Thursday, November 12, 2015

JUMUIYA YA ULAYA (EU) YATOA EURO 200,000 KWA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI TANZANIA

Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi akifafanua jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano wa EU, Eric Beaume. (Picha na Francis Dande)
 Balozi wa Jumuiya ya  Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) akibadilishana hati na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jumuiya ya  Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) akisaini hati na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. 
 Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza katika hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000.
 Na Mwandishi Wetu

JUMUIYA ya Ulaya (EU)imetiliana saini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN), ruzuku Euro 200,000 sawa na sh. Milioni 478.

Utilianaji saini huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya UN nchini , Alvaro Rodriguez na Balozi wa EU, Filiberto Sebregondi.
Sebregondi alisema Tanzania imefanikiwa kutengeneza mfano wa namna bora Mashirika ya UN yanavyoweza kufanyakazi kama taasisi moja katika kuboresha maisha ya watu.

Naye Rodriguez, alisema fedha hizo zimelenga kusaidia miradi ya pamoja ya EU NA UN ya mawasiliano, uragibishi, uimarishaji wa ufuatiliaji na uwazi.
Rodriguez, alisema msaada huo ni muhimu katika ufanisi wa maendeleo kwa Tanzania wakati nchi inajipanga kutekeleza malengo ya endelevu SDGs.

“Nchi ina Rais mpya na inahitaji kuwa ya kipato cha kati sisi UN na washirika wetu ni vyema tukaunga jitihada hizi ili kusiwepo na mtanzania atakayeachwa nyuma katika mchakato wa maendeleo,” alisema.

No comments: