Tuesday, October 20, 2015

MAMIA WAAGA MWILI WA DK.EMMANUEL MAKAIDI VIWANJA VYA KARIMJEE DAR ES SALAAM LEO

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia mwamvuli wa Ukawa, Mhe Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo, Dk. Emmanuel Makaidi wakati wa ibada ya kuuaga iliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam leo mchana. Katika ibada hiyo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali walihudhuria.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wananchi wakiwa wamejipanga foleni wakati wakienda kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Ndg. Philip Mangula (kulia), akipeana mkono wa pole na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Freeman Mbowe wakati alipofika kuhudhuria ibada hiyo.
Mjane wa marehemu, Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela akiwa ameinua mikono wakati akimuaga mumewe katika ibada hiyo
Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mtungi, akizungumza kwa niaba ya serikali wakati wa misa hiyo ya kumuaga Dk. Makaidi.
 Geneza lenye mwili wa aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha National League for Democracy  (NLD) Dkt  Emmanuel John Makaidi likiwa limebebwa  kwaajili ya kuelekea makaburini mara baada ya kuagwa leo katika  viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mjane wa marehemu, Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela akiweka mchanga katika kaburi la mumewe katika mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Sinza Dar es Salaam.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa akiweka shada la maua katika maburi la aliyekuwa  Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo, Dk. Emmanuel Makaidi katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania bara, Philip Mangula akiweka shada la maua katika kaburi la Marehem Makaidi yaliyofanyika katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.
 Watoto wa marehemu,Dk.Makaidi wakiweka mashada ya maua katika kabiri la baba yao kwenye makaburi ya Sinza.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Na Dotto Mwaibale
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Profesa Mwesiga Baregu amesema kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democratic (NLD), na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Dk. Emmanuel Makaidi ni kiashiria tosha cha ushindi wa umoja huo.

Mwenyekiti huyo mwenza wa Ukawa, amezikwa leo jioni  katika makaburi ya Sinza jijini hapa, huku yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa Profesa Baregu aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akitoa salamu za rambirambi na kwa wanafamilia, wanandugu, wanachama na wanasiasa mbalimbali nchini walioguswa na kifo hicho wakati ibada fupi kutoa heshima za mwisho Dk.Emanuel Makaidi yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee.

"Tutaendelea kumkumbuka hususani pale ilipokundwa Ukawa kwani alikuwa miongoni mwa wabunge waliodiriki kususia bunge la katiba lililokuwa likiendelea," alisema.


Alisema kuwa kwa sasa nguvu ya Ukawa inaonekana kukuwa waziwazi na kifo chake kina ashiria kwamba katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika 25 mwezi huu umoja huo utashinda.

Msajili wa vyama vya siasa.
Kwa upande wake Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi alisema kifo hicho kimeacha pengo kubwa kwani alikuwa mkereketwa wa mabadiliko katika siasa.

Makamu Mwenyekiti NLD.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti NLD, Mfaume Hamisi, alisema kuwa chama hicho kitaendelea kiukumbuka na kuyasimamia misimamo na mambo aliyoyaamini Dk.Makaidi wakati wa uhai wake.

Mhe. James Mbatia.
Akizungumza kwa niaba ya Ukawa, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo, James Mbatia alisema umoja huo utaendelea kumuenzi Dk.Makaidi na kubainisha kuwa alikuwa akiamini mageuzi na mabadiliko nchini lakini hadi leo hawako nae tena.

Msemaji wa Familia.
Kwa upande wake Oscar Makaidi ambaye ni msemaji wa familia ya marehemu aliutaka umoja huo kuendelea na kazi katika siku hizi chache zilizobaki kuelekea katika uchaguzi mkuu na kuongeza ushirikiano katika chama hicho kwani aliyekufa ni Makaidi na si chama.

Philip Mangula.
Akitoa salamu za pole na rambi rambi, Makamu Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula alitoa pole kwa wanafamilia wanasiasa kwa kuondokewa mwenzao.

No comments: