Wednesday, September 2, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE ATUNUKU NISHANI MAOFISA 30 WA MAJESHI

 Baadhi ya Maafisa Waandamizi, Wakaguzi, Wakaguzi Wasaidizi, Stesheni Sajini, Sajini na Koplo wa Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama wakifuatilia masuala mbalimbali wakati hafla ya utoaji wa nishani ya utumishi uliotukuka Tanzania, nishati ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya utumishi wa muda mrefu na tabia iliyofanyika jana (Jumanne Septemba 1, 2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Asha-Rose Migiro (kulia) akifuatilia masuala mbalimbali wakati hafla ya utoaji wa nishani ya utumishi uliotukuka Tanzania, nishati ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya utumishi wa muda mrefu na tabia iliyofanyika jana (Jumanne Septemba 1, 2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna Tarishi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akifuatilia masuala mbalimbali wakati hafla ya utoaji wa nishani ya utumishi uliotukuka Tanzania, nishati ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya utumishi wa muda mrefu na tabia iliyofanyika jana (Jumanne Septemba 1, 2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania, Jenerali Adolf Mwamunyange (kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu na Kamishna Jerenali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Minja wakisoma ratiba ya hafla ya utoaji wa nishani ya utumishi uliotukuka Tanzania, nishati ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya utumishi wa muda mrefu na tabia iliyofanyika jana (Jumanne Septemba 1, 2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu msaafu Joseph Warioba wakisoma ratiba ya hafla ya utoaji wa nishani ya utumishi uliotukuka Tanzania, nishati ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya utumishi wa muda mrefu na tabia iliyofanyika jana (Jumanne Septemba 1, 2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama  Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimtunuku ACP Vincent Mosses Karata nishani ya utumishi wa muda mrefu Tanzania katika hafla iliyofanyika ikulu Jijini Dar Es Salaam jana( Jumanne Septemba 1, 2015).
   Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimtunuku Brigedia Jenerali Jacob Gideon Kingu nishani ya utumishi uliotukuka Tanzania katika hafla iliyofanyika ikulu Jijini Dar Es Salaam jana( Jumanne Septemba 1, 2015).
 Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa majeshi ya vikosi vya Ulinzi na Usalama mara baada ya hafla ya utoaji wa nishani kwa Maafisa Waandamizi, Wakaguzi, Wakaguzi Wasaidizi, Stesheni Sajini, Sajini na Koplo wa Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama wakati wa hafla ya utoaji wa nishani ya utumishi uliotukuka Tanzania, nishati ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya utumishi wa muda mrefu na tabia iliyofanyika jana (Jumanne Septemba 1, 2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
1   Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimtunuku ACP Bakari Namkaa Ndembo nishani ya utumishi mrefu Tanzania katika hafla iliyofanyika jana jumanne (Septemba 1, 2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO).

Na Lilian Lundo
MAELEZO
Dar Es Salaam
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku nishani ya utumishi uliotukuka, utumishi mrefu na tabia Njema maofisa wa majeshi mbalimbali 30.

Kati ya maofisa hao 10 ni kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 10 kutoka Jeshi la Polisi na 10 wengine wanatoka Jeshi la Magereza.
Akiwataja  maofisa waliopata nishani za utumishi uliotukuka, Mkurugenzi wa shughuli za Ikulu Juluus Magore alisema nishani hiyo hutunukiwa kwa maofisa walio hai wa cheo cha Meja kwenda juu kwa JWTZ na kwa Polisi hutolewa kwa Mrakibu au maofisa waandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliotimiza si chini ya miaka 20.

Waliotunukiwa nishani hiyo ni Meja Jenerali Yacub Hassan Mohamed, Brigedia Jenerali Jacob Gideon Kingu, Kanali Fadhil Omary Nondo, Luteni Kanali Ian Alphonce Haule, Kamishina wa Polisi Elice Angelo Mapunda, Naibu Kamishna wa Polisi Samson Manoc Kassala, Naibu Kamishna wa Polisi Rashid Ally Omary, Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Ramadhan Mpinga.

Wengine ni pamoja na Kamishna wa Magereza Gaston Kalamu Sanga, Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Magereza Gideon Marco Nkana, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Augustine Sangalali Mboje na Kamishna Msaidizi Muandamizi wa MagerezaVenant Jacob Kayombo.

Aidha Magore alisema nishani ya utumishi mrefu hutunukiwa kwa maofisa walio kwenye utumishi hai wenye kamisheni wa JWTZ na maofisa waliotangazwa gazetini wa Polisi, Magereza na Idara ya Usalama wa Taifa waliotimiza utumishi wa miaka isiyopungua 15 wakiwa wenye tabia njema ya kuweza kusifiwa.

Aliwataja maofisa waliotunukiwa nishani hiyo kuwa ni Kanali Mary Bayu Hiki, Kanali Msafiri Mtalika Hamis, Meja Bernard Paul Masala Mlunga, Kamishna wa Polisi Valentino Longino Mlowol, Naibu Kamishina wa Polisi Ally KihuriLugendo.

Wengine ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Mboje John Kanga , Kamishna Msaidizi wa Magereza Vincent Protas Marissa, Kamishina Msaidizi wa Magereza Bakari Namkaa Ndembo na Kamishina Msaidizi .

Msaidizi wa Magereza Vincent Moses Karata
Aidha alisema nishani ya utumishi mrefu na tabia njema hutunukiwa kwa maofisa wasiokuwa na kamisheni walio katika utumishi wa JWTZ na wakaguzi, wakaguzi wasaidizi, stesheni sajini, sajini na koplo wa polisi na magereza.

Aliwataja waliotunikiwa kuwa ni Afisa Mteule I Atilio Mgimbe, Sajini Taji Theodat Alfred Banda, Sajini Taji Abdallah Hamad Haji, Mkaguzi wa Polisi Ally Faki Haji, Sajini Meja Charles Andrew Simon, Staff Sergeant Asia Albin Maji, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Rukia Hilary Mopey, Staff sergeant Yasini Abedi Msangi na Staff Sajini Regina Elias Bangu.

No comments: