Wafanyakazi wa Benki ya CRDB mkoa wa Arusha wakishindana kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
Watoto wakifurahia michezo mbalimbali katika viwanja vya Olasiti Garden
leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo hufanyika kila mwaka
na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za
wateja.

wateja
leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo hufanyika kila mwaka
na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za
wateja
Watoto wakimkimbiza kuku katika mashindano yaliyofanyika kwenye sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja
Malindi band ya mkoani kilimanjaro ikitumbuiza sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la USA akikabidhi zawadi kwa mtoto |
Habari picha na Woinde Shizza, Arusha.
BENKI ya CRDB imeendelea kukuza kipato cha familia nyingi nchini za hali yachini, kati na juu kwa kuwahimiza wateja wake kufanya uwekezaji wenye tija pamoja na kujiwekea akiba kwa maisha ya baadae.
Hayo yameelezwa Meneja wa Benki ya CDRB tawi la Usa lilipo mkoani
Arusha Jenipher Tond wakati wa maadhimisho ya siku ya Familia ya CRDB iliyofanyika katika viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha na kuzikutanisha familia mbalimbali za wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia za wateja wa benki hiyo waishio jijini Arusha.
Meneja huyo amesema kuwa benki hiyo inaendelea kuhamasisha uwekezaji na kutoa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kuinua pato la mwananchi mmoja mmoja hadi kwa taifa.
Meneja wa benki hiyo tawi la Meru Leonce Mathey amesema kuwa benki hiyo
imesogeza karibu huduma kwa wananchi ikiwemo boda boda ,mama ntilie pamoja na wajasiriamali kwa kuanzisha matawi katika maeneo ya masoko .
Leonce amewataka wafanyakazi wa CRDB kutumia vyema siku familia kwa kukaa karibu na familia zao na kufurahi pamoja kwani muda mwingi wanautumia katika kufanya kazi za kuwaingizia kipato .
“Kama kwenye familia mambo hayako vizuri nyumbani hata kazini mambo hayatakua vizuri ni vyema kuhakikisha mazingira yanakua mazuri kuanzia kwenye familia mpaka kazini” Alisema Leons.
Kwa upande wake Mteja wa benki hiyo Pendo Shoo amesema kuwa benki hiyo imemsaidia kuwalipia watoto wake ada kupitia akaunti ya Junior Acount ambazo huwawezesha pia kupata mikopo kwa ajili ya kuwaendeleza watoto kielimu.
Benki ya CRDB ina matawi 8 na matawi mengine madogo madogo bado yataendelea kuanzisha ili kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.
Benki ya CRDB ina matawi 8 na matawi mengine madogo madogo bado yataendelea kuanzisha ili kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.
Siku ya familia ya CRDB iliambatana na michezo na burudani ambazo
zilipamba siku hiyo ikiwemo mchezo wa kuvuta kamba ,kukimbia na yai mdomoni pamoja na burudani ya muziki .
No comments:
Post a Comment