Wednesday, September 16, 2015

ZAIDI YA WATU 500 WANATARAJIWA KUSHIRIKI KATIKA BONANZA LA KUSHEREKEA MIAKA 17 TANGU KUANZISHWA KITUO CHA MAZOEZI CHA HOME GYM


ZAIDI ya watu 500 wanatarajiwa kushiriki katika bonanza la kusherehekea miaka 17 tangu kuanzishwa kituo cha mazoezi cha home gym kilichopo mwenge jijini dar es salaa litakalofanyika juma pili hii ya septemba 20 katika viwanja vya Escape One.

Andrew Mangomango ni mkurugenzi wa kityuo hicho ametanabaisha kuwa maandalizi yote yamekamalika na kusema kuwa miongoni mwa watu watakaoshiriki katika bonanza hilo ni pamoja na vikundi vya Joging vya jijini DSM, vutio vya gym na yeyote atakayehitaji kushiriki katika bonanza hilo.

Miongonui mwa mambo yatakayoshamirisha bonanza hilo ni pamoja na kutembelea hospitali ya palestina  ya sinza jijini DSM na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa sanjari na kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Bonanza hilo litakalofanyika katika viwanja vya Escape One litaanza Mlimani City majira ya saa kumi na mbili asubuhi kwa washiriki kukimbia kwa mwendo wa taratibu pamoja na kutembea kwa kundi linguine.

Akitaja ratiba kwa siku hiyo amesema baada ya kuwasili katika viwanja hivyo saa mbili asubuhi itaanza AEROBICS mpaka saa nne asubuhi na mara baada ya hapo kutakuwa na michezo mbalimbali ksms vilr kuvuta Kamba, kukimbia na magunia, kukimbiza kuku kunyanyua vitu vizito , kutunisha misuli, mpira wa miguu pamoja na Burudani ya muziki,  lakini pia kutakuwa na michezo mbalimbali kwa watoto hivyo kuwataka wazazi kwenda na watoto wao ili kufurahia kwa pamoja.

Bonanza hilo limebeba kauli mbiu isemayo FANYA MAZOEZI KWA AFYA YAKO likiwa na lengo la kuwahamasisha watu wote kushiriki katika mazoezi ili kutunza afya zao.

Kituo hicho cha mazoezi kilichoanzishwa mwaka 1998  kimekuwa na mchango mkubwa katika kujenga na kulinda afya za watu wengi kupitia mazoezi


No comments: