Friday, October 16, 2015

WAKAZI WA BAGAMOYO WA ENEO LA BANDARI WAFANYIWE TATHIMINI UPYA-RAIS KIKWETE

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
RAIS  DK.Jakaya Kikwete ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kufanya tathimini upya kwa wakazi wa vijiji vitatu wanaopisha bandari ya Bagamoyo.

Dk.Kikwete ameyasema hayo leo  Bagamoyo wakati wa kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ,amesema kuwa wananchi wasiondoke katika maeneo yao wakiwa na manunguniko.

Amesema kuwa mradi wa ujenzi ni mkubwa hivyo wananchi wanatakiwa kupewa haki yake kutokana na eneo ikiwa pamoja na kujengewa nyumba katika kuanza upya kwa makazi ya Kidagoni.

Rais Kikwete amesema mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo umekuja wakati mwafaka kwa kuongeza fursa nyingi baada ya kukamilika kwa mradi huo na kuongeza uchumi wa nchi.

Aidha ameiagiza Mthamini wa Halmashauri  kutafutiwa sehemu nyingine kutokana na kufanya tathimini isiyoendana na malipo hali ya wakazi hao ambao wameachia eneo hilo kwa ajili ya uchumi.

“Nchi haiwezi kuwa safi kuwepo mradi mkubwa wa bandari kubwa Afrika lakini wananchi waliocha eneo hilo wakiwa wananungunika kwa kupuchwa mali zao kwa ajili ya mtu mmoja tu”amesema  Rais Jakaya. 
 Rais Dk.Jakaya Kikwete akizungumza leo  wananchi wa Bagamoyo katika  hafla ya  kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo.
 Rais Dk.Jakaya Kikwete akifungua pazia kwa kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo leo.
 Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza leo  wananchi wa Bagamoyo katika  hafla ya  kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akizungumza  leo wananchi wa Bagamoyo juu ya ujenzi wa bandari ya Bangamoyo. 
Makamu wa Rais Mtendaji wa  Umoja wa Wafanyabiashara wa China, Dk.Hu Jianhua akizungumza katika uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo leo. 
 Sehemu ya viongozi wa waliohudhuria uwekaji wa jiwe la la msingi na uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo  leo.
 Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha na viongozi mbalimbali baada ya kuweka jiwe la msingi na ujenzi wa  bandari ya bagamoyo leo.
Baadhi ya wananchi wa Bagamoyo waliohudhuria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.
( Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya Jamii)

No comments: