Mfuko wa
Pensheni wa LAPF wenye makao yake makuu mjini Dodoma, umetoa msaada wenye
thamani ya shilingi 2,800,000/= kwa kituo cha Afya cha Makole. Baadhi ya vifaa vilivyotolewa
ni Mashuka 50, Vyandarua 50 pamoja na Vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwenye
kituo hicho.
Msaada huo
umelenga kuboresha huduma kwa wagonjwa wanaolazwa kituoni hapo wengi wao wakiwa
ni kina mama wajawazito na watoto. LAPF inaunga mkono jitihada za Serikali
katika kuboresha huduma za Afya nchini.
Kadhalika
katika kuadhimisha siku ya Uhuru tarehe 9 Disemba na kuunga mkono agizo la
mheshimiwa Raisi Dk. John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika kuadhimisha siku hiyo watumishi wa LAPF wakiongozwa na
Mkurugenzi mkuu Bw. Eliud Sanga wameshiriki kufanya usafi katika maeneo yote ya
nje na ndani ya kituo hicho cha Afya cha
Makole.
Mfuko wa
Pensheni wa LAPF umekuwa ukitoa misaada mbali mbali ya kijamii nchini katika
kuboresha huduma za kijamii kama elimu, maji, michezo, vituo vya kulea watoto
yatima na afya. Katika sekta ya afya LAPF imekuwa ikitoa vifaa mbali mbali kama
vitanda vya wagonjwa, vitanda vya kujifungulia, dawa, mashuka, vyandarua pamoja
kufanya ukarabati katika baadhi ya vituo vya afya kila bajeti ya misaada kwa
jamii inaporuhusu.
LAPF
inaamini kuwa misaada hii inawasaidia wanachama wake pamoja na watanzania wote
kwa ujumla, pia inawaasa wadau wengine nchini kuchangia huduma mbali mbali za
kijamii ili kuboresha maisha ya watanzania na hatimaye kuleta usawa katika
jamii.
STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akishiriki kufanya usafi katika maeneo ya kuzunguka ofisi za LAPF Dodoma pamoja na kituo cha Afya Makole.
Suala la usafu likiendelea
Baadhi ya Watumishi wa LAPF walioshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika kituo cha Afya Makole Dodoma Mjini katika kuadhimisha siku ya Uhuru.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akizungumza jambo kabla ya kabidhi Msaada wa Mashuka na Vyandarua kwa ajili ya kituo cha Afya Makole kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dr. Jasmine Tisekwa.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akikabidhi Msaada wa Mashuka na Vyandarua kwa ajili ya kituo cha Afya Makole kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dr. Jasmine Tisekwa.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akikabidhi Msaada wa vyandalua kwa ajili ya kituo cha Afya Makole kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dr. Jasmine Tisekwa.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akitoa neno la shukurani kwa niaba ya uongozi wa kituo cha Afya Makole baada ya kupokea masaada.
No comments:
Post a Comment