Monday, November 9, 2015

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YAFANA SANA JIJINI MONTREAL, CANADA

Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Utalii ambayo yamedumu kwa siku tatu mfululizo katika jiji la Montreal nchini Canada yafana sana. Ubalozi wa Tanzania, Ottawa nchini Canada ulikuwa ni mmoja wa washiriki kati ya washiriki waonyeshaji 400 walioalikwa na sekta ya utalii ambayo ndiyo muandaaji rasmi wa maonesho hayo.

Maonyesho hayo ambayo yamefanyika katika mahali maarufu  la “la Place Bonaventure” katika jiji la hilo, ambalo liko upande wa Mashariki mwa Canada, eneo ambalo wengi wa wakazi wake huzungumza Kifaransa, yamekuwa na hamasa na mashiko makubwa mwaka huu kwa kupata wahudhuriaji zaidi ya elfu thelathini na tatu (33,000).

Kutokana na wingi wa watu, wakiwemo watalii wanaopenda kuzuru nchi mbalimbali, waliohamasika kuhudhuria maonesho hayo, Balozi wa Tanzania Mhe. Jack Mugendi Zoka aliamua kuwa kati ya waonyeshaji na watoa taarifa za vivutio vya utalii katika banda lake kama ionekanavyo katika picha hapo chini.

Aidha, mabalozi wa nchi mbalimbali walifika katika banda la utalii la Tanzania kujionea ni jinsi gani limeweza kuwa kivutio cha watalii wengi. Balozi wa nchi jirani ya Kenya alikuwa miongoni mwa watembeleaji katika banda hilo.

Kati ya mambo yaliyoonyesha kuwavutia watalii hao na hatimaye kutoa ahadi ya kutembelea Tanzania ni: Mlima mrefu kuliko yote Afrika, Kilimanjaro, ambao sasa wamefahamu uko Tanzania, mbuga za wanyama na kisiwa kinachonukia marashi ya karafuu cha Zanzibari.

Kutoka Tanzania Wizara ya Maliasili na Utalii iliwakilishwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ambao walikuwa sambamba za Kampuni Binafsi ya Wasafirishaji Watalii ya ZARA (Zara Tours). Banda la Utalii la Tanzania ambalo lilisimamiwa na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania, Ottawa liligawa zaidi ya vipeperushi elfu kumi (10,000) kwa watu waliolitembelea.
Banda la Tanzani lawavutia wageni mbalimbali ambao hawachelei kufika na kujionea wanayojili.
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka (Katikati) akishirikiana na waonyeshaji kutoa maelezo ya vivutio vya utalii vya Tanzania. Kulia kwa Mhe. Balozi ni Mke wa Balozi, Bibi Esther Nyanzila Zoka. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Bw. Salumu Mayombo wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bibi Aziza Bukuku na Desire Masire wa Ubalozi wa Tanzania, Ottawa.
Afisa wa Ubalozi, Bw. Richard Masalu akiwahamasisha watalii kuitembelea Tanzania.
Watalii wafurika katika banda la Tanzania. Waonyeshaji wakitoa maelezo ya vivutio vya utalii vya Tanzania. Kutoka juu ni Bw. Salumu Mayombo wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bibi Aziza Bukuku na Bw. Desire Masire wa Ubalozi wa Tanzania, Ottawa; na Bibi Mariam Adam wa Zara Tours.
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka (katikati) akishirikiana na waonyeshaji kutoa maelezo ya vivutio vya utalii vya Tanzania. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Bw. Salumu Mayombo wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bibi Aziza Bukuku na Bw. Desire Masire wa Ubalozi wa Tanzania, Ottwa.
Waonyeshaji wa banda la Tanzania akipanga mikakati kabla nafuriko ya watu hayajawavamia. Kutoka kushoto ni Bw. David Mshana na Salumu Mayombo wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Anayewafuatia ni Mwanadiaspora anayeishi Montreal , Bi. Veneranda Mamiro. Katikati ni Mabalozi wa Tanzania na Kenya, Ottawa, Mhe. Jack Mugendi Zoka na Mhe. John Lepi Lanyasunya; na kushoto ni Bw. Adam Rashid wa Zara Tours. Waliotupa mgogo ni watalii.
Mwonyesha wa banda la Cuba akitoa maelezo kwa Balozi wa Tanzania, Ottawa na Mwakilishi wa Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (katikati) alipotembelea katika banda hilo. Kushoto kwa Balozi ni afisa wa Ubalozi, Bw. Paul J. Makelele akifuatiwa na mke wa Balozi, Bibi Esther Nyazila Zoka.
Mmoja kati ya watalii waliowahi kuitembelea Tanzania kwa nyakati mbalimbali akisifia vivutio vya utalii na utamaduni wa Kitanzania, kwa lugha ya Kiswahili mbele ya Balozi wa Tanzania, Ottawa, Mhe. Jack Mugendi Zoka.
Balozi wa Kenya , Ottawa Mhe. John Lepi Lanyasunya (katikati aliyevaa skafu nyeupe) ni miongoni mwa mabalozi waliotembelea banda la Tanzania. Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania, Ottawa, Mhe. Jack Mugendi Zoka na kushoto kwake ni Bibi Mariam Adam na Bw. Adam Rashid wa Zara Tours.

No comments: