Sunday, October 4, 2015

NHC YAZINDUA UUZAJI WA NYUMBA ZA BIASHARA NA MAKAZI ZA MOROCCO SQUARE,WAZIRI KIRUKI AIPONGEZA NHC KWA UFANISI

Na Francis Dande
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki, amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mpango wake wa kujenga nyumba bora na kuwauzia wananchi kwa ajili ya  makazi na biashara.

Waziri Kairuki aliyasema  hayo juzi  jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua  mauzo ya nyumba  za biashara  na makazi zilizojengwa eneo la Morocco Square,  Kinondoni,  jijini Dar es Salaam.

Aliwapongeza Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na wenzake kwa  kazi nzuri wanayoifanya kwa kiasi kikubwa katika kuleta  uhai na taswira nzuri ya  shirika hilo.

Alisema kuwa serikali inatambua kuwa  makazi  ni jambo  muhimu kwa maendeleo ya taifa, ndiyo  maana imekuwa ikichukua hatua  mbalimbali ili kuwezersha sekta  ya nyumba kuwa endelevu na yenye  tija kwa wananchi  na uchumi wa nchi.

Alibainisha kuwa moja ya mambo yaliyofanyika katika kukuza sekta hii ni kuwa  na Sheria ya Mikopo ya nyumba (The Mortgage Financing (Special Provision Act) ya  mwaka  2008,  iliyoanzishwa  kuweza kuwafanya wadau wa sekta ya  nyumba wakiwemo waendelezaji, wanunuzi wa nyumba  na taasisi za fedha  kushiriki kikamilifu katika kukukuza sekta hii muhimu.

Aidha , alisema tangu kuwapo kwa  sheria  hiyo, tangu mwaka 2008 kumeshuhudiwa benki 19 kati ya  zaidi ya benki 50 zilizopo nchini zikitoa  mikopo ya nyumba kwa  Watanzania, 16  kati ya  hizo zikiwa zimesaini makubaliano na  na Shirika la Nyumba la Taifa ili kuweza  kutoa mikopo kwa Watanzania wanao nunua nyumba zinazojengwa na NHC.

Naibu waziri huyo alisema kuwa  kutokana na  kuwepo kwa  changamoto  ya riba kubwa  ya  mikopo ya nyumbva inayotozwa  na benki mbalimbali ambayo ni kati ya asilimia 18  na 25, serikali itaendelea  kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania ili kuona namna bora ya kuewezesha  benki  kupunguza riba  katika  mikopo ya nyumba ili Watanzania wengi waweze kukopa na kununua  nyumba.

Aliwahimiza Watanzania  kutumia  fursa zilizopo za mikopo ya Benki kununua  nyumba zinazojengwa na NHC, ikiwamo kujitokeza  kwa wingi kununua nyumba hizo za  za mradi wa  Morocco Square ambao una nyumba za ofisi hoteli, makzi na maduka makubwa.

 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mauzo ya nyumba za biashara na makazi-Morocco Square uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande)
 Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
  Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu. 
 Wageni waalikwa.
 Wageni waalikwa.
  Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu. 
 Burudani ya muziki.
Burudani ikiendelea.
  Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.  
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.

No comments: