Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikhe Saleh Omar Kabii wakwanza kushoto akitoa maelezo juu ya haki za binaadamu kwa mujibu wa Uislam wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Haki za Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa Dini, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Harusi Miraji na mwisho Jina Mwinyi Waziri Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma na Sheria.(Picha na Miza Othman- Maelezo Zanzibar).
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini maelezo kwa Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekhe Saleh Omar Kabii hayupo pichani katika Mafunzo ya Haki za Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa Dini Mazsons Hotel Zanzibar.
SheikheThabit Nooman Jongo Afisi ya Mufti Zanzibar akiwafahamisha jambo washiriki wa mafunzo ya Haki za Binaadamu katika Ukumbi wa Mazsons Hotel Zanzibar.
Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar).
Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar 01/09/2015.
MASHEKHE na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwashajihisha wananchi kutojiingiza katika makundi yanayoweza kuvunja amani kutokana na kufuatiwa kipindi kigumu cha uchaguzi Mkuu ujao.
Hayo yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikhe Saleh Omar Kabii ambae ni Mgeni rasmini alipokuwa akifunguwa mafunzo ya Haki za Binaadamu yaliyofanyika katika ukumbi wa Mazsons Hotel ya Shangani Mjini Zanzibar.
Amesema Masheikhe na Walimu hao ndio wasimamizi wakuu katika maeneo mbalimbali ikiwemo Miskitini, Madrasani na hata ndani ya Nyumba zao kwani kufanya hivyo ni kutokiuka sheria iliyopangwa katika Nchi yao.
“ Tofauti za dini, jinsia, cheo na Kabila sio njia za ukiukwaji wa Sheria ndani ya Nchi yetu bali ni kutii sheria kwani nijukumu la kila raia,alisema Shekh Saleh Omar Kabii”.
Nae Shekh Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar amewataka Walimu na Mashekhe wenzake kuwamstari wa mbele katika kusimamia juu ya ukumbusho huo kwani kufanya hivyo ni kutekelaza majukumu yao.
Aidha amewataka Masheikhe na Walimu hao kuchukuwa juhudi za hali ya juu na kutumia maneno ya hekima, busara na unyenyekevu ili waweze kufanikiwa malengo waliyokusudia.
Hata hivyo amesema kuwa wakati wanapotoa hutuba zao ndani ya Misikiti na Madrasa ziwe ni zenye kujenga amani kwani kufanya hivyo ni kuzitii sheria zilizowekwa katika nchi yao.
Washiriki wa mafunzo hayo wamesema watayafanyia kazi bila ya kinyongo na kuyafikisha katika maeneo yao kama walivyoagizwa na Viongozi wenzao.
No comments:
Post a Comment