Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fadhil Nkurlu akifungua rasmi Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha.
Mwenyekiti wa muda wa Mkutano wa Baraza la Madiwani Jijini Arusha, Ndg. Daniel Machunda ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha akikabidhi madaraka hayo kwa Mstahiki Meya mara baada ya kuchaguliwa kwa kura 33 kati ya kura 34 zilizopigwa.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Juma Iddi ambaye pia ni Katibu wa Mkutano wa Baraza akitoa muongozo wa namna Mkutano huu wa kwanza unavyoendeshwa kwa mujibu wa kanuni,kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda.
Diwani wa Kata ya Sokoni, Mheshimiwa Calist Lazaro Bukhai(Chadema) akikishukuru baada ya kuchaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Arusha.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha ,Mhe Calist Lazaro Bukhai akiwa na Naibu Meya wake Viola Lazaro Likindikoki kwenye Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Kaloleni Mhe Lewis Kessy (Kushoto) na Diwani wa Kata ya Levolosi Mhe. Efatha Nanyaro wakiwa kwenye Kikao cha kwanza cha Baraza la madiwani wa Jiji la Arusha.
Mhe. Abdulrasul Tojo (kulia) ambaye ni diwani pekee wa CCM kwenye Baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha alipokua akiomba kura katika nafasi ya Naibu Meya wa Jiji hilo.
Mstahiki Meya Mhe. Calist Bukhai (aliyevaa Taji), Naibu Meya Mhe. Viola Likindikoki (tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fadhil Nkurlu (nne kulia), Mkurugenzi wa Jiji, Ndgugu Juma Iddi (tatu kulia) pamoja na Madiwani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Kikao cha Baraza la madiwani.
No comments:
Post a Comment