Tuesday, November 17, 2015

JAMVI LA VIJANA LA UMATI MWEZI HUU LIMEKUWA CHACHU YA KUHAMASISHA VIJANA KATIKA MASUALA YA AFYA YA UZAZI

 Vijana wa YAM ( Youth Action Movement) ambao ni waandaaji wa tamasha hili linalofanyika kila mwezi wakionesha igizo lao lililobeba ujumbe unaosema ni jukumu la wazazi kuwaelimisha vijana juu ya afya ya uzazi na ujinsia ili kuwakinga na maambukizi ya VVU mimba katika umri mdogo na ngono katika umri mdogo.
Mwenyekiti wa UMATI dar es salaam Mr.Harith Shomvi ambae alikuwa mgeni rasmi  katika tamasha hilo akihutubia wananchi na kuwasisitiza wapate huduma za uzazi wa mpango na upimaji ambazo zilikuwa zikitolewa bure katika tamasha hilo. Tamasha hilo lilikuwa na kauli mbiu isemayo "JE kutoa  elimu  juu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana ni jukumu la nani?
 Baadhi ya wananchi wakijiandikisha ili waweze kupata huduma ya upimaji VVU na uzazi wa mpango zilizokuwa zikitolewa bure na UMATI katika tamasha hilo la jamvi la vijana.
 Mtoa huduma wan UMATI Bibi. Neema Orgeness akimpima mteja VVU.
 Mtoa huduma wa UMATI Monika Nkwera akimpatia mama huduma ya uzazi wa mpango wakati wa Tamasha la Vijana lililofanyika jijini Dar es Salaam mapema wikiendi hii. Tamasha hilo lilikuwa na kauli mbiu isemayo "JE kutoa  elimu  juu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana ni jukumu la nani?
Kikundi cha nyota kutoka Temeke wakionesha igizo linaloelezea umuhimu wa wazazi kuwapa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia watoto wao ili kuwaepusha na ngono katika umri mdogo,mimba katika umri mdogo,VVU/UKIMWI,na pia athari zingine zitokanazo na ukosefu wa elimu na habari sahihi kuhusu afya ya uzazi na ujinsia.
Picha na Maelezo.

No comments: