Na Mwandishi
wetu
Ni jambo la
kawaida kwa mtu yeyote ajira yake inapokaribia kufikia ukomo hufikiria namna
atakavyoondesha maisha yake kwa kutafuta shughui itakayo mfanya aweze
kujiingizia kipato kwa ajili yake na famiia kwa ujumla .
Hivyo ndivyo
ilivyokuwa kwa Dakta Gideon Shoo (pichani katikati) , mwanahabari mwandamizi na mkongwe
ambaye aliamua kuingia katika kilimo hai
cha kisasa ambacho hakitumii dawa za
kemikali kutoka viwandani .
Dakta Shoo
kwa sasa kilimo hicho anakifanya nyumbani kwenye shamba katika kata ya Kerege
wilayani Bagamoyo mkoa wa pwani .
Akizungumza
wakati alipotembelewa shambani na nyumbani kwake na maofisa kutoka Envirocare , asasi
isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na mazingira , hakiza binadamu alisema
kilichomhamisha kuingia kwenye shughuli hiyo ni kutokana na kukulia kwenye
kilimo .
‘’ Kingine
kilichonivuta zaidi ni kwamba nimestaafu . Nikwamba nimestaafu wa maana ya
pilikapilika . Kustaafu kwenyewe labda nisababu ya umri . Tangu nimeondoka
kwenye ajira rasmi mwaka 1987 kwenye
magazeti ya uhuu na mzalendo sijawahi kuwa tena kuwa kwenye na ajira rasmi . Nimekuwa nikifanya shughuli
zangu mwenyewe . Hata pale watu wanadhani nimekuwa kwenye ajira . Hapana
shughuli zangu nazifanya mwenyewe’’ alisema Dakta Shoo .
‘’ Nikasema
mimi nadhani sasa nipumzike lakini kupumzika lazima nipate shughui ya kufanya .
Shughuli hii nilibuni siku nyingi
nilikuwa nasubiri tu wakati wa kutekeleza . Shughuli hii nilibuni mwaka
1993 -1994 nikiwa na malengo labda mwaka 2000 nitakuwa nimeanza lakini haikuwa
hivyo hatimaye nilianza mwaka jana na nikafanikiwa kuhamia huku ‘’ aliongeza
Alisema
kabla ya kuhamia hapo tayari alishapanda miti ya matunda ya kudumu . Kupanda
miti kwa ajili ya kilimo chenyewe na miti yenyewe ni miarobaini na mirusina .
Mwarobaini
ni mti ambao unachangia kuendeleza kilimo cha kisasa ambacho hakitumii dawa za
viwandani :
‘’Mwarobaini
ni dawa na umekuwa ukitumika kwa kilimo nchini India tangu kabla ya kuzaliwa
kwa yesu kristo na hakuna haja ya
kufanya utafiti kwasababu wahindi tayari walishaufanya ‘’ alisema Dakta Gideon
Shoo mkulim katika kata ya Kerege
wilayani Bagamoyo .
Amesema
wahindi wamefanya utafiti kwa miaka mingi sana kiasi kwamba unapozungumzia
kilimo cha kisasa cha kutotumia dawa za kuuwa wadudu za viwandani hakuna haja
ya kufanya utafiti mwingine kwani wahindi walishamaliza .
‘’ Mwarobaini mbegu yake inatoa mafuta ambayo
yanauwezo wa kuuwa wadudu na magonjwa aina 600
. Kwa kiasi kikubwa uchanganyaji wake ni rahisi tu . Mafuta unachanganya
na sabuni ya unga kidogo na kupulizia
kwenye mmea bila matatizo yeyote . Kwahiyo mwarobaini ni mti naupenda na
niliupanda kwa miaka mingi nikiwa na malengo hayo ‘’ alisema .
Mwarobaini
unachofanya ni kufubaza wadudu wasiwe na uwezo tena wa kufanya madhara na pia
wakati huo huo majani yake yanatumika kuuwa vijidudu vilivyoko kwenye udongo .
Kwa hiyo nimehamasika na nakifanya kilimo hiki nikiwa na imani kwamba nitapata
mafanikio na watu wengine wanaweza kuiga .
Kinachomsaidia
pia mkulima huyo kutotumia mbolea ya kemikali ni kwamba mimea iliyoko kwenye
shamba lake majani yake yanapeekwa kwenye chemba ili yaweze kuoza na kupelekwa
kwenye biogas ambapo pia anapata mbolea .
‘’ Hatutegemei ufugaji wakati unapopata gesi kwa
upande mwingine unapata mbolea kwasababu
yale maji yanayotoka kwenye mtambo wa gesi ni mbolea na ndio natumia kumwagilia
mimea na jinsi unavyoona mimea imestawi ni mbolea iiyotoka kwenye mtambo wa
gesi ‘’
Amesema
wakati anaposafisha mtambo kuna mbolea ngumu inatoka ambayo ni chakula cha
samaki ambacho anatarajia kuwalisha wakati akianza kuwafuga .
