Thursday, October 15, 2015

MABADILIKO KATIKA UPASUAJI WA UVIMBE WA SARATANI

Dk. Umanath Nayak, mshauri mkuu wa  magonjwa ya saratani ya kichwa na shingo pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti katika hospitali ya saratani ya Apollo Hyderabad nchini India.

Na Mwandishi Wetu,
SEKTA ya afya duniani imeshuhudia mapinduzi yanayolenga kuongeza umri wa kuishi, ubora wa maisha, njia mbadala za uchunguzi, njia bora za matibabu, na pia ufanisi na ubora katika huduma za afya.

 Teknohama imekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya ndani ya sekta hii muhimu. Makampuni yanayohusika na kutengeneza vifaa vya tiba hivi sasa yanalenga katika kutengeneza roboti ambazo hufanya upasuaji kwa ufanisi zaidi bila madhara makubwa kwa mgonjwa.

Kuna matumaini sana katika upasuaji kwa kutumia teknolojia ya Roboti. Teknolojia hii ni ishara ya mapinduzi katika sekta ya afya, na ni moja ya mambo muhimu yanayoongelewa sana katika upasuaji hivi leo. Mfumo wa upasuaji kwa kutumia roboti umeletwa ili kusaidia katika upasuaji mgumu, ambao hufanyika kwa shida, au unaohusisha maeneo ambayo ni magumu kufikika na hatari. Kwa kutumia mikono maalumu inayopatikana katika Roboti hilo upasuaji huo urahisishwa zaidi.

Mikono ya Roboti hudhibitiwa na kompyuta inayoendeshwa na mpasuaji kwa kutumia mikono na miguu. Udhibiti huu ni sawa na ule wa mchezo wa video, maarufu kama ‘video game’ ambao huwezesha upatikanaji kwa usahihi zaidi wa maeneo magumu kufikika ikilinganishwa na njia iliyokuwa ikitumika awali ya  ‘laparoscopic’. Kutumia matundu madogo sana, upasuaji wa aina hii unaweza kuondoa uvimbe uliojificha pasipo uharibifu wa tishu na pia humsaidia mgonjwa kutokaa hospitalini muda mrefu pamoja kupona ndani ya muda mfupi. Teknolojia hii inapunguza hatari ya uharibifu wa mishipa na tishu katika eneo husika.

Upasuaji kwa kutumia Roboti unaweza kutumika kutibu hali mbalimbali kama vile magonjwa ya kina mama (gynaecologic), ikiwa ni pamoja kuondoa mfuko wa uzazi (hysterectomy), kutibu maambukizi kwenye leya ya ndani katika mfuko wa uzazi (endometriosis), uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (fibroids uterine), saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya mfuko wa kizazi, fistula na viungo katika nyonga kutoka nje (pelvic organ prolapsed). Utaratibu wa upasuaji na ushonaji unaweza kufanyika kwa usahihi zaidi kupitia teknolojia hii. Kulingana na huduma ya afya inayoitajika na umri wa mgonjwa, upasuaji kutumia Roboti pia unaweza kusaidia kuboresha afya ya uzazi na kumsaidia mgonjwa uwezo wa kuzaa.

Kwa wagonjwa wa saratani, mara nyingi upasuaji wa aina hii huusisha upasuaji wa  kichwa, shingo, ulimi, tezi dume, magonjwa ya wanawake, kuondoa uvimbe kwenye utumbo (colorectal surgery) na upasuaji unaohusisha nyonga.  

Mfumo huu wa upasuaji una msaada mkubwa kwa wagonjwa ambao wanahitaji upasuaji wa tezi upasuaji unaohusisha kuchana sehemu ya chini ya shingo. Kwa kutumia roboti sasa inawezekana kufanya upasuaji wa tezi bila kuchana shingo kwa sehemu kubwa na bila kuacha kovu inayoonekana.

Dk Umanath Nayak, mshauri mkuu wa wa magonjwa ya saratani ya kichwa na shingo pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti kutoka hospitali ya saratani ya Apollo Hyderabad India ameelezea faida ya upasuaji kwa kutumia Roboti. Anasema kuwa, "teknolojia ya kutumia Robot katika upasuaji itadumu sana kama tunaweza kuona faida nyingi za teknolojia hii ikilinganishwa na njia mbalimbali za zamani za upasuaji. Ni hatua ya pili ya upasuaji kwa kutumia mashine maalumu huku ukiangalia kwenye Skrini ya computer (laparoscopic). Hii itapunguza haja ya kufanya upasuaji wa wazi kwa wagonjwa wenye matatizo ya uzazi "
Anaongeza kuwa, "Upasuaji wa kutumia Robot ni njia mpya ya upasuaji ya isiyo na madhara na inajumuisha upasuaji wa kawaida (Open surgery) na Upasuaji wa kutumia skrini ya computer (laparoscopic). Kwa msaada wa Mikono maalumu ya Robot inayodhibitiwa, daktari anaweza kufanya upasuaji kupitia mikato midogo sana. Teknolojia hii husababisha kutokuwa na makovu makubwa yatokanayo na kukatwa sana, kutokuwepo na upungufu wa damu, maumivu baada ya upasuaji na kupona kwa haraka zaidi ".
Aidha mtaalamu wa magonjwa ya saratani nchini Dk. Harrison Chuwa, anasema kuwa “upasuaji kwa njia ya roboti ni njia kuu ya kufanya upasuaji ambayo itapunguza mapungufu ya kibinadamu na hata kovu la operesheni kuwa dogo ambalo aliweze kufanya mwili wako kuonekana tofauti na ulivyokuwa awali. Faida nyingine ya upasuaji kwa njia ya roboti ni kwamba unahitaji rasimali kidogo ya binadamu ili kufanikisha kazi hii.
Teknolojia ya roboti haipatikani nchini Tanzania, lakini watanzania wengi wanasumbuliwa na saratani za kichwa na shingo na mfumo wa mkojo (mfano. kibofu), uzazi, upasuaji wa utumbo mkubwa, na matatizo mengine wamepata huduma hii mara kadhaa pale walipopata rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali za Apollo nchini India.
Ishara nyingine nyingi bado zina mjadala kwa maana njia hii ni mpya tokea upasuaji wa laparoscopic uanzishwe. Muda unavyosogea, upasuaji kwa njia ya roboti unatarajiwa kuchukua nafasi za upasuaji wa kawaida wa saratani na utakuwa ni msaada na kimbilio kwa wengi wanaoteseka na saratani na mapungufu mengine.  Inaweza tokea siku hapo baadae wakati daktari wa upasuaji amekaa ofisini kwake na anamfanyia mgonjwa operesheni au upasuaji akiwa mbali kwa msaada wa mfumo wa roboti.
Mwaka jana, Hospitali Apollo mjini Apollo Chennai na Hyderabad imefanikiwa kufanya upasuaji mfululizo wa tezi kupitia teknolojia hii. Hakuna shaka kwamba upasuaji wa kutumia Robot ni kifaa muhimu katika masuala ya upasuaji, mchango huu muhimu unajidhihirisha hata katika nchi zinazoendelea.

Kuhusu Hospitali ya Apollo

Hospitali za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Taasisi ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.

Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.

No comments: