Sunday, October 11, 2015

SERIKALI YA JIPANGA KUDHIBITI HOMA YA BONDE LA UFA.

Na Anitha Jonas –MAELEZO
 SERIKALI imeandaa mkakati wa  kuzuia Homa ya Bonde la Ufa (Rift Valley Fever) nchini kutokana na kuwepo na viashiria vya kuwepo na ungojwa huo katika kipindi hiki cha mvua za Eli-nino kama ilivyoripotiwa na Mamlaka ya hali ya hewa.

Ugongwa wa Homa ya Bonde la Ufa ni hatari sana na kwani katika kipindi cha 2006/2007 ulipotokea ulisambaa kwa kasi na kuathiri vijiji 175  kati ya wilaya 11 katika ya Ukanda wa Kati na Ukanda wa Kaskazini Mashariki mwa nchi. 

Hayo aliyasema hivi karibuni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi Dkt.Yohana Budeba alipokuwa akifungua mkutano wa wataalamu kutoka sekta mbalimbali wanaoandaa mkakati wa kupapamba na Homa ya Bonde la Ufa nchini.

“Serikali imeamua kuchukua tahadhari ya haraka ili kuepuka  mlipuko wa ugongwa wa Homa ya Bonde la Ufa,kutokana na kuwepo na taarifa za mvua za Eli-nino,kamati inaandaa mkakati wa kuanza tuoa elimu kwa umma juu ya ugonjwa huu pamoja kutoa chanjo kwa wanyama,pamoja na kuweka dawa katika majoshi ya mifugo kama ngombe,mbuzi na kondoo halikadhalika kupulizia dawa kwa mifugo katika maeneo ya minada”,alisema Dkt Budeba.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma za  Mifugo kutoka katika Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi Dkt.Abdu Hayghaimo alisema Homa ya Bonde la Ufa ni ungonjwa ambao huambukiza kutoka kwa mnyama na kwenda kwa binadamu kwa kula nyama ya mfugo aliyeathirika na ugongwa ,pia husababishwa na aina ya mbu ambao huuma nyakati za mchana .

 “Ninaomba kuwasihi watanzania wote kutoa taarifa katika kwa wataalamu wa Mifugo sehemu yoyote wanapoona dalili kama mimba za mifugo kama ngombe,mbuzi na kondoo kutoka kwani hiyo  ni dalili moja wapo ya  ugongwa wa Homa ya Bonde la Ufa”, alisema Dkt. Hayghaimo. 

Mbali na hayo Dkt Budeba alitoa pongezi kwa Mamlaka ya Hali ya hewa kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa taaarifa zenye kuonyesha ukweli ikiwa  tayari dalili za mvua  za Eli-nino zimeanza kuonekana nchini katika maeneo mbalimbali.

Hata hivyo mkutano huo ulihusidha wadau mbali mbali wa maendeleo nchini wakiwemo CDC,WHO,FAO na UNICEF kwa lengo la kutoaushirikiano wao katika kuisaidia serikali kupambana na ugongwa wa Homa ya bonde la ufa kutokana na mvua za eli-nino kuleta mafurinko makubwa yenye kuchangia kuzaliwa kwa mbu wenye maambukizi ya ugongwa huo.

No comments: