Wanafunzi
wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakielekea
kupandisha bendera ya Taifa wakati wakisherekea mwaka mmoja wa shule
hiyo iliyopo Chalinze Msolwa mkoani Pwani.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakiwa ndani ya darasa la Komputa
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakijibu maswali ya kuhusiana na komputa katika darasa hilo.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial, Ivonne Mnyitafu akitoa ufafanuzi kwa wazazi pamoja na walimu wa shule hiyo.
Mwalimu
wa Taluma wa Shule ya Sekondari ya Imperial, Peter Mwanda akizungumza
katika siku ya Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo iliyopo
Chalinze Msolwa mkoani Pwani.
Wazazi
wakiwasikiliza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakati wa
kusherekea siku ya Impirial iliyofanyika Shuleni hapo leo.
Wazazi
waliowatembelea wanafunzai wa shule ya Sekondari Imperial wakielekea
katika chumba cha masomo ya Sayansi (Laboratory) wakati waliposherekea
siku ya Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo iliyopo
Chalinze-Msolwa mkoani Pwani.
wanafunzai
wa shule ya Sekondari Imperial wakifanya majaribio ya masomo ya Sayansi
ambayo ni Fizikia pamoja na Kemia katika chumba hicho cha majaribio ya
masomo hayo shuleni hapo leo.
Mkuu
wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup
Mukhopadhyay akitolea ufafanuzi moja ya kifaa kinachotumika kuchuja maji
ambayo yamechanganywa na mchanga mbele ya wazazi na walezi waliofika
shuleni hapo kwaajili ya siku ya Imperial iliyofanyika leo shuleni
hapo.
Mwenyekiti
wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial,Buhela Lunogelo akiwapongeza
kuwapongeza wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kufanya majaribio ya
masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo leo.Kulia ni Mkuu wa Shule na
Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup Mukhopadhyay.
Baadhi
ya wazazi wakichukua kumbukumbu zao (Taswira mbalimbali) wakati
wanafunzi wa shule hiyo wakifanya majaribio ya masomo ya Fizikia na
Kemia katika chumba hicho katika shule ya Sekondari Imperial leo.
Baadhi
ya wanafunzi shule ya Sekondari Imperial wakifafanua somo la hesabu la
pembe zinazoundwa na pembe tatu mbele ya wageni waalikwa na wazazi au
walezi wao (hawapo pichani) waliohudhulia katika siku ya Imperial
iliyofanyika Chalinze Msolwa mkoani Pwani leo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperial wakifanya mdahalo katika siku Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo.
Mwenyekiti
wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial, Buhela Lunogelo akizungumza na
waandishi wa habari leo katika shule hiyo kuhusiana na maendeleo pamoja
na uzuri wa taaluma inayotolewa katika shule hiyo kuwa ni ya kimataifa,
aidha amewaomba wazazi wenye watoto wanataka kusoma kidato cha kwanza
mpaka cha nne wawapeleke watoto wao katika shule hiyo iliyonzishwa Machi
3 Mwaka huu.
Mwenyekiti
wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial, Buhela Lunogelo akiwapa zawadi
wanafunzi wa shule hiyo leo Chalize Msolwa Mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu
wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup
Mukhopadhyay.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperial wakiwa katika picha ya
pamoja wakiwa na vikombe na vyeti vyao walivyozawadiwa leo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperialwakitoa burudani katika siku ya Imperial iliyofanyika leo mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment