INTERNATIONAL hospitality consultancy HD Partnership (HDP) kwa kushirikiana na shirika la wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT), wanafanya mkutano wa awamu ya pili wa mwaka Disemba 7 na 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mkutano huu unahusu sekta ya ukarimu na utalii,Katika jukwaa hilo litategemea kuzungumzia ujumbe juu ya ukarimu kwa wadau wa sekta ya utalii wakiwemo wawekezaji, wamiliki wahoteli, kampuni za usimamizi, bidhaa, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, wasambazaji na watoaji huduma. Pamoja watajadili juu ya malengo yanayohusu ukarimu na utalii katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara.
Mkutano huu unahusu sekta ya ukarimu na utalii,Katika jukwaa hilo litategemea kuzungumzia ujumbe juu ya ukarimu kwa wadau wa sekta ya utalii wakiwemo wawekezaji, wamiliki wahoteli, kampuni za usimamizi, bidhaa, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, wasambazaji na watoaji huduma. Pamoja watajadili juu ya malengo yanayohusu ukarimu na utalii katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara.
Mkutano huu ambao unahusisha wadau wa ndani ya nchi na nje ya nchi, una lengo la kuchochea ukuaji endelevu wa sekta hizi kwa kutoa wataalamu husika kuongea na kutoa ushauri pia kutengeneza mazingira ya maonyesho ambayo yatatoa fursa za kubadilishana ujuzi baina ya kampuni tofauti kwenye sekta ya ukariimu na utalii. Kwa mujibu wa Meelis Kuuskler ambaye ni mshauri wa kimataifa kuhusu ukarimu na Mkurugenzi mkuu wa HDP anasema “ mkutano wa mwaka huu umejikita katika masuala maalumu ya kiutendaji yanayoathiri shughuli za kiutalii.
Ikiwa ni pamoja na mjadala kuhusu jinsi gani ya kuiinua ubora wa rasilimali watu, jinsi ya kuchochea zaidi mazingira mazuri ya biashara kwa maendeleo mapya na yaliyopo ya ukarimu, na jinsi ya kuimarisha uhusiano wa sekta zinazoingiliana kwa maendeleo endelevu ya sekta”.
Tanzania inashika nafasi ya 7 kati ya nchi 141 kwa mwaka 2015 katika ushindani wa sekta ya utalii kutokana na rasilimali za asili nyingi zilizopo, hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na jukwaa la uchumi duniani.
Hata hivyo, ripoti pia inaeleza umuhimu wa kuboresha miundo mbinu na mazingira ya kibiashara ili kuimarisha ushindani wa sekta hii kwa ujumla. Kwa mujibu wa Kuuskler anasema “Tanzania imejaliwa kuwa na mbunga za wanyama, fukwe na vivutio mbali mbali vinavutia uwekezaji mkubwa katika sekta ya ukarimu na utalii.
Hata hivyo, faida za maliasili hizi haziwezi kujulikana kwa undani zaidi mpaka masuala kama usafiri wa anga na nchi kavu, soko la ajira and sera za mazingira endelevu zimepatiwa ufumbuzi. Kwa mujibu wa Lathifa Sykes Mkurugenzi mkuu wa HAT anasema “Vikwazo hivi katika maendeleo ya sekta haviwezi kushughulikiwa ipasavyo na sekta binafsi lakini badala yake vinahitaji ukaribu na umakini zaidi wa kiutendaji wa sekta za umma”.
Waandaaji wa HRT mwaka huu wamebaini umuhimu wa kuhakikisha kuwa wanawashirikisha watendaji wa sekta za umma ili kupata mitazamo, mawazo na taarifa za kutoka kwa watendaji hao ili zishirikishwe kwenye sekta binafsi. Na mialiko imefikishwa hadi kwenye wizara ya kazi na ajira, wizara ya maliasili na utalii, idara iliyo chini ya ofisi ya rais inayoshulika na matokeo makubwa sasa (PDB) pamoja na sekta ya uwekezaji Tanzania (TIC). Kwa mujibu wa Kuuskler anasema “Uwezo wa sekta binafsi katika kutekeleza mabadiliko utakuwa bora kama utalindwa na ushirikishwaji wa wazi wa sekta za umma”. Kwahiyo pamoja na kutoa jukwaa la kuchochea ushirikiano mpya, mkutano unalenga kuendeleza na kukuza dira ya pamoja ya maendeleo na harakati za maendeleo kati ta ya wadau wa umma na binafsi.
KUHUSU MRATIBU.
HDP ambaye ni mshauri wa ukarimu wa kimataifa, anafanya kazi na wateja wetu, wamiliki, wawekezaji, shughuli za ukarimu , na mashirika ya usimamizi ili kuendesha matokeo yanayoonekana, katika kuboresha, kuendeleza, kutoa msaada wa kifedha na kuendesha shughuli kubwa na ndogo za ukaarimu pamoja na miradi kadhalika ya F&B.
Ikiwa na ofisi zilizoko nchini Dubai, HDP walileta ofisi yake nchini Tanzania mwaka 2014 ili kusaidia ukuaji mahiri na endelevu wa utalii na ukarimu katika Afrika Mashariki. Kutumia utaalamu mkubwa wa washirika, HDP inaangalia kiundani zaidi juu ya ufumbuzi wa viwango ili kuendeleza mtazamo mpya na kufanya mashirika yawe ya ushindani zaidi. Kwa njia ya uchambuzi wa hali ya juu kwa kila mteja na kuendeleza ufumbuzi wa wateja ambao unakidhi mahitaji ya shirika husika.
KIINGILIO NI BURE KWA WAJUMBE WOTE WA TANZANIA.
Kiingilio ni bure kwa wajumbe waliojisajili mtandaoni. Tunawahamasisha wamiliki hoteli, mameneja, mawakala wanunuzi, wawekezaji na wadau wote kuungana na sisi, ili muendeleze na mkuuze biashara zenu sasa.
Kujisajili tafadhali tembelea tovuti ifuatayo http://www.hospitalityroundtabletz.com/
No comments:
Post a Comment