Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu
(kulia) akimkabidhi mshine ya kupumulia na mashuka, Mratibu wa Tiba
katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu. Makabidhiano hayo
yalifanyika mwishoni mwa wiki. Katikati yao ni Meneja Mahusiano kwa
wateja wa SGA, Sophia Luhikula.
Vitu vilivyotolewa msaada Hosipitalini hapo.
Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu
(kulia) akimkabidhi mshine ya kupumulia na mashuka, Mratibu wa Tiba
katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu. Makabidhiano hayo
yalifanyika mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mahusiano kwa wateja wa
SGA, Sophia Luhikula.
Baadhi ya watumishi wa kitengo cha Ambulance cha SGA
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu akizungumza wakati wa kutoa msaada huo.
Wafanyakazi wa SGA wakibeba msaada huo.
KAMPUNI
ya Ulinzi ya Security Group (T) imetoa msaada wa mashine moja ya kupumlia na
mashuka 40 kwa wodi ya watoto katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam
Kampuni
ya SGA ilikabidhi mashine hiyo ya kupumulia na mashuka vyote vikiwa na thamani
ya Sh milioni tano kwa wodi ya watoto Hospitali ya hapo na kusema hiyo ni
kuonyesha jinsi gani wana jali afya za watanzania ambao wanafanyakazi nao.
“Nifuraha
yetu kuona familia zetu zipo katika afya njema, lakini pia ulinzi wa mali zetu
unaenda vizuri, hivyo leo tumeona tujitoe kidogo kukumbuka jamii yetu hasa
watoto ambao ndio taifa la kesho,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa SGA, Eric Sambu.
Sambu
alisema huo ni muendelezo wa kurejesha kile wanachopata kwa jamii ili kujenga
mahusiano mazuri na wataendelea kufanya hivyo kila inapo wezekana.
Akipokea
msaada huo, Mratibu wa tiba hospitalini hapo, Dk Daniel Nkungu wanaishukuru
kampuni hiyo kuwakumbuka na kuweza kuwasaidia msaada huo ambao kwa kiasi
kikubwa utasaidia ufanisi katika utendaji kazi wao na kupunguza vifo vya watoto
wachanga.
Picha ya pamoja ilipigwa
Wafanyakazi wakiwa wameshika mashuka waliyokabidhi.
Wafanyakazi wa SGA wakirejesha mashuka hayo katika boxi.
Baada
ya hapo wafanyakazi walishiriki katika tafrija fupi ya kufunga mwaka na
kusherehekea mwaka 31 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo nchini ambapo
awali ilijulikana kama Group 4.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu akizungumza na wafanyakazi wakati wa tafrija.
Wafanyakazi wakimsikiliza...
Waliwasikiliza viongozi wao mbalimbali.
Wakuu mbalimbali wa vitengo walizungumza...
wafanyakazi walijumuika pamoja na kufurahi.
Chakula kizuri kiliandaliwa na watu walikula vya kutosha na kupata vinywaji vya kila namna
Watu walikula chakula na kufurahi,
No comments:
Post a Comment