Thursday, September 17, 2015

NANE WAFARIKI KWA KIPINDUPINDU KINONDONI

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty wapili (kushoto) akiwakabidhi ufagio Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Covenant Balozi, Salome Sijaona, wa pili (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sabetha Mwambenja wakati Uzinduzi wa kampeni ya kupambana na kipindupindu katika Manispaa hiyo ambapo benki hiyo imetoa basi kuwatembeza wananchi waliojitolea kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa Kipindupindu na kufanya usafi, kulia ni Mratibu wa Federation Taifa, Khadija Kingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenant, Sabetha Mwambenja, wapili (kushoto) akimkabidhi gari Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty wapili (kulia) kwaajili ya Wanachama wa Taasisi ya Federation waliojitolea kutoa elimu elimu ya  ugonjwa wa Kipindupindu na kufanya usafi katika Manispaa hiyo (kulia) Mwenyekiti wa bodi wa Benki hiyo Balozi, Salome Sijaona na Mratibu wa Federation Taifa, Khadija Kingi.
Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Covenant Balozi, Salome Sijaona, kwa Pamoja na Mkurugenzi wa Benki hiyo Sabetha Mwambenja(Kushoto) wakikabidhi vinywaji kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty, na Mratibu wa Taasisi ya Federation Taifa Khadija Kingi, Ikiwa ni sehemu ya kuwezesha kampeni ya kupambana na kipindupindu kwa Manispaa hiyo.


NANE wafa kwa kipindupindu kinondoni
Dar es Salaam, 17 Sep 2015... Benki ya Covenant imetoa msaada wa basi maalumu kwa ajili ya kuwasafirisha wanachama wa taasisi ya Federation waliojitolea kufanya usafi na kutoa elimu kwa ajli ya kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu katika manispaa ya Kinondoni iliyoko jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Covenant bank, Balozi Salome Sijaona amesema kuwa benki hiyo imekuwa Msitali wa mbele katika kuisaidia jamii ya Watanzania wasio katika sekta Rasmi ambao kwa kiasi kikubwa ndio wanaoishi katika Mazingira magumu na hatarishi.

“Wateja wetu sisi ni wale wa hali ya chini ambao hawako katika maisha bora, tumejenga misingi yetu katika kuwakuza kiuchumi ila uchumi bila kuwa na afya njema hauwezi kufikia malengo ndio maana tumeona ni vyema sasa kuwaaidia kwa kuwawezesha kupata elimu namna ya kupambana na ugonjwa huo na kuutokomeza kabisa ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuwa na matibabu ya uhakika kwa kuwa na Bima za Matibabu” Alisema Balozi Sijaona.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Sabetha Mwambenja amesema wametoa basi ambalo litatumika kuwafikisha watoaji wa elimu ya afya maeneo yote ya manispaa ya kinondoni pamoja na vinywaji na mahitaji mengine kwa wakufunzi hao wa kujitolea ili kuhakikisha Kampeni hiyo inafanikiwa na kumuahidi Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuwa watakuwa bega kwa began a manispaa hiyo katikamutoaji wa huduma za jamii.

Kwa Upande wake, Mratibu wa shughuli wa  taasisi ya Federation, Hadija Kingi akaiku benki na manispaa kwa jitihada  kuuwanga mkono kutokomeza ugonjwa huo.

Awali, mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Injia Musa Natty alisema idadi  waliokufa kwa Ugonjwa wa kipindupindu katika manispaa hiyo imefikia wanane, huku wagonjwa wanaoendelea kutibiwa wakiwa zaidi ya 356.

Alisema ili kuzuia ugonjwa huo, manispaa hiyo imechukua hatua mbalimbali ikiwamo kuzuia uuzwaji holela wa chakula pamoja na kutoa agizo maalumu kwa wananchi kuzingatia usafi katika maeneo yao ili kuendelea kukabiliana na ugonjwa huo ambao bado umeendelea kutesa wakazi wa maeneo kadhaa.

Mkurugenzi huyo, ametanabaisha hayo wakati akihitimisha mafunzo na kupokea msaada wa basi maalum na Vitendea kazi vilivyotolewa na Covenant Bank, vitakavyotumika na wananchi waliojitolea kutoa elimu na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo ili kutokomeza Ugonjwa huo .

“Kipindupindu ni Ugonjwa unaosambaa kwa kasi sana, tumejitahidi kuudhibiti kwa kiasi cha kutosha na ndio maana madhara hayajawa makubwa sana, pamoja na hilo bado tumekuwa na changamoto kwa kuwafikia wananchi wengi kulingana na wingi wa watu na ukubwa wa Manispaa yetu, hivyo kwa kuzindua mpango huu wa kutoa elimu na usafi kwa wananchi kwa kushirikiana na Taasisis ya Federation na kwa kusaidiwa na Covenant Bank, tunaamini tutaweza kutokomeza Ugonjwa huu, alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza.

“Ugonjwa huu bado upo na sasa tuna wagonjwa zaidi ya 300 ambao bado wanaendelea kupata matibabu katika kanda maalum, na kesi mpya bado zimeendelea kupatikana hivyo natoa wito kwa wananchi licha ya kasi kupungua bado wanahitajika kuendelea kuzingatia usafi na kuepuka kula hovyo pamoja na kunawa mikono kabla ya kula na kila wanapotoka chooni”

Mkurugenzi huyo aliongeza kwa kuwapongeza wanachama wa Taasisi ya Federation  ambao watatoa elimu na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa kwa kujitolea na kutoa  wito kwa wananchi kuwapokea na kuwapa ushirikiano ili kuwezesha kutokomeza kabisa Ugonjwa huo.

No comments: