Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akiwaamrisha askari wa getini wizarani hapo kuweka
kufuli na kutoruhusu mtumishi yoyote wa ofisi hiyo kuingia ndani ya
ofisi za wizara ilipotimu saa 1:32 asubuhi mapema leo.(Picha zote na
Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akisimamia zoezi la ufungwaji wa geti hilo, Kulia ni
askari wa SUMA JKT akiweka kufuli katika lango kuu la kuingia katika
ofisi za Wizara ya Afya.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akiwauliza askari wa getini kuhusu daftari la
mahudhurio ya watumishi wa wizara baada ya kufungwa geti hilo, na kupewa
maelezo kuwa watumishi huonyesha vitambulisho pekee na husaini katika
vitengo vyao.
Mmoja
wa wafanyakazi wa Wizara ya Afya akiwasili ofisini huku muda wa kuingia
kazini ukiwa umepitiliza. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akizungumza na
mmoja watumishi wa wizara hiyo na kuagiza kuletewa vitabu vya
mahudhurio kwa vitengo vyote vilivyopo wizarani hapo.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Afya, Michael John
akitoa maelezo kuhusu mahudhurio ya watumishi kwa Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.
Magari
ya watumishi wa Wizara ya Afya yakiendelea kuwasili ofisini bila ya
kutambua kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri, Dkt. Kigwangalla ametoa agizo la
kuizuia watumishi wachelewaji.
Askari
wa getini wakimpa maelezo mmoja wa watumishi wa wizara hiyo kuwa Mh.
Naibu Waziri ameagiza watumishi wote waliochelewa kuzuiliwa kuingia
ndani.
Mmoja
wa wasaidi wa idara ya rasilimali watu akimkabidhi vitabu vya
mahudhurio Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akipitia mahudhurio ya watumishi wa wizara kwa siku
zilizopita.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akipitisha mstari wa kufunga mahudhurio kwa
watumishi ambao wameripiti kabla ya saa 1:30 asubuhi ya leo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akiendelea na zoezi hilo la kupitisha mstari kwa
kila idara za wizara hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu juu
ukaguzi huo katika ofisi za wizara yake ya afya ili kuboresha utendaji
wa wizara hiyo na vituo vyote vya sekta ya afya nchini kote.
Na
Rabi Hume, Modewjiblog
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kingwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za
wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao
walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo
mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini.
Awali
Dkt. Kingwangalla alifika ofisini saa 1:05 asubuhi huku akiingia
ofisini kwa kutembea mwenyewe bila kutumia usafiri wa gari na kwenda
moja kwa moja ofisini kwake ambapo alitoka ilipofika saa 1:32 na kwenda
kusimama getini na kisha kuwaamrisha askari wa geti la kuingia katika
wizara hiyo kulifunga geti hilo na wasiruhusu mtu yeyote kuingia ndani.
“Fungeni geti na kila atakayefika msimruhusu kuingia ndani ninataka
kuona wote ambao wanakuja wamechelewa,” alisikika Dkt. Kingwangalla
akiwambia askari wa getini.
Baada
ya kutoa amri hiyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa
wizara hiyo, Michael John kumpa vitabu vya kusaini kwa vitengo vyote
ili aweke mstari wa kuonyesha kuwa muda wa kuingia ofisini umekwisha na
akafanya hivyo kwa kuweka mstari kwenye vitabu vya mahudhurio kuwa muda
wa kusaini kuingia umeisha.
Baada
ya kukamilisha zoezi hilo Naibu Waziri alizungumza na wanahabari kuwa
ameamua kufanya zoezi hilo katika ofisi za wizara kwa kutaka kuona ni
jinsi gani watumishi wa ofisi hiyo wamekuwa na mwitikio wa kufanya kazi
kwa kasi anayoitaka rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Alisema watumishi hao wameajiriwa na serikali ili kufanya kazi lakini
wamekuwa wakichelewa kuingia ofisini na yeye kama Naibu Waziri ana
wajibu wa kuwasimamia watumishi hao ili wafanye kazi ambayo serikali
imewaagiza kufanya.
“Nina
wiki moja tangu nimeingia hapa ofisini kuna mambo ambayo nimeyaona
hayapo vizuri na sasa naanza na hili ili tujue kuwa ni kina nani huwa
wanachelewa na zoezi hili litakuwa ni endelevu, kama mimi sitasimamia
watumishi wa serikali basi sitakuwa na kazi wizarani tunataka watumishi
ambao wanakuwa wanafanya kazi kwa kujitoa kwa ajili ya maslahi ya
taifa,” alisema Dkt. Kingwangalla.
Aidha
Naibu Waziri huyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu
kuhakikisha watumishi wote waliochelewa kufika ofisini wanaandika barua
ya kutoa maelezo kwanini wanachelewa kufika ofisini na baada ya hapo
Mkurugenzi na yeye atoe maelezo kwanini muda wa kutoka watumishi
wanakuwa hawasaini kuwa wametoka.
Pia
alishauri uongozi wa wizara ufanye mabadiliko ya mfumo wa watumishi
kuingia ofisini kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kadi au kidole
“Biometric” ili kuwa na taarifa katika mifumo ya mawasiliano kujua
wanaochelewa ofisini na wanaowahi kutoka na baada ya hapo uongozi
utajadili adhabu za kuwapa watumishi wote ambao wamekuwa wakichelewa
kufika na kuwahi kutoka ofisini.
No comments:
Post a Comment