Saturday, December 12, 2015

Mpiganaji Haruni Sanchawa wa Global Publishers aagwa Dar, kuzikwa Serengeti Mkoani Mara

MWANDISHI wa habari wa Global Publishers Ltd, Haruni Sanchawa, aliyefariki dunia Desemba 9 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar, ameagwa leo nyumbani kwa mjomba wake Kitunda jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea Mugumu-Serengeti, mkoani Mara, ambapo atazikwa kijiji cha Lemungololi.

Sanchawa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo, alifariki saa chache baada kuhamishiwa katika hospitali hiyo baada ya kupewa rufaa kutoka Hospitali ya Amana alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Marehemu Haruni Sanchawa enzi za uhai wake.Mke wa Marehemu, Adelina Haruni Sancha akiuagwa mwili pamoja na wanaye wawili.Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (wa kwanza mbele ) akiwa na huzuni msibani hapo.Waombolezaji wakiwa msibani.Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigiongo (wa pili kulia) na wafanyakazi wa Global wakiomboleza msibani hapo.Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers wakiomboleza.Huzuni ikiwa imetanda msibani hapo.Jeneza lenye mwili wa marehemu Haruni Sanchawa likishushwa Nyumbani kwa Mjomba wake Kitunda Dar kwa ajili ya kuagwa.Jeneza lenye mwili.Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Benedict B. Salikiwa akiongoza ibada fupi ya kumuombea marehemu.Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kampuni ya Global Publishers.Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu.Ndugu na jamaa wakiuaga mwili wa marehemu Sanchawa.Wafanyakazi wa Global wakiuaga mwili wa mpendwa wao.Mwandishi wa Habari,Gladnes Malya akisaidiwa na wafanya kazi wenzake mara baada ya kushindwa kuuaga mwili wa Sanchawa.Mhariri Mwandamizi, Walusanga Ndaki (mwenye fulana nyeupe) akitoa heshima za mwisho. Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa Sanchawa.Mhariri Kiongozi wa Gazeti la Championi, Saleh Ally (mbele mwenye miwani) na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Richard Manyota (mwenye fulana nyeusi) wakiauaga mwili wa Sanchawa.Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Oscar Ndauka akiuaga mwili wa marehemu.Mkurugenzi wa Global Publishers, Lydia James (mbele) akipita kuuga mwili wa marehemu Sanchawa.Mwili wa Marehemu ukipandishwa kwenye gari kwa ajili ya safari kwenda Mugumu, Serengeti mkoani Mara kwa Mazishi.

"MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU HARUNI SANCHAWA MAHALI PEMA PEPONI - AMEN"

No comments: