Monday, October 19, 2015

MSHAURI WA CHAMA CHA DUNIA CHA MCHEZO WA MPIRA WA KIKAPU AKUTANA NA UONGOZI WA SEKTA YA MICHEZO NCHINI

 Mkurugenzi Idara ya Michezo Bw. Leonard Thadeo (kulia) akizungumza na  Mshauri wa Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) Bw. Lubomir Kotleba (kushoto) alipofika nchini Tanzania kufuatilia maendeleo ya mchezo huo jana Jijini Dar es Salaam.
 Mshauri wa Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) Bw. Lubomir Kotleba (kulia) akizungumza na maafisa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (hawapo pichani) alipofika nchini Tanzania kufuatilia maendeleo ya mchezo huo nchini. Kushoto ni rais wa Mpira wa Kikapu Tanzania Mhandisi John Bandiye.
 Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Henry Lihaya akizungumza wakati Uongozi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ulipokutana na Mshauri wa Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) kujadili masuala mbalimbali ya mchezo huo Jijini Dar es Salaam.
 Maafisa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea kati ya uongozi wa Idara ya Michezo pamoja na Mshauri wa Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) jana Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo

No comments: