Saturday, December 19, 2015

Benki ya NMB Plc Yatoa Msaada wa Vifaa Tiba Zahanati ya Kimara Dar

Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda (kushoto) akipokea baadhi ya mashine za kupimia mapigo ya moyo kwa mgonjwa kutoka kwa Meneja Uratibu wa NMB Plc, Thomas Kilongo. Miongoni mwa mashine zilizotolewa ni pamoja na mashine ya kupimia joto la mgonjwa, mashine 10 za kupimia 'BP' kwa mgonjwa, mashine 10 za kupimia mapigo ya moyo, mzani wa kupimia uzito na urefu kwa wagonjwa, vifaa vya kukusanyia taka, spika na kipaza sauti chake pamoja na mashine nyingine za kisasa kwa ajili ya vipimo anuai kwa wagonjwa. 

Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda (kushoto) akitoa neno la shukrani kwa Benki ya NMB Plc mara baada ya kukabidhiwa mashine mbalimbali pamoja na vifaa vya kutibia wagonjwa katika Zahanati hiyo.
Baadhi ya maofisa wawakilishi wa Benki ya NMB Plc wakiongozwa na Meneja Uratibu wa benki hiyo, Thomas Kilongo (wa tatu kulia) wakisoma orodha ya vifaa vilivyo kabidhiwa na benki hiyo kama msaada kwa Zahanati ya Kimara.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB Plc pamoja na manesi wa Zahanati ya Kimara ya jijini Dar es Salaam wakipokea baadhi ya vifaa vya msaada vilivyotolewa na benki ya NMB Plc. 
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NMB Plc pamoja na manesi wa Zahanati ya Kimara ya jijini Dar es Salaam wakipokea baadhi ya vifaa vya msaada vilivyotolewa na benki ya NMB Plc. 
Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda (kushoto) akitoa neno la shukrani kwa Benki ya NMB Plc mara baada ya kukabidhiwa mashine mbalimbali pamoja na vifaa vya kutibia wagonjwa katika Zahanati hiyo. 
Baadhi ya manesi wa Zahanati ya Kimara ya jijini Dar es Salaam na wafanyakazi wa NMB Plc wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea msaada wa mashine mbalimbali za kuchukulia vipimo kwa wagonjwa. Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 1.9. 
Mkuu wa kitengo cha huduma ya afya kwa mama na mtoto wa Zahanati ya Kimara ya jijini Dar es Salaam, Prosister Kiwango (wa kwanza kushoto) akitoa tangazo kwa wagonjwa kutumia spika pamoja na kipaza sauti kilichotolewa kama msaada na Benki ya NMB Plc kwa Zahanati hiyo. 

No comments: