Friday, December 25, 2015

ASKOFU DR MDEGELLA ATAKA WATANZANIA KUMWOMBEA RAIS DR MAGUFULI KWA KAZI NZURI


Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT( Dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegella akimpa baraka ya Christmas mtoto Monica Kasesela huku babake mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na binti yake Cathelin Kasesela wakishuhudia baada ya kumalizika kwa ibada ya pili katika usharika wa kanisa kuu

Askofu Dr Mdegela akitoa baraka

Mwalimu wa kwaya ya vijana katika kanisa kuu Bw Lupyana Samweli akipokea baraka za Christmas kutoka kwa askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegela leo mara baada ya ibada.

Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegela akimpa baraka za Chritmas mlemavu ambae ni mwimbaji maarufu wa kwaya ya vijana kanisa kuu Gift Mwanuka 

WAKATI waumini wa Dini ya kikristo hapa nchini leo wakiungana na wakristo wenzao kote ulimwenguni kusherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo , Askofu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mdegella amesifu amani iliyotawala nchini kutoka uchaguzi mkuu hadi sasa na kuwaomba watanzania kumwombea Rais Dr John Mapuguli kwa kuleta mabadiliko ya kweli ambayo hata wapinzani walikuwa wakiyataka.

"Salamu zangu na maelezo yangu ni mafupi kila mmoja anafahamu Burundi na Kenya walifanya uchaguzi na hadi leo hii bado wanauana na maisha yanakuwa magumu......ninyi mnafahamu awamu ya kwanza kuja ya pili tumevuka salama ,awamu ya pili kuingia ya tatu pia salama na awamu ya nne kuingia ya tano ndio tumevuka salama salimini zaidi kuliko awamu nyingine zote.....kwa nilitaka kuasema hata wale waliotumia mabomu na kutumia gharama kubwa wakati wa uchaguzi nafikiri walikuwa wamekosa mazoezi kwa muda mrefu ya kutumia mabomu hayo bila sababu Watanzania ni wapenda amani"

Askofu Dr Mdegella alitoa kauli hiyo wakati wa ibada hiyo ya christmas iliyofanyika katika kanisa kuu kuwa hadi hapa sasa Bwana Mungu ametusaidia na sio amesaidia uchaguzi tuo hata mambo mengine ambayo tulikuwa tunayataka kwa kuzungusha mikono kuwa mabadiliko sasa yamekuja.

Alisema kuwa Mungu si kaibadilisha Tanzania na kuipa neema katika uchaguzi mkuu pekee kwani kila mtanzania kwa sasa anaona mabadiliko kawaida ukilinganisha na awali kwani wakati wa kampeni watu walikuwa wakizungusha mikono kama ishara ya kutaka mabadiliko na mabadiliko yameanza kuonekana kwani matajiri walikuwa wamejitajirisha mno na masikini walikuwa wamekumbatia umasikini wao .

"Kulikuwepo pengo kubwa kati ya matajiri na masikini kwani matajiri walijitajirisha zaidi na masikini waliendelea kubaki masikini ila sasa kwa kipindi kifupi cha serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr Magufuli mabadiliko ya kweli yanaonekana "

Askofu Dr Mdegella mbali ya kumpongeza Rais Dr Magufuli kwa utendaji mzuri na baraza lake la mawaziri bado alitaka uzi huu wa kutumbua majibu ambao unaendelea uzidi kukazwa zaidi ili kila mtanzania aweze kufaidi matunda ya nchi yake .

" Sasa ombi langu kwenye watanzania najua Francis Godwin utaandika naomba kila mmoja wetu bila kujali ulimpa kura ama ulimnyima tuzame katika maombi kumwombea Rais wetu ili mabadiliko yaendelee na nchi iwe na amani na maendeleo pamoja na mafanikio ...kwa wale waombolezaji naomba leo kuombeleza kumshukuru Mungu na sisi wote kuungana kumwombea Rais wetu na tarehe 3 Januari 2016 wote kutoa shukurani ya pekee kumshukuru kwa kuvuka salama katika uchaguzi na kuendelea kuona neema hii ya utendaji wa Rais wetu pia kazi ya kutumbua majibu iwe endelevu kwa wakubwa na wadogo ....ukimkamanda mtu mwenye msokoto mmoja wa bangi na kumwacha mwenye gunia la bangi ikome japo sisemi mwenye msokoto mmoja asikamatwe wote washughulikiwi " 

Alisema kuwa watanzania ni watu wanapenda amani na utulivu na ndio maana wamepata kupita katika wakati mgumu wa uchaguzi mkuu pasipo kutokea machafuko yoyote." Kati ya vipindi vigumu ambavyo watanzania tumepitia kwa amani na utulivu ni pamoja na kulinda amani wakati wa uchaguzi mkuu na kuingia katika sikukuu hii ya chritmas bila amani kuvurugika"

Hata hivyo alisema kuwa amani hii watanzania tumeipata bure na kuwa kuzaliwa kwake Yesu Kristo kubisha hodi kwa kila mmoja wetu ili aweze kuingia ndani ya mioyo ya wote hivyo Kazi kubwa kumfungulia ili aweze kuingia ndani ya mioyo yetu.

Alisema kuwa Yesu Kristo amekuja ili kufanana na wanadamu wote na kuwa njia pekee ni kumpokea pasipo kushindana na Mungu .Huku mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela ambae alipata kushiriki ibada hiyo alimpongeza askou huyu Dr Mdegella kwa kumpongeza Rais Dr Magufuli na serikali ya awamu ya tano na kuwa moyo huo wa viongozi wa dini unapaswa kuendelea zaidi kwani kauli zao zinasikilizwa zaidi.

Bw Kasesela alisema amependezwa na askofu huyo kutenga muda wa kuiombea serikali na kudai kuwa kazi kubwa inayofanywa na viongozi wa serikali ya Dr Magufuli akiwemo waziri mkuu na baraza la mawaziri pamoja na watendaji wengine ni nzuri na kila mtanzania anaiona hivyo zawadi kubwa kwa watanzania ni sala na dua zao .
 

Vijana wa kanisa kuu wakiwa katika maombiMaombi maalumu kwa Taifa la Tanzania

Kwaya kuu wakiimba

Kwaya kuu wakiimba wimbo maalumu

Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela kulia akiungana na waumini wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa kanisa kuu kuliombea Taifa na serikali ya Rais Dr John MagufuliWaumini wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa kanisa kuu wakiliombea Taifa wakati wa ibada ya Chritsmas

Askofu Dr Mdegela akitoa salamu za Christmas leo


Askofu Dr Mdegella akitoa baraka kwa waumini wa kanisa kuu leo
Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT( Dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegella akimpa baraka ya Christmas mtoto Monica Kasesela huku babake mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na binti yake Cathelin Kasesela wakishuhudia baada ya kumalizika kwa ibada ya pili katika usharika wa kanisa kuu

Dereva maarufu wa Taxi eneo la Posta mjini Iringa Bw Sisico akiwa katika vazi la Christmas

Na MatukiodaimaBlogNo comments: