Thursday, December 24, 2015

Asasi ya Tushikamane Pamoja Foundation (TPF) yawaandalia Wazee wasiojiweza sherehe ya Krismas na Mwaka Mpya Courtyard protea hotel jijini Dar es salaam

Taswira za shughuli malumu ya chakula cha mchana iliyofanyika pale Courtyard Protea hotel ya Sea View jijini Dar es salam  kwa ajili ya wazee wasiojiweza wanaosaidiwa na Asasi ya Tushikamane Pamoja Foundation siku ya Jumamosi tarehe 19 Desemba, 2015. 
Shughuli iliandaliwa na uongozi wa  Protea na Rickshaw kwa ajili ya kusherehekea Krismas na mwaka mpya. Jumla ya wazee 60 na wajukuu wao  walikaribishwa na kusaidiwa na wafanyakazi wa Protea. Viongozi pamoja na wahudumu waliopokea wageni wao kwa kujituma na uchangamfu mkubwa.
Mama akisubiri kupelekwa kwenye meza yake
Mmoja wa wazee akisaidiwa kupelekwa mezani 
Mmoja wa wazee hao akisaidiwa kuketi 
Bibi akiongozwa kuketi
Pasina kujali nyadhifa zao mafisa wa Courtyard Protea hotel walisaidiana na wahudumu kuhudumia wazee hao kwa furaha na upendo
Bibi akisaidiwa kuketi mezani
Mwenyekiti wa TPF  Mama Rose Mwapachu akikawashukuru Viongozi na wafanyakazi wa Protea na Rickshaw kwa shughuli hiyo iliyofana sana 
Asante sana mwanangu...anaonekana kusema bibi huyu wakati akiandaliwa chakula
Mzee Hashim Ismail Mkurugenzi mkuu wa Protea akimsaidia Mzee Mchopa asieona.
Sister kutoka Msimbazi Kijiji cha wazee nae alikuwepo pamoja na wazee kutoka Kijiji hicho.
Mmoja wa wazee akiendelea kupata vinywaji na chakula
Zawadi zilitolewa kwa wazee hao
Mama Mariam akitoa zawadi kwa wazee
Wakurugenzi wa Protea  wakifurahia kula pamoja na wazee
ikundi cha Tushikamane Pamoja Foundation wakishirikiana na Rickshaw Travels kwa pamoja wanasaidia Wazee wasiojiweza na wenye mahitaji.  Walipata bahati ya kukaribishwa pamoja na wazee kupata chakula cha mchana na Hoteli ya Courtyard Protea na Rickshaw.  

No comments: