Thursday, October 8, 2015

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MADAWATI 200 KWA SHULE YA MSINGI BUYUNI ILALA


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati 200 kwa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Madawati hayo yametolewa na Benki ya CRDB ili kukabiliana na upungufu wa madawati shuleni hapo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati 200 kwa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Madawati hayo yametolewa na Benki ya CRDB ili kukabiliana na upungufu wa madawati shuleni hapo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto) akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 200 kwa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo Chanika katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Kariakoo, Andrew Augustine, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda (wa pili kulia) na Mkuu wa shule hiyo, Maulidi Maliki.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto) akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 200 kwa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo Chanika katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Kariakoo, Andrew Augustine, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda (wa pili kulia) na Mkuu wa shule hiyo, Maulidi Maliki.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Shule Buyuni, Maulidi Maliki, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda na Meneja wa Benki wa Benki ya CRDB tawi la Kariakoo, Andrew Augustine wakipiga makofi baada ya Benki ya CRDB kukabidhi msaada wa madawati 200
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi keki ya maalum ya shukrani Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charle Kimei (kushoto), akikagua sehemu ya madawati 200 yaliyokabidhiwa na Benki ya CRDB kwa uongozi wa Shule ya Msingi Buyuni. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Kariakoo, Andrew Augustine.
 Wanafunzi wakiwa wamekaa katika madawati waliokabidhiwa na Benki ya CRDB.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Buyuni
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akiangalia sehemu ya madawati 200 yaliyokabidhiwa na Benki ya CRDB kwa uongozi wa Shule ya Msingi Buyuni iliyopo Chanika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Kariakoo, Andrew Augustine na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charle Kimei (Katikati) akiwa na Mkuu wa Shule ya Msingi Buyuni, Maulidi Maliki (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Asha Mapunda  (kulia) na Meneja wa Benki hiyo tawi la Kariakoo, Andrew Augustine (wa pili kulia), wakiwa pamoja na wanafunzi wa shule hiyo baada ya kukabidhi madawati 200 yaliyotolewa na uongozi wa Benki ya CRDB. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Dar es Salaam.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Buyuni wakiwa na furaha baada ya uongozi wa Benki ya CRDB kukabidhi madawati 200.
 Sehemu ya madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB.
Madawati 200 yalitolewa na Benki ya CRDB.

BENKI ya CRDB imetoa msaada wa madawati 200 yenye thamani ya sh milioni 20 katika Shule ya Msingi Buyuni iliyopo katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaa ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya huduma kwa wateja wake.
Akikabidhi madawati hayo shuleni hapo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei alisema huo ni mchango wa benki hiyo kwenye sekta ya elimu inayoithamini.
Mbele ya wazazi, Kamati ya shule, walimu na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Dk. Kimei alisema benki yake imechangia pato la taifa kwa kulipa kodi ya sh bilioni 50 kwa serikali huku akisisitiza kwamba lazima wanafunzi wapate elimu bora ili waone umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.
“Mazingira bora ya mtoto kupata elimu ni pamoja na kukaa kwenye dawati… CRDB tumesikitishwa na uhaba wa madawati shuleni hapa hivyo tumeahidi kuendelea kuwasaidia hasa kipindi hichi cha wiki ya huduma kwa wateja wetu.
“Tunarejesha asante kwa jamii tunayoihudumia kwa kutuamini, tumetenda sh bilioni 1.3 tutakazozirejesha kwenu kwa njia mbalimbali, tunasema asante sana,” alisema Dk. Kimei aliyekubali kuwa mlezi wa shule hiyo.
Asha Mapunda aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala na aliipongeza benki ya CRDB kwa kuisaidia serikali kwa njia hiyo huku akikiri kuwepo kwa uhaba wa madawati katika shule mbalimbali zilizo chini ya ofisi yao.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Maulid Chinyanya baada ya kuishukuru benki hiyo alimuomba mkurugenzi huyo kusaidia uzio wa shule kwa kuwa wamezungukwa na makazi ya watu hali inayoondoa umakini wa wanafunzi wakati wa masomo.
Shule ya msingi Buyuni, Ilala ina walimu 39 wanaofundisha wanafunzi 2,054 wanaotumia matundu 20 ya vyoo na madawati 398.

No comments: