Thursday, October 15, 2015

TANROADS NA KAMPUNI YA SUMITON MITSUI CONSTRACTION CO. LTD WASAINI MKATABA KWAAJILI YA UJENZI WA BARABARA YA JUU ENEO LA TAZARA LEO JIJINI DAR

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma risala kwa mbele ya wadau wa ujenzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mara baada ya kukutana na kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly over) eneo la Tazara jijini Dar es Salaam mkataba uliosainiwa kati ya Tanroads na kampuni ya Sumiton Mitsui Constraction Co. LTD ya nchini Japan mkutano uliofanyika  jijini Dar es Salaam leo.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada akizungumza na wadau wa ujenzi walipokutana kusaini mkataba wa ujenzi wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly over) eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale wakiwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada wakisaini mkataba kwaajili ya ujenzi wa barabara ya juu (Fly over)eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wadau wa ujenzi leo jijini Dar es Salaam na kuhusiana na kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly over) maeneo ya Tazara ambao utajengwa na kampuni ya Sumiton Mitsui Constraction Co. LTD ya nchini Japan. 

 
Baadhi ya wadau waliohudhulia mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

MKATABA WA UJENZI WA TAZARA FLYOVER WASAINIWA, JIJINI DAR ES SALAAM.
WIZARA ya Ujenzi imetiliana saini na kampuni Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd kutoka Japan mkataba wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover), katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba huo, Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Serikali ya Japan na Shirika la Maendeleo la JICA kwa miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara inayofadhili hapa nchini na kusisitiza inahuisha uchumi wa Tanzania na kuimarisha uhusiano kati nchi hizo.

“Kusaini mkataba wa ujenzi wa Flyover ya TAZARA ni faraja kubwa kwangu na wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa kuwa ni mwanzo wa ujenzi na  suluhisho la msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam”, amesema Dkt. Magufuli.

Waziri Magufuli ametaja miradi mingine iliyofadhiliwa na Japan kuwa ni barabara ya Mwenge-Tegeta, Mwenge-Moroco na Rangitatu-Tazara ambayo yote ina lengo la kupunguza msongamano na kurahisisha magari kuingia na kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga ameishukuru Serikali ya Japan kwa misaada mbalimbali inayosaidia Tanzania na kusisitiza kwamba Serikali itaitunza miradi hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni Ujenzi wa barabara ya Iringa-Dodoma, Mayamaya-Bonga, Nantumbo-Tunduru, Daraja la Rusumo, Arusha-Namanga, na kueleza kuwa bado Japan imeonesha nia ya kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye sekta ya ujenzi ili kukuza uchumi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale amesema taratibu za kumpata mkandarasi zilianza huko Japan tangu Januari 2014 ambapo zimepitia hatua zote na Mkandarasi Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd amefanikiwa kushinda zabuni kwa gharama za shilingi Bilioni 87.156 na ujenzi wake utadumu kwa miezi 35.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan, Toshio Nagase amesema ujenzi wa Flyover ya TAZARA ni muendelezo na alama ya uhusiano mwema kati ya Tanzania na Japan na mradi huo utapokamilika utakuza uchumi wa Tanzania wa kurahisisha huduma za uchukuzi na upotevu wa muda unaosababishwa na msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa takribani shilingi Bilioni 411 zimekuwa zikipotea kwa mwaka hapa nchini kutokana na msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, hivyo kukamilika kwa ujenzi wa Flyover ya TAZARA itakuwa mwanzo mzuri wa suluhisho hilo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi 

No comments: