Thursday, November 19, 2015

Vodacom Foundation yatoa msaada wa vifaa vya elimu Kisarawe

Wanafunzi wa shule ya msingi Chazinge A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani wamenufaika kwa kupatiwa msaada wa vifaa vya elimu kutoka taasisi ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation.Vifaa hivyo ambavyo vimetolewa jana ni madaftari ya kuandikia na mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set)pamoja na kalamu.

Akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa hivyo kwa wanafunzi jana,Kaimu Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia alisema elimu ni moja ya kipaumbele ambacho taasisi hiyo inatoa na vipaumbele vingine vikiwa ni kusaidia kuboresha sekta ya afya.

“Vodacom Foundation tunaelewa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na hakuna jamii ambayo inaweza kuendelea bila kutoa elimu kwa watu wake ndio maana tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu nchini”.Alisema Mworia.

Alisema kuwa taasisi ya Vodacom Foundation pia inaendelea kutekeleza mkakati wake wa kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hususani zile zinazomilikiwa na serikali wanapatiwa kompyuta za kuwawezesha kusoma somo hili kwa vitendo ili wasiachwe nyuma katika karne hii ya sayansi na teknolojia.

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake baada ya kupokea msaada huo mwanafunzi Aisha Salum anayesoma darasa la nne shuleni hapo alitoa shukrani kwa msaada huo “Tunashukuru Vodacom Foundation kwa kutupatia vifaa na tuna imani vitatusaidia katika masomo yetu.
Mwanafunzi wa darasa la sita Jonson Khamsini (wa pili toka kushoto) wa shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani akipokea vifaa vya elimu-madaftari,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set) pamoja na kalamu toka kwa Kaimu Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kulia) ikiwa ni msaada ulitolewa na kampuni hiyo kupitia taasisi ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.
Kaimu Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kulia)akimkabidhi Mariam Yusuf msaada wa vifaa vya elimu,madaftari,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set)ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.Msaada huo ulitolewa na kampuni hiyo kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani,wakigawiwa vifaa vya elimu na Kaimu Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kulia) vikiwemo,madaftari,kalamu,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set) ikiwa ni msaada uliotolewa na kampuni hiyo kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.
Meneja Biashara wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kulia) akiwagawia vifaa vya elimu wanafunzi wa shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani, vifaa walivyokabidhiwa ni,madaftari,kalamu,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set) ikiwa ni msaada uliotolewa na kampuni hiyo kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani,wakifurahia na kuviinua juu vifaa vyao vya elimu, Vikiwemo,madaftari,kalamu,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set) ikiwa ni msaada uliotolewa na Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.
Wanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Chazige A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani,Jonas Mkwagi (kushoto) na Khamis Haji(kulia) wakishirikiana na Meneja wa Vodacom Foundation,Sandra Oswald (katikati) kubeba boksi lenye vifaa vya elimu vikiwemo madaftari,kalamu,Mikebe yenye vifaa vya kusomea somo la hisabati (Mathematics set) ikiwa ni msaada uliotolewa na Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya jamii ya Vodacom Foundation hivi karibuni.

No comments: