Meneja
wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akikabidhi vifaa vya
kufanya usafi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Jeshi
Lupembe ,vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kutekeleza agizo la rais
Magufuli la kufanyika wa usafi siku ya Desemba 9.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jeshi Lupembe akiwa ameongozana na
Afisa afya mkuu wa manispaa hiyo,Mgeta Sebastian wakati wa kupokea
msaada a vifaa vya kufanyia usafi kutoka Benki ya Azania tawi la Moshi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jeshi Lupembe akipokea rasmi msaada
kutoka benki ya Azania uliowasilishwa na Meneja wa benki hiyo ,Hajira
mmambe kwa ajili ya kufanyia usafi.
Meneja
wa Azania Bank tawi la Moshi,Hajira Mmambe akisalimiana na Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jeshi Lupembe alipofika ofisini
kwake kuitikia wito wa rais John Magufuli ya kufanya usafi Desemba 9 kwa
kuchangia vifaa vya kufanyia usafi.
Afisa
afya mkuu wa manispaa ya Moshi,Mgeta Sebastian akisalimiana na Meneja
wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe alipotembelea ofisi za
halmashauri hiyo kutoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi.
Meneja
wa Azania Bank ,Hajira Mmambe akitia saini katika kitabu cha wageni
ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.Jeshi Lupembe
(kulia).
Wafanyakazi
wa Azania Bank tawi la Moshi,wakishusha mifagio ,iliyotolewa na benki
hiyo kwa ajili ya shughuli za usafi zitakazofanyika Desemba tisa mwaka
huu,kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi ,Jeshi
Lupembe.
No comments:
Post a Comment