‘’ Mimi nina
mabwaya ya samaki ambayo sijaweka maji nasubiri kuchimba visima na kujaza maji
nifuge samaki . Kwahiyo unaona kuna mzunguko hapa eneo moja linategemea eneo
linguine ‘’
Amesema
changamoto inayowakabili wakulima ni kutokuwa na maabara ya kupima udongo ambayo
inatoa majibu ya haraka .
‘’ Unaweza
mbolea ukamimina tu kumbe unaharibu . Udongo unakuwa labda potassium imezidi au
imepungua calcium au imepungua phosphorous nakuendelea .
Sasa hivi .
Napeleka Nairobi . Najua watu watasema mbona kuna SUA au Mlingano . Kwasababu
ukipeleka udongo jumatatu siku ya alhamisi unapata majibu . Wako kwenye
biashara na sisi hapa Tanzania sijui kama tunazo maabara ambazo zinafanya
shughuli hiyo kwa namna hiyo . Bado hatujafika huko kuna changamoto .
Amesema
katika kuondokana na changamoto hiyo ameagiza mashine ya kupima udongo kutoka
India na kazi ya kupima ataifanya shambani kwake ambapo hatakuwa na kazi tena
ya kupeleka udongo mahali popote kupimwa .
‘’
Changamoto hiyo nadhani serikali lazima iibebe . Haiwezi kukwepa jukumu lake la
kuendeleza kilimo kwa kuangalia vitu vya msingi ikiwemo pia upatikanaji wa
maji ambavyo vitamsaidia mtu anayetaka kulima katika eneo dogo aweze kuzalisha zaidi badala
ya serikali kukimbilia kwenye matrekta
.’’
Changamoto
ya kuwepo kwa maabara za kupima udongo ambazo zinaleta majibu ya haraka pia
imeungwa mkono na Mkurugenzi mtendaji wa Envirocare bibi Loyce Lema ambaye pia
ameshauri serikali isaidie katika upatikanaji wa maofisa ugani watakaosaidia
wakulima kutambua udongo unaofaa kwa ajili ya kupanda mazao fulani .
‘’ Ni vuri
mkulima akajua udongo wake uko katika kiwango gani na unavirutubisho gani ili
kama vimepungua aweze kuongeza kilichopungua katika udongo . Mara nyingi sana sisi watanzania tunalima tu
kwasababu tu umeona ni udongo . Unaona unaweza kuzalisha kwa hiyo mwisho wa
siku hautavuna chechote .
Kwa hiyo
tungeambiwa udongo wetu una matatizo gani na tukaweza kuuboresha tungeweza
kuvuna sana.
Tunataka
kuiomba serikali itusaidie kutupatia maofisa ugani watakaosaidia kuwaelimisha
wakulima kujua udongo umepungua kiasi gani ‘’ aliomba Bi. Loyce .
Kuhusu
kilimo hai amesema kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kuna mambo mengi
yametokea katika mazingira ikiwemo wadudu kuongezeka kwa hiyo ili wakuma waweze
kuvuna lazima watumie viwatilifu .
‘’ Wako
wachache ambao wanalima kidogo wao wanaweza kulima bila kutumia viwatilifu
. Sasa hivi sisi envirocare
tunahamasisha wakulima kulima hasa majumbani kwao . Wanaweza kulima kwa ajili
ya familia bila kutumia viwatilifu kama tulivyoona nyumbani hapa kwa Dakta Shoo
ambaye ameweza kulima kwa ajili ya familia yake na hata majirani . Ametuonyesha
kwamba ukiwa na ndoo chache unaweza ukalima kwa ajili ya familia’’ aliongeza .
Kwa upande
wake bibi Euphrasia Shayo , Meneja wa mradi wa wiki ya kijani kutoka envirocare
amesema wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii kula vyakua
vinavyotokana na kilimo hai .
‘’ Tumeona
pia magonjwa mengi watu wanapata kutokana na ulaji wa vyakula vinavyotokana na
matumizi ya kemikali zenye sumu kutoka
viwandani . Kwahiyo tunahamasisha jamii iweze kulima bila kutumia dawa au
mbolea ya viwandani ‘’ alisema bi. Euphrasia .
Kitendo cha
envirocare kumtembelea mkulima huyo ni sehemu ya wiki ya kijani ambayo inafanyika kila mwaka
mwishoni mwa mwezi septemba hadi oktoba kwa ajili ya kuhamasisha kilimo hai
ambacho hakitumii sumu ya kemikali kutoka viwandani .
Wiki hiyo
imeandaliwa na shirika lisilo la
kiserikali la Swedish Society for Nature
Conservation ambapo familia
zinahamasishwa kulima vishamba vidogo katika maeneo yao kwa kupanda mbogo
ambazo ni safi na salama na pia kusaidia kupunguza gharama za kwenda kununua
mboga .
No comments:
Post a Comment