiji hicho ambaye yeye na wenzake watano  walichukua hatua ya kuanza kuhimiza ufuatiliaji wa pesa hizo kama walivyokubaliana na baada ya mazungumzo marefu na pia ushirikishaji wa wananchi wote wa kijiji kupitia mikutano ya kijiji waliweza kufanikisha upatikanaji wa  ya million 300/ kama malipo ya mwaka 2009 – 2013 .
Mama maimuma saidi (Mwenye kilembo)akitoa  maelezo jinsi gani walivyofanikisha kupatikana kwa maendeleo katika kijiji cha Mwime kutoka katika mgodi wa Buzwagi  kwa baadhi ya waandishi wa habari na wataalamu wa mitandao ya kijamii  niliombatana nao 

 Hivyo Maimuna Said kupitia ufahamu aliopatiwa alimshawishi Diwani mara kwa mara kuweza kuchukua hatua zaidi, kwa kuwa yeye alikuwa na mamlaka zaidi.Na mwishowe kupitia harakati mbalimbali na ushirikishwaji wa wananchi wenzao walifanikiwa  kupata kiasi hicho cha pesa.
Pesa hizo pia zilitumika kuboresha shughuli mbalimbali za maendeleo na huduma za kijamii  kama ujenzi wa miundombinu ya umeme ,nyumba za manesi, nyumba ya kupumzikia wageni kama kitega uchumi lakini haya yote yalikuwa kama kipaumbele cha wananchi kufaidikapia kiasi kilichobaki kulipa baadhi ya fidia kwa wananchi waliotoa maeneo yao katika upanuzi wa barabara .
Moja ya nyumba zinazojengwa katika kijiji hiki cha Mwime kama moja ya matumizi ya pesa walizopata kutoka katika mgodi wa Buzwagi 

Huu mchakato wote usingeweza kufanikiwa kama Wanamwime wenyewe wasingesimama pamoja na kudai haki yao. Kwa hakika ili tupate tutakachotaka ni lazima tuchukue hatua za dhati pasipo kuchoka wala kukata tamaa huku tukishirikiana na viongozi wetu kwani kuna msemo unasema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu kama dhana waliotumia wanaMwime  wakafanikiwa katika harakati zao za kujiletea  maendeleo kijijini hapo. Imeandaliwa na MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG 

No comments: