Sunday, November 22, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Shirika la maendeleo ya mafuta na petrol (TPDC) nchini linatarajia kuzindua awamu ya pili ya utafiti wa mafuta kwa kutumia ndege maalum kwa mikoa ya Arusha, Singida,Tabora, Shinyanga, Simiyu na Lindi . https://youtu.be/pcQpoKgwnHo

Katika hali isiyokuwa ya kawaida gari dogo aina ya Cresta laacha njia na kuangukia korongoni huku dereva akitoka salama. https://youtu.be/bClG9nGUMpk

Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mapema mwezi ujao limeadhimia kutumia mfumo mpya wa sheria ya usalama barabarani, kufuatia ongezeko la ajali za barabarani. https://youtu.be/ZouwzPNeCkw

Baadhi ya wazazi wenye watoto wenye midomo sungura waeleza changamoto wanazokutana nazo watoto wao ikiwemo kushindwa kupumua na kula vizuri.https://youtu.be/SaE9NjLwaTE

Uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Ulanga wafanyika hii leo huku kukiwa na mwamko mdogo wa wapiga kura. https://youtu.be/CGWjAgXoPrQ

Jamii ya kisingasinga inayoishi jijini Dar es salaam yajitolea damu kwa ajili ya kusaidia wagonjwa mbalimbali wenye mahitaji ya damu. https://youtu.be/ghHTC8NjMYc

Kata takribani 6 nchi nzima zimefanya uchaguzi wa madiwani hii leo baada ya kuhairishwa hapo awali huku mwitikio wa wapiga kura kwenye kata ya Boma Ng’ombe Mkoani Kilimanjaro ukiwa mdogo. https://youtu.be/xVz7M7MJops

Watu 4 akiwemo mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja Wilayani Mbinga wanusurika kifo baada ya kunywa togwa iliyowazuru. https://youtu.be/RK3BZekEXIY

Mfuko wa bima ya taifa ya bima ya afya ya NHIF wasema haihusiki na huduma duni zinazotelewa katika vituo vya afya, zahanati na hospitali mbalimbali zinazoshirikiana na mfuko huo. https://youtu.be/L4PDYftljUU

Mmoja wa manusura wa ajali ya machimbo ya Nyangarata wilayani Kahama waliokaa shimoni kwa siku 41 afariki dunia; https://youtu.be/eJeODqFEReI

Mtu mmoja amefariki Mkoani Tabora mara baada ya kutumbukia kisimani  wakati akijaribu kutafuta simu yake iliyotumbukia kisimani humo wakati alipokuwa akiteka maji; https://youtu.be/Gu0d-Q2I9kU

Serikali nchini inatarajia kuanzisha  mradi wa utafiti wa utoaji wa huduma ya afya ya mzazi na mtoto kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kwa lengo la kukabiliana na vifo vitokanavyo na uzazi;  https://youtu.be/cuJ81blNzBs

Wananchi wa jimbo la Lushoto Mkoani Tanga wajitokeza kupiga kura ya kumpata kiongozi atakaye wawakilisha huku bado mwamko wa wapiga kura ukitajwa kuwa mdogo; https://youtu.be/U6IcEojvjwU

Watu 140 wenye tatizo la kupasuka midomo kutoka mikoa ya shinyanga,Geita na Mwanza wanatarajia kufanyiwa upasuaji kuanzia novemba 23 mwaka huu mkaoni mwanza; https://youtu.be/fth2WjzckcI

Timu ya taifa ya kilimanjaro Stars imeanza vyema michuano ya kombe la Challenge inayoendelea huko nchini Ethiopia mara baada ya kuitandika Somalia goli 4 kwa 0;https://youtu.be/HV-yU5URMLU

Klabu ya Real Madrd imeangukia pua mara baada ya kutandikwa goli 4-0 kutoka kwa mahasimu wao klabu ya Barcelona; https://youtu.be/ovSK6itw6ro

Baadhi ya wanaume nchini watajwa kuwa moja ya chanzo cha vifo vya wanawake vinavyotokana na saratani ya shingo ya uzazi; https://youtu.be/MopqhHrBYvE

Tanzania yaelezwa kuwa miongoni mwa nchi ambazo bado zinakabiliwa na uhaba wa wataalamu wa upasuaji wa midomo Sungura; https://youtu.be/F83Qh2uog5U

Mamlaka ya hifadhi za wanyama pori nchini TANAPA yaendelea kujidhatiti katika kupambana na tatizo la ujangili nchini; https://youtu.be/o8s9t7aIKdA

Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimesema kinapeleka shauri mahakamani la kutaka kibali cha kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa Mkoa wa Geita marehemu Alphonce Mawazo;https://youtu.be/4WPYtkMpGlA

Wachezaji wa zamani wa Tanzania stars na wale wa Zanzibar Heroes wameandaa mchezo maalumu kwa lengo la kuhamasisha amani katika visiwa vya Zanzibar;https://youtu.be/KSYIx_8AisU

Kocha wa klabu ya Real Madrid amewataka wachezaji wake kusahau kipigo walichokipata kutoka kwa mahasimu wao Barcelona; https://youtu.be/zhZ0krY307o

No comments: