Meneja
wa Kiwanda cha bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari, akitoa maelezo kwa
waandishi wa habari waliofanya ziara ya mashindano ya kuonja bia hivi
karibuni(hawapo pichani)
Meneja mawasiliano wa TBL Makao makuu, Editha Mushi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya.
Meneja
wa Kiwanda cha bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari, akitoa maelezo kwa
waandishi wa habari waliofanya ziara ya mashindano ya kuonja bia hivi
karibuni
Waandishi wa Mkoa wa Mbeya wakipata maelezo lutoka kwa Meneja wa kiwanda.
Baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye chumba cha mikutano wakisubiri maelekezo.
Mmoja wa wafanya kazi wa Tbl Mbeya akisambaza vinywaji kwa washiriki wa shindano la kuonja bia kabla ya kuanza.
Washiriki wa mashindano wakiendelea ma zoezi
Washiriki wa shindano la kuonja nia wakiwa makini kugundua aina ya bia iliyomo kwenye grasi.
Mshindi
wa kwanza katika shindano la kuonja bia, David Nyembe kutoka Mbeya fm
akikabidhiwa zawadi na Meneja wa kiwanda cha Tbl Mbeya Waziri Jemedari.
Mshindi
wa pili katika shindano la kuonja bia, Emmanuel Lengwa kutoka ITV
akikabidhiwa zawadi na Meneja wa kiwanda cha Tbl Mbeya Waziri Jemedari.
Joseph Mwaisango akipokea grasi tayari kwa ajili ua kujaribu bahati yake.
Baadhi ya watumishi wa TBL Mbeya wakifuatilia kwa makini shindano la waandishi la kuonja bia.
Mkuu wa usalama wa mahali pa kazi wa TBL Mbeya, Godfrey Kisulilo akiwaonesha waandishi wa habari namna ya kutunza maji.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na uomgozi wa tbl.
Waandishi wa habari Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara katika kiwanda cha bia cha TBL Mbeya.
WAFANYABIASHARA
mkoani Mbeya wamehimizwa kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda cha bia cha
TBL mkoani kwao kwa kujihusisha na biashara zenye mahusiano na kiwanda
hicho ili waweze kunufaika na uwepo wake.
Miongoni mwa fursa zilizopo ni pamoja na kuanzisha viwanda kwaajili ya kusaga unga wa mahindi utumikao katika kutengenezea bia.
Meneja
wa kiwanda cha TBL Mbeya Waziri Jemedari alitoa hamasa hiyo
alipozungumza na wanahabari mkoani hapa kwenye shindano la kuonja na
kutambua ladha ya bia lililofanyika kiwandani na kuwashirikisha
wanahabari kutoka vyombo mbalimbali.
Jemedari
alisema bado wafannya biashara na wakulima mkoani Mbeya hawajaitumia
vyema fursa ya uwepo wa kiwanda hicho hatua inayopelekea wenzao kutoka
maeneo ya mbali kunufaika na fursa hiyo.
Alisema
licha ya mkoa wa Mbeya kuwa miongoni mwa mikoa inayozalisha kwa wingi
mahindi,bado kiwanda hicho kinalazimika kuagiza unga kutoka
Arusha,Iringa,Kibaigwa na Dar es salaam.
“Wafanyabiashara
wa Mbeya bado wamejikita katika biashara nyingine ikiwemo ya kununua
nafaka kutoka kwa wakulima na kuziuza tena pasipo kuziongezea
thamani.Hii inatulazimu kuagiza unga wa mahindi wa dona kutoka mbali
wakati hapa mahindi yanalimwa kwa wingi.”
“Nadhani
hawajatambua uwepo wa kiwanda hiki unavyoweza kuwanufaisha.Hatuwezi
kufungua viwanda vya kusaga unga wa dona kwakuwa tutakuwa tunawanytima
wengine fursa.Sisi tunatengeneza bia,tunahitaji wadau wengine wa
kutuzalishia malighafi za kulisha kiwanda chetu” alisisitiza.
Alisema
kwa sasa mahitaji ya unga wa mahindi wa dona kiwandani hapo ni mkubwa
ambapo jumla ya tani 30 hutumika kwa kila juma moja hivyo ni fursa nzuri
kwa watakaopenda kuwekeza kwenye uzalishaji wa malighafi hiyo.
Alisema
TBL iko tayari kukutana na mfanyabiashara yeyote atakayeonesha nia ya
kuwekeza katika biashara hiyo na itahakikisha inampa mwongozo juu ya
namna gani malighafi inayohitajika na kiwanda inavyopaswa kutengenezwa.
Aliitaja
fursa ya kilimo cha Shayiri kuwa faida nyingine ambayo wakazi wa Mbeya
hawajawekeza ipasavyo kwani hadi sasa kwa mkoani hapa ni wakulima wa
wilaya ya Mbozi pekee wanaozalisha huku kiwanda kikilazimika kununua
bidhaa hiyo kutoka maeneo mengine ikiwepo Sumbawanga mkoani Rukwa.
Alisema
licha yak ampuni kutoa fursa ya kuwawezesha wakulima katika shughuli
mbalimbali za uzalishaji wa zao hilo,bado mwitikio wa wakulima mkoani
hapa ni mdogo mno katika kilimo cha zao la Shayiri wakati soko ni la
uhakika.
Katika
shindano la kuonja bia,mtangazaji wa Mbeya FM David Nyembe aliibuka
mshindi akifuatiwa na mwakilishi wa ITV mkoani hapa Emmanuel Lengwa
aliyeshika nafasi ya pili.
No comments:
Post a Comment