NA BASHIR YAKUB -
Unapomdai mtu kupitia mahakanma na hukumu ikatolewa kuwa ni kweli unamdai na anastahili kukulipa basi mtu huyo hustahili kulipa. Lakini mara kadhaa hutokea mtu kusema sina hela ya kulipa au vinginevyo ilimradi tu asilipe deni.
Lakini pia madai hapa si lazima iwe hela tu inayotokana na kukopeshana. Yapo pia madai ambayo hutokana na mtu kushinda kesi. Kwa mfano mwanamke alifungua kesi dhidi ya mme wake akitaka matunzo yake na ya mtoto/watoto. Au shauri limekwisha na mtu aliyeshindwa ametakiwa na mahakama kulipa gharama. Au malipo ya fidia na mengineyo yote ambayo huamuliwa na mahakama kuwa yalipwe. Haya yote unaweza kuyafanya yalipwe kwa kukamata mshahara wa mhusika kwa njia za kisheria .
Hatua hii imeelezwa katika amri ya 21 ya kanuni ya 47 ya sura ya 33 ya sheria ya mwenendo wa mashauri ya madai.
1.HATUA YA KUKAMATA MSHAHARA WA MTUMISHI.
Mahakama inapotoa hukumu ikimtaka mtu fulani kutekeleza jambo fulani au kulipa kiasi fulani kwa mtu fulani amri hiyo hutakiwa kutekelezwa kwa hiari na si vinginevyo. Yule aliyeamrishwa hutakiwa kutekeleza kama alivyoagizwa na ndani ya muda alioelezwa. Ikiwa atatekeleza bila kukosa basi hatua hizi za kukamata mali zake ikiwemo hii ya kukamatwa kwa mshahara wake hazitachukuliwa. Hii ni kwakuwa atakuwa ametekeleza kwa hiari. Hatua za kukamata mali zake ikiwemo mshahara wake huchukuliwa ikiwa kama njia ya kumlazimisha mtu kutekeleza kile alichokataa kutekekeza kwa hiari .
2. KUKAMATA MSHAHARA WA MTUMISHI WA SERIKALI.
Watumishi wa serikali huwa na taratibu za malipo ambazo zipo tofauti na taasisi binafsi. Lakini pia hata ndani ya serikali yenyewe idara na taasisi nazo huwa na taratibu tofauti katika malipo. Kwa mfano wapo watumishi ambao mishahara yao huanzia hazina na wapo ambao utaratibu wao wa mishahara hauanzii huko. Hivyo basi ikiwa malipo ya mtumishi huanzia hazina basi mamlaka za hazina zitapewa taarifa ya kimahakama itakayoeleza kile alichofanya mtumishi ikiwa ni pamoja na ile amri ya kukamata mshahara wa mtumishi kulipia deni kwa mujibu wa hukumu na tuzo(decree) . Wahasibu na watoa malipo(cashier) watalazimika kufuata vilevile kama ilivyoamriwa na mahakama .
3. KUKAMATA MSHAHARA WA MFANYAKAZI ASIYE WA SERIKALI.
Ikiwa mshahara unaotakiwa kukamatwa kufidia deni ni wa mfanyakazi asiye wa serikali basi taarifa rasmi itatolewa kwa mwajiri wake kama ni kampuni, asasi ya kiraia au vinginevyo. Mwajiri atatoa taarifa hiyo kwa afisa anayehusika na malipo ili kuanzia hapo mshahara wa mhusika utumike kulipia deni kwa mujibu wa agizo la mahakama.
4. KUKAMATA MSHAHARA NUSU AU WOTE.
Kwa mujibu wa sheria niliyotaja hapo juu mshahara wa mfanyakazi unaweza kukamatwa wote kwa ujumla wake au sehemu yake kutegemea na maamuzi ya mahakama. Ikiwa deni ni kubwa sana basi inaweza kuamuliwa kuwa kiasi fulani kiwe kinakatwa kila mwezi labda kwa kipindi cha miaka miwili au mmoja kutegemea na deni lenyewe. Au kama mshahara ni mkubwa na upo uwezekano wa kulipa deni kwa mkupuo mmoja(single installment) na likaisha basi inaweza kuamuliwa mshahara ukamatwe wote na ulipie deni kwa mkupuo mmoja ili deni liishe kabisa.
Hata hivyo katika mashauri yanayohusisha familia kama matunzo ya watoto, ada, mavazi, malazi na matunzo ya mwanamke mara nyingi huwa inaamriwa kiasi fulani kila mwezi kikatwe na kiingie katika akaunti ya mwanamke au kipelekwe mahakamani kwa ajili ya matunzo kwa familia hiyo.
5. MALIPO KUFANYIKA HATA KAMA MFANYAKAZI YUKO NJE YA MKOA.
Ikiwa kesi imefunguliwa mkoa fulani na mfanyakazi anakofanyia kazi ni mkoa mwingine bado hili halizuii mshahara kukamatwa. Popote anapofanyia kazi na popote ofisi yake ilipo mshahara utatakiwa kukamatwa na kulipia kile anachostahili kulipia. Yote hayo ni kwa mujibu wa amri ya 21 ya kanuni ya 47 ya sura ya 33 ya sheria ya mwenendo wa mashauri ya madai.
MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.

No comments:
Post a Comment