Tuesday, November 24, 2015

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI


Baada ya uteuzi wa waziri Mkuu Kassim Majaliwa,fumbo la baraza la mawaziri laendelea kutesa vichwa vya watu wengi huku Wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wakitoa maoni yao. https://youtu.be/lu0uKdIO00s

Wachambuzi mbalimbali nchini waendelea kutoa mitazamo na maoni yao juu ya baraza jipya la mawaziri la serikali ya awamu ya tano. https://youtu.be/BlpbU4iOQTc

Serikali ya Ujerumani yaipatia Tanzania msaada wa ndege mbili maalum kwa ajili ya kufanya doria katika mbuga mbalimbali ili kusaidia juhudi za kudhibiti ujangili. https://youtu.be/zZ_3w3Gn7lA

Wananchi mkoani Kagera wajitokeza kusindikiza mwili wa aliyekuwa mtangazaji na mwandaaji wa vipindi Prince Baina Kamukulu. https://youtu.be/WC3TUyzNuPE

Imeelezwa kwamba vitanda 120 kati ya 300 vimefungwa katika taasisi ya MOI ya hospitali ya Mhimbili ili kuwezesha wagonjwa kupata huduma hiyo. https://youtu.be/3D_rZNe5a2Q

Baada ya kukamilika kwa uchaguzi mdogo katika jimbo la Ulanga mkoani Morogoro hapo jana, Chama cha Mapinduzi CCM kimefanikiwa kutetea jimbo hilo. https://youtu.be/130r6grz24U

Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Lushoto mkoani Morogoro amemtangaza mgombea wa CCM kuwa mshindi wa kiti cha ubunge katika jimbo hilo kufuatia uchaguzi mdogo uliofanyika hapo jana. https://youtu.be/XucfToyEQKA

CH10: Raisi John Magufuli afuta sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya uhuru na badala yake kuwataka wananchi kufanya usafi siku hiyo. https://youtu.be/m-Ndw_TwAx8

Serikali imetoa siku tatu kwa kampuni ya Philips inayotengeneza mashine za CT SCAN na MRI kukamilisha matengenezo yake ili ziweze kuwapatia huduma wagonjwa katika hospitali ya Mhimbili.https://youtu.be/K9QcKge67VU

Wakazi wa ubungo darajani na ubungo maziwa wailalamikiwa TANESCO kwa kushindwa kutekeleza makubaliano ya kuwalipa fidia baaa ya kuhama maeneo yao yaliyo jirani na mitambo ya umeme. https://youtu.be/v6OvTIQMA4I

Waziri mkuu Kassim Majaliwa awataka wafanyakazi katika ofisi ya waziri mkuu kutambua jukumu walilonalo kwa kuwahudumia wananchi wakati akizungumza na wakuu wa taasisi. https://youtu.be/_LJRR3y4nl0

Tanzania yateuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya urithi wa dunia kwa kipindi cha miaka 4 kufuatia mkutano wa UNESCO ulifanyika nchini Ufaransa. https://youtu.be/RAi6Kl6gxBA

Jeshi la polisi nchini latoa onyo kufuatia tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi baada ya takwimu kuonyesha wastani wa jumla ya watu 3 kuuwawa kila siku nchini. https://youtu.be/4Hn_QDH-9o0

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetupilia mbali sherehe za maadhimisho ya uhuru ;https://youtu.be/EF6XOuxtixY

Mkuu wa wilaya ya Bokombe Mhe.Amani Mwenegoha amemfukuza kazi Dkt. Johanes Makobwe kwa madai ya kukataa kumuhudumia mgonjwa; https://youtu.be/7IQ4BE5SN_k

Wanafunzi wa shule ya msingi Nanyati mkoani Mtwara waelezwa kusomea chini ya mti kutokana na ukosefu wa majengo; https://youtu.be/tdQ2rKmvMsQ

Wawakilishi wa wanawake kutoka kanda tano za Afrika wamekutana mkoani Arusha kwa lengo la kupigania haki ya mwanamke katika kumiliki rasilimali za nchi; https://youtu.be/-2xluiOx310

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimefungua kesi ya madai katika mahakama kuu kanda ya Mwanza kutengua zuio la jeshi la polisi kuhusu kuagwa kwa mwili wa marehemu Alphonce Mawazo;https://youtu.be/EUNGOklcPXs

Zaidi ya tani 250 za miwa Wilayani Kilombero mkoani Morogoro zimetupwa kwa madai kuwa hazifai kwa kutengeneza sukari; https://youtu.be/H7m4cLQ5_Mg

Inaelezwa kuwa Sepp Blatter pamoja na Michel Platin wako hatarini kufingiwa miaka saba kutokujihusisha na masuala ya mpira wa miguu;https://youtu.be/eWXZxgwUSVQ

Rais John Magufuli amewaagiza viongozi wote wa serikali kusimamia vilivyo zoezi la usafi ifikapo December 9 ili kupambana na kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu; https://youtu.be/mCaeujNkPwY

Waziri mkuu mteule Mhe.Kassim Majaliwa amewataka watumishi wanaofanya kazi katika ofisi yake kuwajibika kikamilifu; https://youtu.be/cEY-vM4AdoQ

Baadhi ya wananwake mkoani Shinyanga wamelalamikia vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya waratibu wa mradi wa TASAF mkoani humo; https://youtu.be/KHOYX8dnDcA

Inaelezwa kuwa zaidi ya wafanyakazi 130 wa migodi ya North Mara,Buzwagi pamoja na Bulyanhulu wanatarajiwa kupunguzwa kazi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ; https://youtu.be/k2me11i1zjg

Jeshi la polisi nchini limeitaka jamii kutumia mfumo wa Tehama katika kuibua matendo ya uhalifu ndani ya jamii badala ya kujichukulia sheria mkononi; https://youtu.be/HZD3nprwK-0

Inaelezwa kuwa mauzo ya hisa katika soko la hisa la Dar es Salaam DSE yameongezeka kwa asilimia 57;https://youtu.be/i37WJrtH3a0

Wadau wa uzalishaji wa sukari nchini wameendelea kumsifia Rais Magufuli kwa hotuba yake aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa bunge la 11; https://youtu.be/jraXO4gxt7M

Benki ya Exim imetangaza uuzaji wa hati fungani ya mda mrefu ya bilioni 15 ili kuboresha shughuli mbalimbali za utoaji huduma za benki hiyo; https://youtu.be/6InDAfkTDWM

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars wameshauriwa kucheza kwa kujituma katika michuano ya kombe la Challenge na kurejea na kombe ili kuwafuta machozi watanzania; https://youtu.be/nUS-Akz8fiA

No comments: