Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager kimewasili salama katika mji wa Blantyre nchini Malawi jioni ya leo tayari kwa mchezo wa marudiano siku dhidi ya wenyji siku ya jumapili.
Stars inayonolewa na makocha wazawa Charles Boniface Mkwasa na Hemedi Morocco iliondoka leo kwa usafiri wa shirika la ndege la Fastjet na kuwasili jiji la Lilongwe saa 4 asubuhi kabla ya kuanza safari ya bus kuelekea Blantayre iliyochukua takribani masaa 3.
Wachezaji wote wapo katika hali nzuri kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Malawi siku ya Jumapili ambapo Stars itashuka dimbani kusaka matokeo mazuri yatakayoiwezesha kufuzu kwa hatua ya pili, katika mchezo wa awali uliochezwa jijini Dar es salaam, Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2- 0.
Stars inatarajiwa kufanya mazoezi kesho jioni katika uwanja wa Kamuzu Banda uliopo Blantyre, uwanja ambao utatumika kwa mchezo wa siku ya Jumapili.
Kuelekea mchezo huo wa marudiano, Kocha wa Stars Charles Mwasa amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri kiafya, kifikra na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo.
Katika hatua nyingine mabus mawili yenye washabiki wa Stars Supporter yako njiani kuelekea nchini Malawi kwa ajili ya kuipa sapoti timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mchezo huo wa Jumapili.
No comments:
Post a Comment