Thursday, September 3, 2015

TAMASHA LA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIKA NA UCHUMI LAWAELIMISHA WANANCHI NAMNA YA KUIMARISHA AFYA YA AKILI

 Mwenyekiti wa Basicneed Foundashon Tanzania, Prof. Joseph Mbatia akizungumza juu ya kula vyakula vyenye lishe bora na kunywa maji ya kutosha kufanya mazoezi ya viungo angalau mara tatu kwa wiki, (kujali afya kila siku kujitambua na epuka vitu vinavyoathiri afya yako) ikiwa ni siku ya pili ya muendelezo wa Tamasha la  mtandao wa wanawake na katiba na uchumi linaloendelea kufanyika ndani ya TGNP jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa TGNP Mtandao Rehema Mwateba akizungumza na wananchi juu ya kujipa muda wa kutafakari maisha yako mara kwa mara na muda wa kulala uwe wa kutosha wastani wa masaa 7 kwasiku  ili kuchukuwa hatua madhubuti kukabiliana na dalili za msongo wa mawazo ikiwa ni siku ya pili ya muendelezo wa Tamasha la  mtandao wa wanawake na katiba na uchumi linaloendelea kufanyika ndani ya TGNP jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Basicneed Foundashon Tanzania, Prof.Joseph Mbatia akifafanua jambo wakati wa Tamasha la  mtandao wa wanawake na katiba na uchumi linaloendelea kufanyika ndani ya TGNP jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Basicneed Foundashon Tanzania, Prof.Joseph Mbatia akifafanua jambo  ikiwa ni siku ya pili ya muendelezo wa Tamasha la mtandao wa wanawake na katiba na uchumi linaloendelea kufanyika ndani ya TGNP jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Emmanue Massaka)

No comments: