Hali imekuwa shwari katika Jiji la Dar es Salaam hasa wakati wa upigaji kura kuwachagua madiwani, wabunge na Rais wa Awamu ya Tano. Jiji hilo lenye pilikapilika nyingi za maisha mfukuto mkubwa wa kisiasa lakini hali haikuwa hivyo bali ilitawaliwa na amani kila mahala. Pichani ni baadhi ya barabara zikiwa hazina misururu ya magari na vyombo vingine vya moto kama ilivyozoeleka.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Hali ilivyokuwamchana wa leo katika barabara za Morocco na Morogoro eneo la Magomeni Dar es Salaam.
Kwenda Kinondoni kutoka Magomeni Mataa
Kwenda Ilala, eneo la Mataa Magomeni
Eneo la Banana Jimbo la Ukonga Dar
Hata wafanyabiashara hawakuwepo Banana, Ukonga Dar.
==================
Wakazi wa Dar Wasimamisha Shughuli Kupiga Kura, Wajitokeza kwa Wingi.
Wananchi na wakazi wa maeneo ya Tabata Liwiti wakiwa katika foleni ya kupiga kura leo jijini Dar es Salaam. |
Wananchi na wakazi wa maeneo ya Tabata Liwiti wakiwa katika foleni ya kupiga kura leo jijini Dar es Salaam. |
Wananchi na wakazi wa Tabata Shule wakiangalia majina yao kabla ya kupiga kura yao. |
Mkazi wa eneo la Matumbi akipiga kura yake leo. |
Mkazi wa Kawe akipiga kura yake leo. |
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
WAKAZI wa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam leo wamesimamisha shughuli zao na kushiriki zoezi la upigaji kura kuchangua viongozi wanaoona wanafaa kwa ajili ya kuwaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Viongozi waliokuwa wakipigiwa kura leo ni wa ngazi ya udiwani, wabunge na nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zoezi katika maeneo mengi ambayo mtandao huu ulitembelea ya Tabata, Ubungo, Sinza, Magomeni, Kigogo, Buguruni, Matumbi, Mwananyamala, Kawe pamoja na Kijitonyama zoezi limeenda vizuri huku idadi kubwa ya wapiga kura wakijitokeza kutimiza haki yao ya msingi.
Maeneo mengi vijana wameonekana kujitokeza kwa kiasi kikubwa huku vituo vingi vikitawaliwa na amani na utulivu katika vituo hivyo. Licha ya changamoto ndogondogo ambazo zilikuwa zikijitokeza kama baadhi ya wakazi kukosa majina yao kwenye orodha waliweza kupewa mwongozo ya nini cha kufanya na wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi.
Ramadhan Mabula ni Msimamizi wa Kituo Kata ya Ubungo akizungumzia eneo hilo alisema zoezi kwa kiasi kikubwa linaendelea vizuri na zipo changamoto ndogondogo ya baadhi ya watu kutoona majina yao lakini utatuzi umetolewa na ofisi za juu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wanaendelea na zoezi vizuri.
Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa vituo vya Kata ya Kigogo, Daudi Chambo alisema vituo vyote 59 vilivyopo sehemu mbalimbali katika Kata hiyo zoezi linakwenda vizuri na hata wananchi waliokuwa wakijitokeza kulalamika kutoona majina yao walisaidiwa na baadaye kupiga kura.
"...Unajua wapo waliokuwa wakilalamika hawaoni majina yao lakini ukifuatilia kiundani unakuta alikuwa akitafuta jina sehemu ambayo sio na aliposaidiwa aliweza kupiga kura na kuondoka," alisema Chambo.
Licha ya idadikubwa ya wananchi kufika vituoni mapema zaidi yaani saa kumi za asubuhi na saa kumi na mbili zoezi limeanza majira ya saa moja asubuhi na wapiga kura kuendelea na upigaji kura huku wakiongozwa na wasimamizi na makalani vituoni. Katika vituo ambavyo vimetembelewa hakuna vilivyokwama kutekeleza shughuli hiyo ya upigaji kura.
Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wa ndani ya nchi wakijadiliana jambo wakiwa kazini katika kituo cha Tabata Liwiti. |
Maeneo mengine foleni zilitembea haraka kiasi cha kumalizika mapema... |
Eneo la Ubungo ambalo muda wote huwa na idadi kubwa ya watu na mishemishe nyingi leo lilikuwa shwari... |
Foleni za wapiga kura eneo la Ubungo... |
Baadhi ya waangalizi wa kimataifa wakifuatilia zoezi la upigaji kura kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam.. |
Foleni ya wapigakura Kata ya Ubungo.. |
Maeneo mengi ya jiji hata yale ambayo huwa yamechangamka leo yalikuwa yamesimamisha shughuli zake na watu kuelekea kutimiza wajibu na haki yao ya msingi ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowapenda. Mwandishi wa habari hizi ametembelea maeneo ya Ubungo, Sinza, Msasani, Kawe, Magomeni, Kinondoni na mengineyo ambapo idadi kubwa ya maduka yalikuwa yamefungwa na hakuna mikusanyiko ya watu hali inayoonesha wamesimamisha shughuli kutekeleza zoezi la kupiga kura.
Tayari vituo vingi vimehitimisha zoezi la upigaji kura na kujipanga kuanza kujumlisha kura kabla ya kutoa matokeo kama taratibu zinavyoelekeza. Endelea kuwa nasi tutakuletea matokeo kituo baada ya kituo kadri tunavyo yapokea.
Maeneo mengine makarani na wasimamizi waliwasubiri wapiga kura... |
Foleni ya wapiga kura Mwananyamala Jijini Dar es Salaam... |
Maeneo ambayo muda wote huwa bize leo hali ilikuwa ni tofauti, yaani yalikuwa kimyaaa kupisha zoezi la upigaji kura... |
Wapiga kura na wakazi wa Kawe wakiendelea na zoezi hilo bila tatizo lolote... |
Wananchi Kata ya Magomeni wakitimiza wajibu wao wa kuchagua viongozi... |
Wakazi wa Segerea wakiwa katika foleni kwaajili ya kuendelea na zoezi la kupiga kura katika kituo cha Magereza Segerea muda huu huku hali ya usalama ikiwa shwari kabisa
Foleni ikiwa bado ndefu huku mwamko ukiwa mkubwa kwa rika zote kuanzia vijana na wakina mama na baba zoezi linaendelea vizuri mpaka sasa
Blogger Josephat Lukaza akiwa katika foleni ya kupiga kura katika kituo changu cha Magereza segerea kwaajili ya kupiga kura kumchagua kiongozi atakayenifaa
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Wakazi wa Segerea ambao wamjiandikisha katika kituo cha Segerea Magereza wakiwa wamejitokeza kwa wingi muda huu katika kituo hiko kwaajili ya kushiriki zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi mbalimbali kuanzia Rais, wabunge na Madiwani. Hali ni shwari hakuna vurugu wala viashiria vyovyote vile vya vurugu japokuwa kuna changamoto za hapa na pale ambapo mkazi mmoja ameambiwa na msimamizi wa uchaguzi kuwa hawezi kupiga kura kutokana na namba ya Kitambulisho chake cha kupigia Kura kutofautiana tarakimu moja tu na Namba ya kitambulisho iliyoandikwa katika karatasi la majina ya kuhakiki. Mkazi huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema kuwa anasubiri Mkuu wa kituo cha Uchaguzi Segerea Magereza kuweza kuongea nae na Kutatua swala hilo endapo ataruhusiwa basi atapiga kura na asiporuhusiwa basi hatopiga kura
Wakazi wa Segerea wakiwa kwenye foleni kusubiri kupiga kura
Baadhi ya wakazi wa segerea wakiwa katika foleni tayari kwa kupiga kura.Picha Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Endelea kuwa nasi hapa tutakuletea kila kinachojiri kwenye vituo vilivyo karibu yetu.
==================
==================
PIRIKAPIRIKA ZA HAPA NA PALE KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA KUPIGIA KURA JIJINI MWANZA.
Ni katika Vituo mbalimbali Jijini Mwanza ambapo zoezi la Upigaji Kura limeenda vyema huku likitawaliwa na utulivu katika vituo mbalimbali vya kupigia kura.
Na:George GB Pazzo
Katika Mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza hakukuwa na foleni za Magari kama ilivyozoeleka na hata shughuli nyingi zilisimama ili kupisha zoezi hili na muda si mrefu mbivu na mbichi zitaanza kujulikana hivyo ni vyema pande zote zikawa tayari kuyapokea matokeo kwani kwenye uchaguzi kuna kushinda na kushinwa.
Zoezi la upigaji kura limetawaliwa na utulivu wa hali ya juu katika vituo mbalimbali huku hamu ya kila mmoja kushiriki zoezi hilo ikiwa ni kubwa pia
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la kupiga kura
Kulia ni Makoye Magige ambae ni Msimamizi Mkuuu wa Kituo cha Kitangiri Kati, eneo la Wazi namba Moja akiw-ongea na Wanahabari juu ya zoezi la uchaguzi katika kituo hicho ambapo amesema kuwa mambo yameenda shwari na hakukuwa na mapungufu makubwa mbali na baadhi ya wananchi kutotambua mapema majina yao yalipo katika Kata hiyo, japo changamoto hiyo imeshughulikiwa mapema.
Mwenye kofia ni Aloyce Mtani ambae ni Msimamizi wa Kituo cha Uchaguzi cha Bismack Jijini Mwanza akizungumza na Wanahabari
Kushoto ni Goodluck Masatu ambae niMtendaji wa Kata ya Kitangiri na msimamizi mkuu wa Uchaguzi katika Kata hiyo akiongea na Wanahari
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Piga Kura kwa Amani
Zoezi la Kupiga kira likiendelea mapema hii leo
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Wenye mahitaji maalumu nao wamepata usaidizi kwa uzuri kabisa
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII.
Kumbuka Uchaguzi Usitutenganishe, Zingatia Amani ndiyo Watanzania wanahitaji.
No comments:
Post a Comment