Saturday, September 19, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI



Mlemavu wa ngozi mkazi wa Bunda mkoani Mara anusurika kuuwawa baada ya kutekwa na watu wasiojulikana wakati akielekea nyumbani. https://youtu.be/Eossn9mT8QI 
Chama cha mapinduzi mkoani Dodoma chalalamikia hujuma zinazofanywa na wafuasi wa Chadema baada ya kuharibu mabango ya chama hicho.https://youtu.be/WTVGZSHzO7M 
Waziri wa ardhi na makazi William Lukuvi afanikiwa kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu wilayani Ilemela mkoani Mwanza.https://youtu.be/hsTJ6qoClN8
Kanisa la TAG nchini limetoa msimamo wake wa kutofungamana na chama wala mgombea yeyote na kutoa nasaha kwa viongozi wa dini.https://youtu.be/1a_Oc2xZHGk 
Dr.Fenela Mukangara azindua kampeni zake jimbo la Kibamba huku akiaahidi kuondoa kero ya maji kabisa katika mkutano ulio hudhuriwa na wananchi lukuki.https://youtu.be/5FeQ95LAYPY
Mgombea uraisi wa CCM apokelewa jimboni kwake kwa kishindo huku akihaidi kuletea maendeleo na kuwataka wananchi kuungana kwa pamoja .https://youtu.be/dl0YdhIiAzU
Mgombea wa uraisi Zanzibar aomba ridhaa ya kuchaguliwa tena huku akihaidi kupambana na vitendo vya rushwa katika sekta ya afya.https://youtu.be/7tU23PsjslY
Mgombea uraisi kupitia Chadema Edward Lowassa aendelea na kampeni zake mkoani Kagera huku akihaidi kutatua kero za wakulima. https://youtu.be/l47VqMJ0GPw
Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akanusha tuhuma za chama chake kupendelewa katika majimbo ya UKAWA. https://youtu.be/5vMVgkJITNo
Wanawake wajasiriamali nchini watakiwa kutumia muda mwinigi katika manbo ya kuwaongezea kipato na badala ya mambo yasiyo wanufaisha kiuchumi.https://youtu.be/xGK6KDx-jxE
Mgombea Ubunge wa jimbo la Mafinga awataka wananchi kumchagua ili aweze kuwaondolea kero zinazowakabili. https://youtu.be/_xYDv2Mx3m4
Tume ya taifa ya uchaguzi yakutana na wawakilishi wa vyama vya siasa katika semina ya kuvikumbusha vyama vya siasa maadili ya uchaguzi. https://youtu.be/0XfqVoF6jVY
Raisi Kikwete aanza kuendesha viakao vya jopo la watu mashuhuri duniani katika kujadili athari za milipuko duniani.

No comments: